September 09, 2007

Asanteni 'TAIFA STARS' Safari Ndiyo Imeanza!!!!!!!

Naam kwa jasho jingi lililowatoka,toka mwanzoni mwa michuano hii.Hakika mnastahili pongezi kwa kazi nzuri.Kzi yenu ilikuwa ngumu,na mara nyingi ninamini kwamba huko ni kuwabebesha msalaba wa dhambi kwa uonevu.

Asanteni kwa kazi nzuri mliyoifikisha hadi wakati huu,hakika sina cha kuwalipa zaidi ya kuwashukuru kwa kazi yenu nzuri.

SASA kazi ndiyo imeanza,wakati ndiyo huu wa kudhihirisha kwamba mnaujua vilivyo mchwezo wa kandanda bila kujali matokeo yetu ya kipindi hiki.

Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa sana achilia mbali wakati huu,pia tunawakaribisha wadogo zetu 'serengeti'{chini ya 17} ili kuweza kujifunza kukabiliana na soka la dunia hii.Hakika hili ni soma tosha na ulikuwa ni mtihani mkubwa wa vijana wenzangu,hawa.
kama mtihani huu ndiyo jaribio la kwanza katika ulimwengu wa kabumbu.
KAZI NDIYO IMEANZA STARS HAKUNA KULALA.

September 05, 2007

Unakumbuka 'inshu' ya Dito au umesahau

Jamaa hapa ananidokeza ndogo ndogo za mjini Mbinga na maeneo mengine ya nchi hususani Darisalama eti kuna jamaa wandai haki katika kesi zao kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa wa m******** ya kijana wa daladala huko Darisalama,ndugu Dito mzuri.

Jamaa wanaona kesi yao haitendewi haki hivyo wanatumia jina la Dito angalu kudai kile wanchoita haki.Lakini hivi haki ni nini hasa?mbona watu wanalalamika sana suala hilo.
Inawezekana kuna namna ambayo kila raia anapaswa kumiliki haki hiyo hata hivyo imetoweka na kuchukuliwa na watu mithili ya dito,mimi sijui maana kazi yangu kuvua samaki kwetu nyasa lakini suala la sheria namwachia Ndesanjo anajua hizo kesi ni nini.

Hta kama atabeza kazi kwake maana ye' ni mwanasheria mahiri tu.kama humjui hebu zama hapa www.jikomboe.com

Tufunge na Kuomba Mungu...

Ndiyo tunalazimika kusali sala za imani yoyote ili kuwawezesha waqvuja jasho wetu wa Taifa Stars kushinda mechi yao a mwisho dhidhi ya Wamachina toka Msumbiji.Yaani tunahitajika kuwa na moyo wa chuma kwelikweli ili tushinde.

Sala zetu ziwe na haja ya kupata magoli 3 kwa nunge kwani wale jamaa kule Senegali lazima watakataa kuadhibiwa idadi kubwa ya mabao lakini tunahitaji sala za maombezi kwa wote Rastafarian,wakristo,wabudda,waislamu n.l ili mradi tuwe na lengo moja tu la kushinda mchezo huo.

Tulia kwa dakika 5 tu omba kadiri uwezavyo angalau uwe na moyo wa huruma kwa vjana hawa wanaoteseka kwa kuweka rehani mioyo yao ili wapate ridhiki ya maisha.

Hapa nilipofika leo Mbinga kuna watu tokana na baridi+Taifa Stars=kihoro na homa matumbo zimejaa tele kumbe watu wanaugulia mechi hiyo,wanajiuliza itakuwaje yaani hata maofisini mambo ni hayo hayo.
uhuru daima

Tanzanite Inaitajirisha India!

Tanzanite inachimbwa Tanzania na inapatikana hapa pekee,lakini habari toka India zinaseama madini hayo yamewezesha ujenzi wa viwanda 15 nchini humo.Viwanda hivyo vinajihusisha na uchongaji,utengenezaji wa bidhaa zinazohusu madini pamoja na usambazaji dunia kote!!!!!

Kitabu cha orodha ya makampuni cha India kinaeleza kuwa makampuni hayo yapo katika miji ya Jaipur,Jimbo la Rajastham nchini humo.Majina ya makampuni hayo ni Gems,Pankas Gems,Sumati Gems,Daga Gems,Vidhan Gems na Ghoshi Export n.k yaani ayko mengi mno kifupi ni hayo.

Najua utashangaa nimepata wapi wakati hapa kwetu Nyasa habari tunategemea Redio za Malawi,Redio za Tanzania ambazo ni chache tu.Lakini habari hii nimeiona leo hapa Mbinga mjini bwana maana leo nilipania kuja mjini kujionea shughuli za walioelimika.Acha tuendelee kuvua samaki huku tukidumisha utamaduni wa nidhamu.Yaani nimestaajabu hata ikirejea nyumbani Yule mzee wangu(baba) mwenye hasira na kutowaendeleza wananchi sijui atasemaje.

Lakini hali hii si njema kwani hata Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki aliwahi kuwaambia wasomi wetu pale chuo kikuu Mlimani 'waone soni'kwani madini hayo yanainufaisha sana nchi yake.Hii niliambiwa na rafiki yangu wa palepale,hivyo usishangae kuwa kwangu kijijini LUNDU hapa nikashindwa kujua huko mjini mnafanya nini.
Jamani mimi napata mfumuko wa hewa(pulesha) maana hali hii si njema.
uhuru daima amka mwana wa Tanzania,wakati ni huu

September 03, 2007

Jumatatu hii ninaanza na hasira

Kuna jamaa wanapenda sana kuchezea muada wa watu.Lakini ukiwaambia kwa lugha ya kikoloni kwamba "Mastering;Time Management"wanadhani jamaa anajidai eti kasoma..sivyo ila ni lazima kuzingatia muda wako la sivyo utajikuta kila kitu harijojo.

Ndio maana mwanablogu freddy macha anasema kuna watu hawana nidhamu hususani sisi vijana.Yaaani hata salamu hakuna,ndio utamaduni wawapi huu,unatokea wapi huu eeeh.

Lakini siku ya leo nimeanza kwa kupotezewa muda na watu wasio kanuni maana wanaishi kama wapo hekaluni wakati hata huko hekaluni kuna kanuni sasa hivi jamaa linanipigia simu sijui nini wakati anajua wazi kuwa hapa kwa wanyasa ni mvumo waziwa tupu.Kama sauti kubwa basi ujue kuna ngoma mahala tena utasikia watu wanasema kuna kipaimara na ukatakumeni n.k
sijui kuishi bila kuwa kanuni na miiko inakuwaje hivi wenzangu mnasemaje hilo