April 06, 2008

LINDA Yuko Hoi ,Ligambusa Limemchosha

Ama kweli huu ni urithi kwa Wanyasa.Hivi unakumbuka kisa cha JANETI kutua nyasa na salamu yake "inyahi"?,umesoma au hujasoma?{kitafute humu}.Basi Janeti ana nduguye huyu dada LINDA yaani watoto wa kinyasa hawapotei.Ikawa harusi Jumamosi hii,ngoma za wanaysa zikaporomoshwa hapo,madogoli yakakolea nyuzi bin nyuzi,watu wanakatika viuno kwa maraha ya harusi.Lakini LINDA mtoto wa wanyasa anaishi mjini kakumbana na ngoma za wanyasa "Ligambusa" kaanza kubinua viuno,kafunga kanga kiunoni,viatu kaweka kando,kacheza sambamba na wanyasa,kadhihirisha unyasa licha kuwapo mjini yaani ilikuwa burudani, acha nicheke niringe nina mwanya?.Basi dada kaona ngoja acheze kwa bidii huku mpigaji akivuta nyuzi bin nyuzi Ligambusa linakubali bila ubishi watu wanaselebuka,dada huyu naye kaanza kuonyesha madoido yake ya hapa na pale akamudu kwenda sambamba na watoto wa kinyasa.Kwa hakika ngoma ya Ligambusa kwa wanyasa linachezwa zaidi na vijana kuliko watu wazima kwani inahitaji ukakamavu,mitindo yake ya kasi,inahitaji pumzi.Sasa nashuhudia harusi ya kinyasa hapa nilipo na wanyasa wanasuuza nyoyo za wasio wanyasa, wanaduwaa.Mwishowe ananijia na kuniambia "unalijua Ligambusa mtoto wa nyasa wewe?".kuona hivyo nikamwambia subiri uchovu baada ya kucheza.Mmmh leo jumapili kaamka analamika "Nipo hoi,nguvu sina, mwili umechoka",nikamkumbusha nilivyosema,akabaki kucheka akidai wanyasa ni watu safi sana,yaani licha ya uchovu lakini Ligambusa limenikuna sana natamani kucheza kila siku nyuzi bin nyuzi,kasahau uchovu.Heeeh sijui nimejieleza vizuri kuhusu Linda,hivi inaeleweka?.karibuni nyasa jamani utamu wa Ligambusa mwaujuaaa??

April 05, 2008

Wanyasa+Mapenzi+Upendo n.k

Kuna jambo linanikumbusha kitu muhimu sana katika nyanja za uelimishaji kwa wengine.Jambo hili nililitafakari sana katika ulimwengu huu kwani kila siku yanatokea.Mara nyingi nawapenda sana wanyasa wangu kama mfano wa mambo ya hapa na pale.Basi tukio lenyewe lilikuwa nyakati Maalumu zile za wanyasa/Pasaka.Kuna siku tukiwa tunatazama mpira {siyo kwenye Tv}nilipata falsafa ambayo lazima leo niiseme hapa.Ilikuwa hivi; 'Hivi jamani oneni wanaume wanavyopenda mpira wa miguu/soka yaani haielezeki,ndiyo kusema wanapenda mpira kushinda sisi wake zao?Mmh,acheni niseme jamani kama wanaume wote duniani wangewapenda wake zao au kuonyesha mapenzi kwa wake zao kama wanavyoupenda mpira hakika ndoa zingedumu daima.eti nani anabisha hapa?.Oneni wenyewe wanavyokumbatiana kwa upendo wewe unadhani ingelikuwa hivyo kwa wake zao mbona ndoa zingekuwa ni zaidi ya upendo huo?Lakini wao wanakumbatiana sasa wakirudi kwa wake zao wakali,wamefura,wamekunja ndita kwa ghadhabu wala hawawakumbatii,hujifanya hawatuoni vile mmh".
Siyo siri nilijikuta nikiwa na maswali mengi,nikakosa jibu.Kifupi hii ni kauli ya dada mmoja hivi wakati wa kutazama mpira hapa nyasa si unajua siku muhimu kama ile lazima kuwe na burudani kwa wasiokunywa Myakaya,komoni n.k Sasa sijui wenzangu mnasemaje kwani haya ni mawazo ya dada wa kinyasa,analilia upendo wa waume zao mmh sijui wamepeleka wapi,tuusake sasa!

April 02, 2008

Hebu Msome Mnyasa huyu jifunze maisha

Malezi ya familia ni magumu pale unapokutanisha tamaduni mbili tofauti.Hili anatuelimisha dada yetu huyu yale anayoyaona huko ughaibuni na kwetu afrika hususani kwa wanyasa.Lakini ni habari njema kwani kila siku watu wanahitaji kujifunza mapya na kama alivyopata kusema Mwanafalsafa Galileo kwamba huwezi kumfundisha mtu kitu kama hajachukua hatua za kujifunza,sasa tuchukue jukumu tujifunze muda ndiyo huu.Hebu soma habari nzima jionee mwenyewe mambo hayo,wanyasa mpoooo!!!!

www.ruhuwiko.blogspot.com