February 24, 2008

SIMAMISHA.KILA KITU SOMA FALSAFA HII

"Elimu siyo shahada wala cheti,ni uwezo wa kuchambua,kufikiri kwa njia pana,kuwa mbunifu,kuuliza maswali,kuwa jasiri,kujiamini,kujua jinsi ya kujifunza zaidi,kupanga mambo vizuri,kupima,kuhoji,kuweza,kutatua matatizo ambayo hujawahi kukabiliana nayo".Vipi ndugu yangu Dada JANETI unaonaje hayo na ndugu yangu Dada SUZI pale chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere unaonaje hii.Simamisha kila kitu kwani usiposoma basi unafukuzwa katika ulimwengu huu au kusoma blogu hii{natania}.kazi kwenu wanazuoni hasa Ndesanjo

February 23, 2008

Haa!!Kumbe Watawala wetu "VAYIVA?"

Jamani tusishangaane hapa,mbona hii hatari kwa wanyasa sisi?Yaani hawa viuongozi wetu "VAYIVA"? haya maajabu wala hawaoni noma!.Neno "VAYIVA" lina maana "WANAIBA",nimelitumia hili kustaajabishwa na hali ya majambazi wa wa nchi yetu ambao tumewapa mamlaka ya kutuongoza.Wezi wakubwa hawa na kikundi chao na wizi yaani "VAYIVA" hawana hata aibu halafu wanalilia kusikilizwa mbona makubwa.Huku nyasa wala hatuna habari lakini eti nimefika hapa Mbinga ndiyo napewa kale haotuba ka mnyakyusa aliyesoma kale karipoti kanakowataja wale wezi wetu.Yaani "VAYIVA"?..