September 05, 2007

Unakumbuka 'inshu' ya Dito au umesahau

Jamaa hapa ananidokeza ndogo ndogo za mjini Mbinga na maeneo mengine ya nchi hususani Darisalama eti kuna jamaa wandai haki katika kesi zao kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa wa m******** ya kijana wa daladala huko Darisalama,ndugu Dito mzuri.

Jamaa wanaona kesi yao haitendewi haki hivyo wanatumia jina la Dito angalu kudai kile wanchoita haki.Lakini hivi haki ni nini hasa?mbona watu wanalalamika sana suala hilo.
Inawezekana kuna namna ambayo kila raia anapaswa kumiliki haki hiyo hata hivyo imetoweka na kuchukuliwa na watu mithili ya dito,mimi sijui maana kazi yangu kuvua samaki kwetu nyasa lakini suala la sheria namwachia Ndesanjo anajua hizo kesi ni nini.

Hta kama atabeza kazi kwake maana ye' ni mwanasheria mahiri tu.kama humjui hebu zama hapa www.jikomboe.com

Tufunge na Kuomba Mungu...

Ndiyo tunalazimika kusali sala za imani yoyote ili kuwawezesha waqvuja jasho wetu wa Taifa Stars kushinda mechi yao a mwisho dhidhi ya Wamachina toka Msumbiji.Yaani tunahitajika kuwa na moyo wa chuma kwelikweli ili tushinde.

Sala zetu ziwe na haja ya kupata magoli 3 kwa nunge kwani wale jamaa kule Senegali lazima watakataa kuadhibiwa idadi kubwa ya mabao lakini tunahitaji sala za maombezi kwa wote Rastafarian,wakristo,wabudda,waislamu n.l ili mradi tuwe na lengo moja tu la kushinda mchezo huo.

Tulia kwa dakika 5 tu omba kadiri uwezavyo angalau uwe na moyo wa huruma kwa vjana hawa wanaoteseka kwa kuweka rehani mioyo yao ili wapate ridhiki ya maisha.

Hapa nilipofika leo Mbinga kuna watu tokana na baridi+Taifa Stars=kihoro na homa matumbo zimejaa tele kumbe watu wanaugulia mechi hiyo,wanajiuliza itakuwaje yaani hata maofisini mambo ni hayo hayo.
uhuru daima

Tanzanite Inaitajirisha India!

Tanzanite inachimbwa Tanzania na inapatikana hapa pekee,lakini habari toka India zinaseama madini hayo yamewezesha ujenzi wa viwanda 15 nchini humo.Viwanda hivyo vinajihusisha na uchongaji,utengenezaji wa bidhaa zinazohusu madini pamoja na usambazaji dunia kote!!!!!

Kitabu cha orodha ya makampuni cha India kinaeleza kuwa makampuni hayo yapo katika miji ya Jaipur,Jimbo la Rajastham nchini humo.Majina ya makampuni hayo ni Gems,Pankas Gems,Sumati Gems,Daga Gems,Vidhan Gems na Ghoshi Export n.k yaani ayko mengi mno kifupi ni hayo.

Najua utashangaa nimepata wapi wakati hapa kwetu Nyasa habari tunategemea Redio za Malawi,Redio za Tanzania ambazo ni chache tu.Lakini habari hii nimeiona leo hapa Mbinga mjini bwana maana leo nilipania kuja mjini kujionea shughuli za walioelimika.Acha tuendelee kuvua samaki huku tukidumisha utamaduni wa nidhamu.Yaani nimestaajabu hata ikirejea nyumbani Yule mzee wangu(baba) mwenye hasira na kutowaendeleza wananchi sijui atasemaje.

Lakini hali hii si njema kwani hata Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki aliwahi kuwaambia wasomi wetu pale chuo kikuu Mlimani 'waone soni'kwani madini hayo yanainufaisha sana nchi yake.Hii niliambiwa na rafiki yangu wa palepale,hivyo usishangae kuwa kwangu kijijini LUNDU hapa nikashindwa kujua huko mjini mnafanya nini.
Jamani mimi napata mfumuko wa hewa(pulesha) maana hali hii si njema.
uhuru daima amka mwana wa Tanzania,wakati ni huu

September 03, 2007

Jumatatu hii ninaanza na hasira

Kuna jamaa wanapenda sana kuchezea muada wa watu.Lakini ukiwaambia kwa lugha ya kikoloni kwamba "Mastering;Time Management"wanadhani jamaa anajidai eti kasoma..sivyo ila ni lazima kuzingatia muda wako la sivyo utajikuta kila kitu harijojo.

Ndio maana mwanablogu freddy macha anasema kuna watu hawana nidhamu hususani sisi vijana.Yaaani hata salamu hakuna,ndio utamaduni wawapi huu,unatokea wapi huu eeeh.

Lakini siku ya leo nimeanza kwa kupotezewa muda na watu wasio kanuni maana wanaishi kama wapo hekaluni wakati hata huko hekaluni kuna kanuni sasa hivi jamaa linanipigia simu sijui nini wakati anajua wazi kuwa hapa kwa wanyasa ni mvumo waziwa tupu.Kama sauti kubwa basi ujue kuna ngoma mahala tena utasikia watu wanasema kuna kipaimara na ukatakumeni n.k
sijui kuishi bila kuwa kanuni na miiko inakuwaje hivi wenzangu mnasemaje hilo

September 02, 2007

Hata iwe vipi,maarifa yapo popote

Haah! acha tu nishangae kwani kuna mambo yanyoendelea katika sayari hii ya dunia ni ajabu kabisa..hebu tafakari hujamuaona mtu wa karibu yako ambaye ni rafiki yako halafu ukisikia yupo karibu hapo utafanyeje.bila shaka ni faraja tu.
Haya achana na hilo kuna hawa jamaa nawaona kama wakombozi hebu watazame kwanza.

http://www.bongocelebrity.com/

http://www.uchambuzi.wordpress.com/

http://www.saidiyakubu.blogspot.com/

http://www.harakati.blogspot.com/

http://www.blog.mirecipe.com/

http://www.freddymacha.blogspot.com/.

Ya pili kutoka chini kwenda juu ni ya dada mmoja hivi machachari sana.
Hebu burudika humo ndio maana nasema kuna watu wana mambo mazito kwa watu makini,na wengine wote wa Tanzania kwani wote ni ndugu.

September 01, 2007

Uwongo si Mzuri..

Kuna jamaa hapa kanichezea sana,yaani nilijikuta natamani kumeza samaki mbichi kabisaa,unajua ni samaki gani 'mbasa'.Usishangae kwani huwezi kula samaki mbichi mpaka achomwe au kupikwa?

Jamaa kaniahidi kuniletea kitabu fulani hapa lakini matokeo yake hajaonrkana kwa kinyume na muda tulioahidiana wa saa 4,yaani nimengojea hadi saa 5 kasoro hivi jamaa haonekani.Aaaa nikaona huu sasa ni ujuha ngoja niongee na watu hapa kidogo lakini sina hasira naye kabisaa moyo uko safiiii....lakini si vizuri kudanganya kama masikini wa siasa na dhiki za siasa au vipi
u kwa vile mimi napenda sana vitabu na anajua kwamba nachukia sana uwongo...ananifanyia kusudi.

Aaa ndio huyu sasa anakuja huku mimi naandika waraka huu,eti anasoma..jamani ananikaripia,kwani mikono yake.....haya leta kitabu we' mbuni mnyasa feki maana jamaa anajiita mnyasa kumbe ....

August 31, 2007

Barua Ya Sekunde Moja

Jana nilikuwa karibu naandika ujumbe kwa watu mbali mtandaoni,lakini nakuambia nilistajabu mtu ninayemwandikia alikuwa kakaa karibu na kompyuta yake bwana naye akaanza kujibu hapo hapo wakati mimi nilikuwa naamini naandika barua ili nijibiwe kama ilivvyo posta mara anuani,kulamba stempu,kushika wino,kununua karatasi n.k

Acha bwana Fred Macha akajibu hapo hapo,ee nikashangaa mzee wangu kumbe yupo nami muda huu toka London.yaani kaacha kulicharaza gita halafu anapiga gumzo hapa? Gumzo hilo si lile la kulonga kimahaba "chat" katika mtandao bali unaandika barua kama unamwandikia baba,mama,kaka,dada,binamu n.k huku ukikaa miezi sita au wiki kadhaa kusubiri majibu,lakini jana nikajibiwa kwa sekunde moja.Yaani ilikuwa saa moja na dakika tano usiku halafu kanifahamisha kwamba yeye pale London ni saa 11 jioni yaani walikuwa wajidai mitaani tu huku wabongo tunajificha ndani kuogopa wakora...kisha kuamka siku inayofuata kwenda kutafuta mkate.

acha kabisa barua za sekunde moja hizi

Haya Wananchi Kazi Kwenu

Ndiyo wananchi sasa kazi kwenu maana kila kukicha serikali yenu inataka kuwahudumia kwa njia bora.sasa ni zamu yenu kuwahudumi wakuu na mamwinyi ukijumlisha na mabwanyenye.

Tovuti ya wananchi ndiyo hiyo ipi hewani msipotoa maoni kazi kwenu,lakini kweli maoni haya yatamfika mkuu wenu,msihofu kila kitu anakijua sana tu.hakuna haja ya kushangaa,toeni hoja,dukuduku,ushauri,na kila kitu chema kwa nchi yenu kwa kuwahudumua wote eehh sasa ingieni katika tovuti hii

www.wananchi.go.tz

Da' Maria karibu

Kupiga gumzo mtandaoni ni raha sana,basi jana nikaanza kuandika ujumbe kwa dada Maria Mtawali..sijui yuko wapi siku hizi hasemi mahali alipo labda ananiogopa.Nikawa naandika ujumbe kadhaa kwa ajili yake...mara nikakuta ujumbe unaoniuliza 'nyasa' ni nini? halafu...'wewe ni mnyasa?' duuh! kufikia hapo nikaona sasa dadangu amenikuana sana anaponiuliza kuhusu nyasa.

Ndiyo..tunavua samaki aina tofauti,kwanza hata wengine hawajui hata nikisema samaki ndio nin..si hiyo misangara yenu ila mandongo,kambale,ngorokoro n.k au waulize wale wazungu kule Liuli wanafanya nini,kisha njoo makao makuu yangu hapa LUNDU niambie unataka samaki wa aina gani au unataka mihogo ya kutafuna ambayo huko ughaibuni wengine wanasikia tu hewani.

Lakini dada maria miye ni toto la kinyasa yaani usijaribu yaani nakupenda nyasa kwangu hapa,kwani nguvu za kukaa katika kompyuta wananipa wao.Jana nilikula sana samaki kutoka mtera halafu nikabeza hawana hata harara kwa mwenye njaa.
Da' maria mi ndio mwenyewe nipo nimetulia nakukaribisha.....njooooo...katika darasa la Ndesanjo hili tujidai mpaka basii

Upweke mmhh

Jamani wakati mwingine huwa najichekea peke yangu au nikimwona mtu ninaye mfahamu huu napenda sana utani matokeo yake naambiwa nina tatizo la kisaikolojia.Hivi unajua kwanini?. Mara nyingi nakuwa mpweke sana yaani napenda kuwa sehemu tulivu mno.

Huwa naongea peke yangu mara nyingi tu huku nikitoa nafasi kwa ubongo wangu kufanya kazi sawa sawa si unajua tena mambo ya kuvua samaki nyavu inapaswa kuwa salama muda wote..
Acha bwana yaani najiona bonge la mjanja nikiwa pekee halafu nikikutana na washkaji naambiwa oooo nina ugonjwa sijui nini huko...

Hivi unavyonitazma kweli unaweza kuamini eti nina unini sijui.. ...sawa lakini napanga mikakati ya kuikamata nchi yaani kuwa rais halafu Ndesanjo anakuwa waziri mkuu,kisha Fred Macha naye anakamata wizara ya utamaduni..ili acharaze vyema gitaa lake...aaa sijashau bwana Michuzi anakama wizara ya sheria ili asiibiwe tena wahuni toka Nigeria maana wataiba hata *****za ndani jamani si fujo hizo hebu lete fimbo jamaa kaandika neno la minyotanyota kibao hapa nani huyu alaa.