October 24, 2007
KWAMBE;nyasa,sifa na uzuri
Naam hiki ni kijiji kinachopakana na kijiji cha chiwanda.kwa asili kinashabihiana sana jirani yake huyo.Sifa kubwa ya kijiji hiki ni upepo mkali nyakati za kiangazi,upepo ambao huambatana na na kasi ya mimea kupukutisha majani yake.Ni kijiji ambacho sifa hiyo inakifanya kiwe tofauti na jirani zake kwani ingawa kipo katika ukanda mmoja kina tabia hiyo tofauti na vijiji vingine.Wakaazi wake wengi ni kama vijiji vingine kwani hutegemea sana uvuvi,kilimo,na ufugaji ambao kuna makundi makubwa ya ng'ombe na wanyama wengine.Pia kiji hiki kinategemea zao la Mpunga kama nguzo ya uchumi kwa kiasi fulani.Ardhi yake ni kama kilivyo kijiji cha chiwanda kwani ni ya mchanga na kuna mabonde makubwa ambayo hufanya watu kulima mpunga katika nyakati tofauti iwe masika au kilimo cha umwagiliaji.Umwagiliaji huu huwa katika mifereji iliyochimbwa katika mashamba hayo ili kupitisha maji kwa wingi kama zao lenyewe linavyotaka maji kwa wingi.Wakaazi hawa hupata maji safi na salama ya bomba yaliyopishwa hapo kwa miaka mingi hivyo kupunguza idadi ya magonjwa yanayoambatana na ukosefu wa maji salama.Ziwa nyasa limekuwa kama kiunganishi chao na wakaazi wa nchi jirani ya Malawi.Kuna mito ambayo husaidia wakaazi hawa kulima bustani nyingi kwani maji yanayotokea katika mito ni mengi sana hivyo hurahisisha kazi ya umwagiliaji wake.Naam kwa wakati huu kijiji hiki hulima kilimo cha mpunga kwa kumwagilia kwani hakitegemei masika pekee,hivyo huwa na vipindi viwili vya ulimaji wa zao hilo.Tukutane katika kijiji kingine nan kisha tutaenelea na masimulizi yenye ufasaha kwani tunawakaribisha sana kuogelea na kujiliwaza katika ukanda wa ziwa nyasa.
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
kwambe,
Nyasa
October 21, 2007
Nyasa,habari,mseto na karibu njema
Naam leo nizungumzie jambo lamseto tu au kama habaro fulani tu ili tuendele na mambo ya ukanda huu.Ni maeneo ya ajabu sana kwani kuna baadhio ya maeneo yana kumbukumbu za vita baina ya wanyasa,wamatengo dhidi ya wangoni wavamizi hawa waliotoka nchi za kusini mwa afrika.kuna mapango yenye kusimuliwa na wazee wetu namna vita hivyo ilivyokuwa huku wanyasa wakipoana tokana na uwezo wao wa kuogelea hivyo walipozidiwa walikimbilia ndani ya maji.Tukumbuke wakati huo sialaha kubwa ilikuwa mishale,majambia,mapanga n.k lakini maadui waliweza kuopeshwa na silaha hizo.Maeneo haya yana mambo ambayo wakati mwingine hayajionyeshi kwa uwazi bali mpaka unapofanya uchunguzi na kuwahoji waliokula chumvi nyingi ndipo unaweza kupata habari motomoto za nyasa.Mfanao wenye asili ya wanyasa ni kundi kubwa ambalo limesambaa Malawi kwa kiasi kikubwa na lugha zao hushabiahiana hata asili ya majina yao.Nilibahatika kukutana na "mkoloni" mmoja hivi{mzungu} yeye ameweka maisha yake katika mji wa Mbamba Bay ambao ni kama kitovu kikuu ca maeneo haya achilia mbali Liuli na Lituhi au Lundu.Yeye anauwezo wa kuongea kiswahili fasaha kuzidi mzaliwa wa nchi yetu.anavutiwa na historia inayofungamana ya wanyasa,wangoni,wamatengo na wenyeji wengi wa malawi.Nyasa ina mambo mengi ya kumbukumbu ya taifa ambayo hayaandikwa.Mfano uwepo wa kituo cha Jando na unyago katika kijiji cha KILOSA ambapo majengo au eneo lake limehifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo.Tutaendelea polepole na mengine mengi,huu ni mwanzo tu na mengi ya mkoa wa Ruvuma hususani wilaya ya Mbinga tutajadili na kuyaweka pazuri.KARIBUNI NYASA.
Madhumuni
dondoo,
habari,
kumbukumbu,
Nyasa
October 20, 2007
CHIWANDA;wanyasa na eneo lake
Hiki kijiji cenye sifa zinazokaribaiana na vijiji vingine,kinapaka na chimate kwa upande wa kusini.Nacho kipo mwambao huohuo wa nyasa na shughuli kubwa hapa ni kilimo,ufugaji,uvuvi, na biashara.Eneo kubwa la kijiji hiki ni tambarare sana hivyo hutofautiana na jirani zake wa chimate.ardhi yake ni ya udongo wa kichanga ambao upo katika maeneo mengi ta barabarani na pia kuna maeneo makubwa sana ya kilimo hususani katika maeneo yenye ardhi inayokubali kilimo cha mpunga.Maendeleo si makubwa kiasi cha kufananisha na miji ambaypo angalau ina miundo mbinu fulani lakini jitihada zipo kwani wananchi wake wamekuwa wakajituma katika shughuli za kujiletea maendeleo kuliko kusubiri serikali,Pia raia wake katika kijiji hiki wanasaka elimu kwani walikuwa katika muungano wa kata yao katika ujenzi wa shule ya sekondari iliyopo katika kijiji cha chimate.Kubwa zaidi hapa ndipo Meli zinazofanya usafiri katika ziwa nyasa upande wa Tanzania ziliweka kuwa kituo cha mwisho na kurejea tena Itungi,lakini tokana na asbabu mbalimbali ikiwemo kina cha maji kituo hicho kikaondolewa na kuwekwa mbamba bay.hata hivyo mabaki ya majengo yake yanatumika kama sehemu ya mafunzo ya uvuvi kwa wakaazi wa eneo hilo na kuwa makao makuu ya vijiji vingine kwa shughuli za ukaguzi wa zana imara za uvuvi ambazo hazihatarishi maisha yao.Naam tuonane katika kijiji kingine na habari zaidi za vijiji nilivyoandika tutarejea ili kuona mambo yaliyopo maeneo ya NYASA na WATU wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)