August 20, 2007

Nikiwa mbali...

Ndiyo nikiwa mbali natafakari sana kuhusu eneo nililopo la LUNDU,nafikiria sana kuhusu kijiji changu.Nakumbuka mengi niliyofanya,burudani,utulivu,upendo na amani,porojo na kila kitu ilimradi siku zisonge mbele kwa furaha,kijijini hakuna msongamano,hakuna vurugu kama mijini yaani raha tupu.

Nikiwa mbali natafakari sana kuhusu kijiji hicho namna ninavyokipenda,nalitzama jua la mawio na machweo katika ziwa murua la Nyasa,ziwa lenye dhoruba kali kuliko yote ulimwenguni lakini likitulia utapenda ndio maana rafiki yangu Mark Wood wa Uingereza,hachoki kuja NYASA,hachoki kwasababu anapenda mandhari yake safiiiii.

Maji salama yasiyo na chumvi kama hilo bahari lenu la hindi,ufukwe haunuki kama huo wa kwenu wa hindi achilia mbali kuwa mchafu ovyo kabisa sijui wamekufa kibudu.

Karibuni sana Nyasa msiogope wageni tunawakaribisha dira yetu ni upendo na amani.
Karibuuuuuu

Fomu za Big Brother ilikuwa moto?

Heee! inaweza kuwa ngeni hata kwangu lakini ndio ukweli kwamba uchukuaji wa fomu za kushiriki katika shindano la Big Brother Afrika ilikuwa moto mkali sana,

Hebu tafakari Salama Jabir(EATV),Tayana(Clouds FM)Witness(Wakilisha) na wengine,ama ilikuwa bonge la ushindani.Lakini mwishowe kijana Richard akaibuka kinara,kwanini?Najiuliza sana hapo, imekuwa dada zangu hao kutoswa?kulikoni hawa waendashaji?Duuu! kwa maana hiyo wanahitaji mtu asiyefahamina au siyo,

Jamani hebu fananisha ujulikanaji wa akina dada hao na huyu mchizi wangu Rich we acha tu yaani maajabu.

Lakini naamini kwamba kijana atafanya zaidi ya mwenzetu 'Mwisho Mwampamba' mwenye bonge la jina la kitanzania!upo hapo...hebu soma jina la mwakilishi huyo wa 2003.

OOh bahati mbaya mwaka huu sijawa mtazamaji kama shindano la kwanza hii ni kutokana na kupoteza kitu fulani katika shindano la mwaka huu,yaani kwa mtaalamu wa vitu aliyeona lililopita 2003 kwa hili ataona kama mdoli tu na ndivyo nilionavyo,maana wamepelekwa wazee watupu tazama umri wao....

aaaah ni porojo tu burudani

Ingia katika tovuti yao ya www.mnetafrica.com

August 19, 2007

Utumwani tena!!!

Mateso ya moyo katika mtumizi ya lugha za kikoloni.Kila siku kuna wasomi wasiojua kitu na ambao vichwa vyao vimejaa nukuuu za kikoloni.

Hakuna jambo lisilofanywa kwa nukuu za kikoloni,mfano unaweza kumkuta mtu akizungumza lugha ya kiswahili huku akichapia maneno mengi tu ya lugha ya kigeni hususani ya kijivuni(kiingereza) maarufu kama 'code mixing','code switching','code alteration' n.k wengi wawasomi wetu wamefilisika kichwani mwao hawana tena uzito unao stahili.Mfano unaweza kuwa na cheti za Uzamili lakini matokeo yake au usomi wako hauwezi kukufanya uwe na maarifa kadhaa hivyo kujikuta ukibabaika sababu ya lugha ya kikoloni huku jambo hilo unalijua vyema.

Wanafunzi wa elimu ya juu wengi wanatumia kitu kinachoitwa "copy and Paste" yaani si hao tu kuna idadi kubwa sana ya vijana tunaotumia silaha hiyo matokeo yake kila mtu anapigana namna ya kufaulu darasani,huko sekondari ndio kabisaaaaa ndipo mauaji haya yanapoanzia.

Kwanini tusitumie lugha yetu yenye kukupa hamu ya kuizungumza?inakupa uwezo wakunyumbulisha,kupambanua na kuelewa zaidi mambo...
Je kwanini tusitumie lugha hiyo(kiswahili) katika vyuo vyetu sasa,hakuna lugha iliyokamilika hapa ulimwenguni.Kiingereza kina maneno mengi ya kuazima toka kifaransa,kilatini,kireno,kiswahili(tazama neno;'safari')utakubali.
Njoo tuungane,kiswahili kina maneno ya kutosha kinachoogopwa eti gharama kubwa; ni ujinga...au nini maudhi ******

BUNGE; Somo la uraia limepotea..

MOYO KABLA YA SILAHA......
Hakuna asiyefahamu kwamba hivi sasa habari za mbunge Zitto Kabwe zinarindima kila kona ya nchi kwani kusimamishwa ubunge imekuwa kama wanachochea nguvu ya raia kukubali kwamba bunge letu limepoteza somo mahiri la uarai.

Hivi tatizo ni lipi hasa hadi tunaogopa kuwa na tume hiyo aliyopendekeza?
kwani kujua ukweli uko wapi kwa porojo za siku hiyo zinaweza kumaliza nguvu za chama tawala? kushushwa hadhi maana yake nini?kwani ukishushwa hadhi unaweza kufa?

Haya mwingine alishatanguliza adhabu kabla hata Big bunge hajatoa uamuzi,bila shaka alipangwa huyo,wazee wetu hawatujali tena ni wakati wa mapinduzi sasa,ewe kijana simama usiogope,umasikini wako si tija bali nguvu zako na hekima zako zikuondoe katika utumwa,pesa si kila kitu bali moyo wa huruma kwakizazi kinachokuja.

Tuache ushabiki kwa suala hili;kwanini mkataba usainiwe wakati Rais alishasema kwamba hakuna kufanyika hilo hadi mikataba mingine ipitiwe upya?Nini maana ya kwenda kusainiwa London? Haijalishi kwamba ilikuwa hotelini au wapi ilahoja kwanini ilifanyika huko?.

Toa maoni..uspitwe
uhuru daima

August 18, 2007

Lundu & karibuni Nyasa: Lundu & karibuni Nyasa: Si Vita,ni kujiweka sawa tu

ETHANOL ni jibu?

Ili kuondokana na Utegemezi wa mafuta,inaonekana kwamba hili lijamaa 'ethanol' ni njia sahihi ya kupata nishati mbadala.

Lakini nishati hii inapingwa na magwiji kama Rais Hugo Chavez,Fidel Castro kwa madai kwamba itasababisha njaa duniani.

Ikumbukwe 'ethanol' ni nishati kwa kutumia mimea hasa mahindi na miwa n.k.Magwiji hao wanapingana na Rais joji kichaka wa marekani kwamba inaweza kusababisha madhara ulimwenguni hasa kutokana na kwamba bei ya chakula itapanda na watu masikini watakosa chakula.
Brazil ndiko hasa 'ethanol'ilikogunduliwa na huku kichaka akitangaza kuwa ni bora zaidi ili kuonmdokana na gharama za nishati ya mafuta.

Je kama Tanzania tuna ardhi ya kulima chakula tunazidi kuomba,tutaweza wakati huo?

Lundu & karibuni Nyasa: Si Vita,ni kujiweka sawa tu

Lundu & karibuni Nyasa: Si Vita,ni kujiweka sawa tu

johari ya matumaini

nimeirudisha hii nikikumbuka nilipoanza kublogu, daaa imenikumbusha mbali sana nakesha nasoma mistari ya NDESANJO kila jumapili. Leo nimeisoma tena si unajua kuhifadhi ukipendacho

Nikiwa Mbeya;kidato cha sita 2005

Ni wakati wa kujiliwaza; kwetu Nyasa

August 17, 2007

HUYU HAPA..

Kwa wapenzi wa filamu lazima wamtambue huyu kijana wa kitanzania ambaye anafanya vitu vyake huko majuu..
Nani huyo?
Ingia hapa...<strong>www.kibirafims.com au www.tzuk.net

Unatafuta kazi....ingia hapa

Kwa wale wanaosaka kazi huko majuu(ughaibuni) na wenye usongo wa kubomoa tamaduni zao kwa masuala mbalimbali,wanaweza kujipatia kazi safi na salama zaidi kama unapenda kazi hizo.
Usipitwe hebu jaribu kuingia katika mitandao ili utimize ndoto zako za kwenda majuu

Ingia hapa haraka......www.myprimejob.com
kuna nafasi nyingi za kazi.

Unayajua maneno haya..

Inawezakana kwamba katika lugha yetu maridadi ikawa inachezewa na watu wasioelewa umuhimu wake.Wengi wanadhani kuongea lugha za Wakoloni ni njia salama zaidi ili kujiunga katikadunia tambarare hii..
Hebu tutazame maneno haya....

KISAGALIMA(vi-)=Ni jembe lililochakaa,kiselemo.

KIPWEPWE=Ugonjwa wa ngozi wenye kutoa madoa mekundu.

KIPETE=Kibahasha

MZAFAFA=Mwendo wa maringo.

NSONO-Tendo la kukoroma.

MNUMAMNUMA=Mtu apendaye sana kutafuta mambo ya uramali,mtukutu,apendaye kuulizia mambo ya uchawi,mshirikina.

MLEO (mi-)=Mwendo wa kupepesuka.

MGALABA(mi-)=Mshindani.

August 16, 2007

Blogu ni nini?

Nimeona ni vyema nikaweka hapa maana ya Blogu ili kuwezesha wengine wajifunze kama mimi nilivyojifunza.

Haya twende sambamba ili tusamabze maarifa kwa wengine.............
"BLOGU" ni neno la lugha ya kikoloni(kiingereza) limetokana na neno "Weblog".

"BLOGU" ni teknolojia mpya inayowezesha mtu yoyote,kikundi chochote au shirika lolote kuwa na ukurasa wake katika mtandao.

Hii ni kama shajara "notibuku" ya mtandaoni kazi yake ni sawa na ya vyombo vya habari mfano Magazeti,Redio,Runinga n.k.Aidha Blogu haihitaji kuwa na gharama zozote maana huduma hii ni bure.Bali kinachohitajika ni muda wako tu kuanzisha Blogu yako tena inakufanya utumie dakika 5 tu ili kukamilisha ndoto zako za kuwa na safu yako.

Hii inakuwezesha kuwa na safu yako mwenyewe kama vile ilivyo kwa wanasafu wa magazetini.Pia inahitaji wewe kuwa na hamu ya mabadiliko ya habari duniani,ambayo huenda mbio mithili ya upepo mkali lakini huu si upepo wa kupita bali ni upepo endelevu........maana hii nimeazima na imetolewa na kufundishwa mara kwa mara na......"Ndesanjo Macha" ;muone katika.."www.jikomboe.com'

Namna ya kuanzisha BLOGU yako.
Ingia hapa; HYPERLINK "http// mwongozo.wordpress.com,http//mwongozo.wordpress.com.

Blogu za kitanzania;ingia hapa; http//tinyurl.com/rwyow