September 23, 2007

Nyasa Na Mazingira Yake

Ukanda huu kama nilivyosema awali kwamba una mengi ya kujivuni licha ya ziwa hilo.
Eneo hilo lina shughuli nyingi tu ikiwemo kilimo,ufugaji,uvuvi ambao ndiyo nguzo.
Sasa ukanda huu una mambo ya kujivunia sana kwani hakuana matatizo ya njaa kwa wakazi wake hivyo ni maeneo yenye adhi nzuri na maandhari yenye kuvutia kwa wageni na wenyeji
pia bila kujali asili.Taratibu tuitaingia katika uchambuzi wa vijiji na miji midogo ya eneo hilo ambalo nisehemu kubwa inayounda jimbo la uchaguzi la Mbinga magharibi na wakazi wake ni wanyasa ambao mchanganyiko wake wengine ni kutoka Malawi au wenye asili ya huko lakini
raia wa Tanzania,kwani ukiuatilia asili yao wengi wanaishi nchini Malawi au kuna uhusiano
kati ya wanyasa wa Tanzania na wale wa Malawi licha ya ukaribu wao.

September 17, 2007

Kwa ufupi leo

Ni kwamba nipo katika chuo kikuu hapa mlimani katika tawi la chang'ombe,si unajua tena mambo ya kusaka elimu ya dunia hii.Basi ni kwamba kabla sijaandika kuhusu nyasa ngoja nidokoe japo kidogo.
Lero nipo hapa chuo kikuu nafashughulikia masuala yangu ya ya masomo si unajua dunia ya sas bila kusoma kazi bure tu ndugu yangu lakini kuisoma ni maarifa si vyeti.
Ndiyo nipo katika elimu juuuuu zaidi.Achana na hilo halihusu kabisa kuhusu nyasa bado nafanya upembuzi yakinifu kwa mahitaji ya wasomaji

Uzuri Wa Ukanda Wa Nyasa

Kwa kawaida ni ngumu kukubalina na hoja kwamba maeneo ya vijijini kuna uzuri wake licha kuwa na tabia za kijijini.kwanini nasema hivyo kwasababu mara nyingi wageni husasni wazungu wakija maeneo haya huvutiw na mandhari yake,si hao pekee kun a wenyeji huvutiwa zaidi ya kuona kila siku mana ni burudani tosha katika ulimwengu mzuri wa raha kama nyasa.Ni muda huohuo ninaoufanya kuifurahia hali ya hewa na uzuri wake.
Kweli maeneo haya yanapendeza sana licha ya kuwa na tabia za vijiji,ambavyo nchi yetu haifanyi juhudi za kuendeleza vijiji vyake.Kama nilivyosema awali kwamba ni wakti wa kuonyesha hali yake nzuri na furaha ya ukanda wa nyasa ulivyo maana ni burdani tosha katika maisha ya kila siku ya wanyasa ambao hujituma kwa kuafanya kazi za kuleta maendeleo yao.Tuatoana kila eneo la kijiji na shughuli zake za kila siku.