August 29, 2007

Furaha Ni Kitu Adimu

Wengi tunadhani furaha ni kumiliki magari,wanawake wazuri,wanaume wazuri,kazi nzuri,nguo nzuri n.k lakini hawataji hasa kwanini mtu ajisikie furaha.

Furaha si kitu cha kuuzwa ma kununuliwa kama peremende kamwe furaha hailazimishwi bali huja kama anayehiotaji yupo sawa na kweli anahitaji furaha.Furaha si kwenda kanisani kupayuka,kulia,kuogopa mungu atakufa hivyo,kuogopa vifo n.k lakini fauraha haiji kama hitaki kuwa na furaha yenyewe.

Tujiulize kwanini leo Bili Geti anaamua kusaidia watu wa hali chini ambao wanadai kuwa ni masikini wakati ana mapesa,magari,mke mzuri,kampuni za mitaji mikubwa n,k lakini ameamua kusaidia watu wengine.Baaada ya kujikombea feza hizo kwa faida yeye anaamua kutoa bure kwa wengine ingawa suluhisho la kuondokana na hali ngumu si kutoa feza na magari.

Amkeni acheni ujuha,furaha ni kitu ambacho kila mwanadamu anakitegemea kwa mwingine,huwezi kuwa na furaha bila wanadamu wengine,acha rushwa,ubinafsi wape nafasi wngine nao wakupe furaha ya maisha wala haihitaji kununua dawa za kupata furaha kama huko kwa akina joji kichaka wanavyofanya.Furaha ni kitu adimu sana hakiji kwa kutumia nguvu nyingi au mapesa.

Mtabaki Na Labda Hivyo Hivyo

Hivi mbona watu hatujui siku zetu zilivyo hapa duniani?mbona kila raia ana hamu za kijinga hivyo?.

Utakuta kiongozi anahutubia raia wake huku akijifanya anauchungu na hali zao ngumu kumbe anaomba apewe nafasi ampeleke kimada wake ughaibuni kwenda kuzubaa na kushangaa shangaa na kuzunguka kama tiara.halafu akirejea anakuta raia wake wanazidi kuteketea na hali ngumu ya maisha,mwishowe nabaki na labda mungu,labda mizuka na nini uji**** mwingi tu.

Kujali maisha ya wengine hakuhitaji gharama au kuwa tajiri na kumiliki kampuni kama mabwanyenye au mabepari uchwara.hakuhitaji kuwa na mapesa mengi ambayo haywezi kukufanya kama ulivyo.
hivi labda sijui,huenda...m.k hazitaisha bila kutumia muda wetu kupanga huruma na raha kwa wengine.

Acheni Dhihaka

Kama hasira ni mbaya basi bora ziendane na tukio halisi,na kamwe siwezi kuacha hasira za na uchungu moyoni kama TUPAC SHAKUR,BOB MARLEY,J.K NYERERE n.k kwani kama watu hawa walipigani kuondoa unyonge wetu,halafu sisi kwa kujifanya kuja tunakaribisha tena unyonge ambao wenzetu walipigani uondolewe.

Yaani hatuna jeuri kabisa,kila kukicha eti lazima kuongea kiingereza au kuheshimu lugha hiyo kwa kuwa ya kimataifa,hivi mataiafa gani?.Ninaposoma vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiswahili nafarijika na kujihoji kwamba hivi wanaojifanya wasomi leo mbona hata msamiati mmoja wa kiswahili hawajui?Ilikuwaje Biblia ikatafsiriwa kwa kiswahili na kueleweka namna ile?

Mbona kamusi yetu ina maneno mengi tu yanayoashoria kwamba tuko zama sahihi ikiwa tutaamua kutumia lugha yetu? kwani maneno mengi ya kiingereza mbona yanatokana na lugha ya ya kikabila iliyozungumzwa zamani ya kibritaini pale visiwani uingereza halafu leo tunasema ya kimataifa na kimawasiliano.Kwani kiswahili si lugha ya kimawasiliano,acheni dhihaka nyie ****** wana wa kizazi cha wajivuni mbona wazee wetu waliamini miaka hii ndiyo ya kuruhusu lugha yeu kwani wakati ule walibanwa nbavu na hao wanaofanana na rangi ya ngozi ya nguru****?

Hisia toka moyoni;wakati ndio huu.Daahhh! nilitamani kutwanga ngumi mtumbwi wa mvuvi mmoja juzi baada ya kujidai anayajua maneno ya akina blea.lakini nikaona hii mbaya nikatulia na ghadhabu zangu na kumwambia acha dhihaka ndugu yangu mbona Wachina wanaongea kikwao na wanafanikiwa?

Tunadharau kiswahili..

Niliposoma makala inayozungumzia kiswahili katika gazeti moja leo hii baada ya kuingia toka kijijini Lundu,nilikuta natamani kutwanga ngumi ukutani,nilahamanika ile mbaya kwani nikaona watu wote hapa wilayani Mbinga kama vimulimuli.Makala inazungumzia namna Watanzania tunakidharau na kuona kiswahili kama lugha isiyo ya kisomi,ya kishenzi,mbovu,haina maana n.k

Lakini ukitazama hao wanaojiita wasomi eti kwa kuwa wanajua maneno kadhaa ya lugha ya kikoloni ni majuha na watumwa namba moja kuliko wale wasiosoma hapa ulimwenguni.Kwani utawakuta wakiamini eti Kiingereza ni lugha ya kuwasiliana! heee sasa kiswahili ni lugha ya kufanya nini nyiwe watumwa?,Usomi gani hata matumizi ya lugha yenyewe yanwashinda halafu muwe wajivuni?

Wengine hata sarufi maumbo,miundo,na matamshi hawajui matokeo yake hujifanya eti wanashindwa kuongea vyema kiswahili au nini sijui huko, yaani ******** hamna adabu kabisa hivi mnafikiri usomi ni kuja kiingereza na kubetuanetua midomo kama joji kichaka? mlaani***tena mpotee kabisa.

Usomi gani wa kuwa mambumbumbu wa wa lugha yako ya asili,usomi gani huu kama si mauaji ya fikra.Ndio maana tunasema kwamba eti wasomi wa siku hizi hakuna kitu,hivi mnadhani ni nini kama si hiyo lugha yenu ya midabwada.Wengine eti hujifanya kuongea na kuchanganya maneno ya kiingereza na kiswahili.Hilo nasema mko*** kabisa,mtaendelea na utumwa huku wenzenu wakitamani lugha hii ingekuwa yao maana wanaiendeleza sana.

August 26, 2007

:Kushushwa hadhi maana yake nini?

Karibuni Nyasa: Kushushwa hadhi maana yake nini?

Haya wamekwenda kuagua Buzwagi.

Inawezekana kama mzaha lakini ndiyo ukweli wenyewe maana kila siku ni za magonjwa tu.
ziara imekuwa zogo,inafunika kile kinachozungumzwa na kilichosababisha jamaa kuondolewa kule kijiweni kanda ya kati.

Kuna matatizo kule hivyo inaonyesha bora kwenda kuagua ili angalu kuponya na kuzimisha moto wa wenyewe na kuwaonyesha meno 32 na kwa vyovyote wasahau kwa vijijengo vyao vya laki moja kama viota vyipwa baada ya kuondolewa kwenye makasri yao ya maana.
salamu zao haa nilipo ni mbali na mako yetu,kwasabau huku nyasa tumezoea kuvua samaki mfano ngorokoro,perege,mandongo,kambale,mbasa,manswena,ntaka n.k.
lakini tunashukuru tunashiba sijui hao wenzetu huko Buzwagi washiba hivyo vijumba vyao maana naona kila siku natumiwa taarifa huku kijijini kwangu na marafiki waliopo mjini eti jamaa wamejengewa viota ili wahame na mali itegulishwe uchumi. samahani huku kwetui tunakula hata mlenda,kisamvu,matembele lakini hatuna dhahabu sijui ingekuwaje;maana wanyasa ninavyowajua! wangewangiwa kama huko kwenye madini?

August 24, 2007

Simon Regis ni nyota angavu

Nimekuwa nikijiuliza huyu bwana kwanini anouwezo wa kuchora namna hii.kumbe ni mazoezi na bidii ya kutunza kipaji chache.Yaani huyu bwana anachora picha ambazo kwa mtu makini anaweza kudhani ni mashine tu kumbe ni mkono wake wa kuume ndio huo unaofanya kazi yote hii.
kama unabisha hilo jaribu kuingia katika sehemu moja upande wa kulia hapa inaitwa kwa lugha ya kikoloni OLDER POST halafu tazaqma picha ya kwanza aliyotuma kwangu,yaani mchoro fulani hivi wa SADC-sijui ndio mdudu au ni mdomo wa wakoloni.
Mtazame katika blogu yake ya..........
regiscartoon.blogspot.com

Karibuni Nyasa: Kushushwa hadhi maana yake nini?

Karibuni Nyasa: Kushushwa hadhi maana yake nini?

Karibuni Nyasa: Kushushwa hadhi maana yake nini?

Karibuni Nyasa: Kushushwa hadhi maana yake nini?

Unampenda nani...

Wako watu wanaosemekana wanampenda mungu wao na wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya mungu huyo.Wanabeba tabasamu wakati mwingine utadhani mungu kawaambia kwamba ni wao pekee watakao uona ufalme wake(sijui uko wapi).

Jambo la ajabu watu haohao wanaweza hata kuchukia ndugu zao na kumpenda mungu wasiyemuona eti kwamba yeye anaouwezo wa kumwona yoyote.Wanatenga binadamu wenzao kwa misingi ya imani zao,itikadi zao juu ya dini.Uadui unakuwa mkubwa kwasababu wanamtetea mungu ambaye hata siku moja hajaweza kuwaambia wamtetee.

Hoja kuu hapa ni kwanini watu wanaweza kumpenda sana mungu halafu wanahukia hata ndugu zao waliozaliwa nao tumbo moja?Mungu atawapa thawabu kwa kuonyesha jeuri na ujivuni kwamba wanazo imani tosha? binadamu tunapaswa kupendana bila itikadi za imani za dini au vinginevyo tunahitaji kuwa katika njia moja ya kuombeana lakini utakuta madhehebu mbalimbali yanahuburi ujinga na kuwalisha waumini wake ujuha tu.
amani na upendo kwa wote bila kujali imani ya dini ni muhimu sana kwa binadamu

Kushushwa hadhi maana yake nini?

Hivi kuna hekima gani kudai haki ya kushushwa hadhi hapa ulimwenguni?kwanini tunazungumzia kushushwa hadhi katika masuala muhimu ya nchi?
Utakuta kiongozi au raia fulani akidai kwamba ameshushwa hadhi..halafu anaidai hadhi hiyo kama kitu chochote mano wa pipi au kijiko h asukari.

Kama kuna anayebisha basi awatazame viranja wetu kule kijiweni kwao Dodoma,awatazame walivyo na nyuso kama yuda kwa kudai kwamba wameshushwa hadhi,hivi sijui hadhi ni mdudu gani huyu.Halafu hoja kuu inageuka mkuki kwa nguruwe na huku shangwe zikimiminika kama wachanganyaji wa saruji sehemu za ujenzi.

Hivi kuna kifo hochote ukikosa hadhi? kwani hadhi maana yake nini?kwani kuna hadhi inayolindwa na sheria za nchi hii?.Sitaki ushahidi hapa ila viranja wetu ni kama wako chekehea au kama kanbi za mahujaji maana ni porojo na uwongo mwingi ndio ajenda za siku zote.
Amka kijana,nhi imevamiwa na wakimbizi wazaliwa wa nhi yenyewe.