April 14, 2008
Mitandao Imetekwa Nyara,Kaa Chonjo!!
Nimejikuta nikishindwa kuangua kicheko,yaani nimecheka mpaka jamaa hapa pembeni ninavyoandika akajiuliza hili jamaa vipi?Unajua kwanini?Kipindi hiki hapa nyasa kuna dhoruba kaqli mawimbi yanapiga toka upande wa kaskazini kwenda kusini,basi wanyasa wanaona hii kero,lakini hawajaacha kuvua samaki shauri ni kitoweo chao.Basi jamaa kanishtua hapa nyasa anahisi harufu ya kutekwa nyara mitandao ulimwenguni kwahiyo wanaoblogu na wenye tovuti wawe makini.Nikabisha sikubali bila kuona,lakini nikakumbuka kublogu mpaka niingie mjini Mbinga,Looh! nikakumbuka jambo nililosoma kwa Mwalimu wangu Ndesanjo Macha pale jikomboe.Kumbe jamaa ananishtua hilo wakati nilikuwa nalo kichwani kitambo.Ni Hivi hakika mitandao imetekwa nyara kila anayeblogu akae chonjo saa ya hatari lakini kwa wanyasa tunaweza kujificha ndani ya maji lakini usiulize tutapaje pumzi...sawa..?.Mmmh!!utajuaje kama natania?Jamani mnamkumbuka yule mwizi wa kura za haki kule Kenya?Juzi hapa kateua mawaziri 44 nadhani hii sherehe ya kutafuna mali,basi kateka nyara mtandao; bonyeza hapa http//www.twitter.com/MwaiKibaki,ngoja nisubiri majibu yako..
April 12, 2008
TANGAZO;Nina kila kitu mbona sina Mpenzi?.
Nimekumbuka kisa cha rafiki yangu asimini usiamnini.Yaani leo tangu nimeamka najiuliza hivi kisa hiki hakifai kuwepo hapa?Nikajiuliza vipi kisa hiki watu wakisoma?Lakini nikaona nitakuwa mtu wa visa na vituko lakini sitaacha!...Ni hivi kuna rafiki yangu mmoja hivi anasema anacho kila kitu ambacho mwanamke anaweza kuvutiwa.Ana sura nzuri,ametulia,anajua kupenda,anatabasamu ,mzungumzaji mzuri,anahitaji kupendwa n.k lakini anaseama yeye hajaona mwanamke anayempenda na hajui kwanini.Huyu amekuwa wakati mwingine hana muda wa kukaa na wanawake/wasichana hao anashughulika na kazi zake za hapa na pale.Anashindwa hata kuanzisha mazungumzo na wanawake/wasichana kwani anaona aibu kufanya hivyo na wakati mwingine anaogopa kuwahitaji wanawake/wasichana akidhani watamwona 'mwingi wa habari'.Lakini huyu anamasharti ambayo labda anadhani yanamkosesha wanawake/wasichana.Tatizo lake akianza kuchambua kasoro za wanawake/wasichana anaodhani anawahitaji basi huishia kusema 'mbona huyu anakasoro hii na ile au jambo hili na lile.Yaani yeye kwake kila mwanamke/msichana fulani 'mbona anakasoro hii au ile'.Mpaka naandika nimeshindwa kushauri kwani naona jambo hili lipo mikononi mwake.Je unamtaka na unadhani unaweza kumfariji rafiki yangu huyu?anaumia sana,hajui kwanini hana mpenzi/rafiki wa kike.Mimi sijui cha kumsaidia,karibuni ndani.Yaani yeye kila siku ananimbia "rafiki nina kila kitu mbona sina mpezi?" jamani nifanyeje nashindwa kumsaidia jambo hili.Tangazo
Madhumuni
Hisia za moyo,
kwambe,
mapenzi,
Nyasa,
soga
Subscribe to:
Posts (Atom)