April 20, 2008

Ziwa Limechafuka,Wanyasa na Ngalawa Tu

Nilikaa juu ya jiwe nikiangaza huku na huko kuwatazama wanyasa wanavyohaha katika shughuli zao za maisha ya hapa na pale.Nikaona ngalawa zinaumiza vifua vya wanyasa kwani hali siyo nzuri katika ziwa kwa sasa.Hakika ziwa nyasa limechafuka namaanisha dhoruba kali sana wiki hili,kila myasa/mvuvi unayemuona kanuna,kafura kama chatu ghadhabu imejaza vibaba wala haimithiriki zaidi ya hapo,hawacheki.Ziwa linanguruma mawimbi makali makali,nyavu zinapotea nyakati hizi shauri maboya yanazama kwa kushindwa kuhimili nguvu ya mawimbi.Lakini pamoja na kuchafuka kwa ziwa hilo hakuna hata mvuvi anayethubutu kusema atabaki nyumbani kujipumzisha au kurejesha zana za uvuvi nyumbani ili kupisha dhoruba hiyo,wapi bwana sahau kabisa habari ya wanyasa kuogopa dhoruba nyakati hizi au kuacha ngalawa ili kukosa kitoweo,hakuna mnyasa anayefikiri kula nyama za kuku wasiokomaa,wanaotafunika hata mifupi,wanaokuzwa kwa kudungwa sindano,wanatia kinyaa kuwala,au chipsi za huko mijini.Wanyasa wanaelewa uzuri wa kuwa wajuzi wa ziwa hili ambalo wenyewe wanasadiki kuwa hakuna ziwa lenye dhoruba kali ulimwenguni zaidi ya hili.Hakuna aliyeka chini kuacha ngalawa au kuacha kupanda mitumbwi.Yaani uvuvi unaendelea kana kwamba ziwa lipo shwari wakati "limekasirika" utafikiri limedungwa sindano ya kukasirika.Yote hao ni kitoweo cha asili hiki utamu adimu huu.

April 19, 2008

Nyasa,Mila,Desturi+Miaka 14 Ughaibuni

Kuna habari moja imenifurahisha sana. nimjikuta nikiwa katika tafakari kuhusu habari yenyewe. lakini ni jambo muhimu kukumbuka mambo ya nyumbani nyasa kwa wale mliopo ughaibuni.Hii habari lazima tuitafakari sisi wanyasa ambao tumeishi sana na wamisionari hivyo twayajua mengi.Soma habari nzima ,bonyeza hapa www.ruhuwiko.blogspot.com inahusu namna maisha ya wazungu yanatawaliwa na ubinafsi na kujitegemea mwenyewe kinyume na wanyasa tuombao chumvi kwa majirani zetu.ughaibuni haipo hiyo....utaomba kwa nani

April 14, 2008

Mitandao Imetekwa Nyara,Kaa Chonjo!!

Nimejikuta nikishindwa kuangua kicheko,yaani nimecheka mpaka jamaa hapa pembeni ninavyoandika akajiuliza hili jamaa vipi?Unajua kwanini?Kipindi hiki hapa nyasa kuna dhoruba kaqli mawimbi yanapiga toka upande wa kaskazini kwenda kusini,basi wanyasa wanaona hii kero,lakini hawajaacha kuvua samaki shauri ni kitoweo chao.Basi jamaa kanishtua hapa nyasa anahisi harufu ya kutekwa nyara mitandao ulimwenguni kwahiyo wanaoblogu na wenye tovuti wawe makini.Nikabisha sikubali bila kuona,lakini nikakumbuka kublogu mpaka niingie mjini Mbinga,Looh! nikakumbuka jambo nililosoma kwa Mwalimu wangu Ndesanjo Macha pale jikomboe.Kumbe jamaa ananishtua hilo wakati nilikuwa nalo kichwani kitambo.Ni Hivi hakika mitandao imetekwa nyara kila anayeblogu akae chonjo saa ya hatari lakini kwa wanyasa tunaweza kujificha ndani ya maji lakini usiulize tutapaje pumzi...sawa..?.Mmmh!!utajuaje kama natania?Jamani mnamkumbuka yule mwizi wa kura za haki kule Kenya?Juzi hapa kateua mawaziri 44 nadhani hii sherehe ya kutafuna mali,basi kateka nyara mtandao; bonyeza hapa http//www.twitter.com/MwaiKibaki,ngoja nisubiri majibu yako..