February 07, 2008
Wanyasa kwa Samaki huwatoi kabisa,.. Hata wakiwa Ughaibuni..
Nilijikuta najiuliza hivi hawa wanyasa bila samaki ingekuwaje?Basi ni hivi nimepata waraka kutoka Ughaibuni,yaani dadangu huyu huko Ughaibuni anakwambia anakumbuka Magege yakiwekwa chumvi na pilipili pembeni we acha kabisa..Lakini usishangae nimepataje hii habari kwani utajua kuwa nipo hapa nyasa.Jibu ni ndiyo lakini nimeibukia hapa Mbinga hapa kama kawaida kudandia maisha.Dada anakumbuka samaki wa ziwa nyasa yaani njozi zote mambo ya nyumbani.Wanyasa, hebu soma sehemu ya ujumbe huu "Nimevutiwa na Blogu yako,mimi mnyasa yaani nakumbuka nilipokuja mwaka jana mwezi novemba nilipewa magege na chumvi kisha na pilipili yaani acha nijichane we acha tu nyumbani bwana".Mtoto wa kinyasa utamjua tu si unaona alivyochambua aina ya samaki hao? yani anajua viungo vyake na bila shaka liapewa samaki wa kuchomwa.Ukitaka kujua yuko wapi hebu peruzu jiografia nchi ya Sweden ilipo ndipo utajua ninachokisema.Dada yupo ughaibuni lakini hajasahau nyumbani {Tanzania}anakuja kutembelea,Je wengine mpo?Lakini ndugu yangu Ndesanjo anatembelea sana Jeff na wenzake.Mwenzetu anakumbuka samaki lakini amesahau dagaa,kambale,ntaka,mandongo,mbasa,ngogo n.k ndiyo nyasa hiyo watu wanaselebuka kwa raha kama dada yetu anavyoselebuka toka ughaibuni na samaki wa nyasa. Wanyasa kwa samaki huwatoi kabisa....yaani mpaka ughaibuni?
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
lundo
February 06, 2008
Fumbo katika Maisha kutoka Nyasa...
Jua limekuwa likitoka na kutua kila siku ya wiki iliyokwisha na litafanya hivyo hivyo katika wiki inayofuata.Mambo yataendelea hivyo bila kujali jinsi ninavyofanya au hata jinsi ninavyokuwa,Muda unapita na sote tunaona,wavivu kwa wachapakazi,wasiojali kwa wenye nidhamu hali kadhalika.Tunasimama katika mwanzo wa wiki hii,muda ambapo wiki mbili zinapokutana zinaweza kuleta harufu ya uchungu kwa baadhi yetu.
Uchungu wa kumbukumbu ya kushindwa kwa nyakati zilizopita,lakini pia inakuja na alama ya furaha kwetu sote kwa vile ni muda wa tumaini jipya linalofungulia mlango wa mafanikio mapya...Huu ni muda wa mafaniko mapya.
HEBU SASA TAFAKARI....Wiki iliyopita imepita,Hivi ilikuwa na maana gani kwangu?Inapokuja ilinikutaje?Na sasa imeniachaje?Na hapa inaanza wiki mpya nyingine.Je italeta nini au itaniletea nini?Hivi nitajisikiaje kadiri saa zake zitakapokuwa zinapita siku?Hayo yote ni fumbo kwangu kwa sasa....Hivi kila siku itakuwa na rangi gani?Na itaweka sura gani mbele yangu,kadiri nikitazama mshale wa saa ukisonga,hilo ni fumbo kwangu.

amani na upendo,
falsafa,
Nyasa
February 05, 2008
JANETI katua Nyasa na salamu yake "inyahi"....
Moja ya chanagamoto zinazowakabili ndugu zangu Wanyasa waliopo mijini na ughaibuni ni kuwaelimsha watoto wao mahali walipozaliwa wazazi.Chanagamoto hii ni kwamba wazazi wasije wakadhani kuishi mjini pekee ndiyo kunamfanya mtoto kujisikia vizuri zaidi ama kuwa na maarifa zaidi.Lakini mahala panapoitwa mjini ni mkusanyiko wa tamaduni mbalimbali ambazo Mwanafalsafa Karl Marx aliziita "Union Tribe" yaani muungano wa makabila kama ilivyokuwa huko Roma.Wazazi wetu hawa wanapaswa kuwaeleza watoto wao kwamba ni mahala gani walipozaliwa ili nao waweze kujionea asili ya wazazi wao ukizingatia hatari ya historia kupotea juu ya mambo kadhaa yatuhusuyo.Naam basi kama unavyojua wazazi wengine walivyo makini kuwafundisha watoto wao asili zao na utamaduni wake mfano angalia wachezaji kadhaa wa dunia hii waliozaliwa ughaibuni wanavyogeuka na kutafuta asili zao mfano Mwanasoka mahiri Frederic Kanoute wa Mali licha kuchezea timu ya Taifa ya Ufaransa aliamua kurejea asili yake.Hivyo kama kawaida Wanyasa kujivunia unyasa wao,mwezi januari katua dada JANETI hapa nyasa kwetu ikawa balaa yaani vumbi tupu,binti kachangamka licha ya kuona sisi Wanyasa kama 'katuni'{natania tu},jambo lake la kwanza ni kujifunza kusalimia kwa lugha ya Nyasa ukizingatia eneo alilokuwepo la MBAHA ni Wampoto kama ilivyo kwa LUNDU na maeneo ya karibu.
Wacha kabisa ndugu yangu huyu kaanza kuongea maneno kadhaa ya lugha ya hapa kasheshe tupu.Bahati mbaya neno lake lilikuwa moja tu "INYAHI",ingawa neno hili linamaanisha "nzuri" katika salamu ya neno "MONILE" lakini haliwezi kukaa katika kiitikio cha kila salamu,......acha kabisa dada katua kwa wanyasa yeye ni "INYAHI" tu wala haoni noma ndiyo kujifunza asili ya mzazi wake huko ni fahari sana katika afrika yetu.Kila salamu yeye ni "INYAHI" tu hakuna kikwazo yaani saaafi sana...Nyasa jamani yaani furaha sana najua akisoma hapa atanisaka tena hadi huku nyasa tunakovua samaki na kuzitafuna kiasili.....lakini nakupenda dadangu wala sikudhihaki ni kujielimisha huko.....natumaini atajifunza neno lingine mie sijui...acha ningoje nistabiri..

Nyasa,
soga
Subscribe to:
Posts (Atom)