June 02, 2008

Uoto wa Asili Nyasa Yetu...Karibu jionee

Angalia kunavyopendeza,angalia uoto wa asili,majengo ya asili.Lakini hapo ni makazi ya muda mfupi, unajua wanyasa huwa wanakwenda kuvua samaki mahli ambako hakujavulia siku nyingi?Basi wakifika huko hujenga nyumba kama hizo.Karibuni nyasa jamani yaani hapo tu sijawawekea wale wamisionari walioishi huku enzei zile za wale wahuni kutoka ulaya na wizi wao.Lakini kwetu walikuwa mapadre na mabruda.Mmh inanikumbusha nikiwa na ndoto ya kuwa Padre au bruda lakini samaki walinizidi kete wakanipa hamu ya kuvua.Muulize dada pale ruhuwiko{tafuta kwenye ukurasa wa Tovuti/blogu}bloguni akupe hamu ya wanyasa kuingi katika Monesteri za kijerumani..Mhh ngoja nikumegee msomaji unajua dadangu huyu alitaka kuwa nani?Utajiju nenda kaone pale Chipole misheni halafu utaniambia lakini usije ukanisingizia nimekwambia mimi..wala tena najificha uvunguni mwa kitanda...aaaah nimekumbuka kitu najua utasema mbona leo nina usongo wa kublogu...jibu sijaandika siku nyingi nimekuja na ari ya zamani,nguvu za zamani na kasi ya zamani.Naenda kula ugali na dagaa leo,tena jana jumapili nimekula

Nyasa .....Hiyo usiulize Maswali picha itakasirika ..

Usiul;ize mnyasa vipi mbona kuna mtu hapo humtaji au hao huwataji?Mimi nakupa madoido ya Nyasa wala sitaki kelele.Mimi mtoto wa kinyasa utanimbia nini wakati najua utamu wa kuishi nyasa.Ngoja kwanza...jana kulikuwa na kichekesho eti jamaa alitaka kunitwanga ngumi wakati naadaa hizi picha,kisa eti wanyasa wanajiona matawi ya juu wakati hawana lolote.Mimi nikamwambia ingelikuwa hawana lolote basi wangelikuwa vichaa kwani mungu katuwekea kitu na tunacho nacho ni ubongo hivyo huwezi kumwambia mtu hana lolote kimaisha.Labda akifanya ujinga au kuleta ujivuni wakati hana ujuzi wa kile anachokisema au kukifanya.Yaani wapo watu ambao hawapendi kuheshimu wanachofanya wenzao hata kama ni jambo dogo....Nakwambia nilikasirika nikapiga ngumi kali ukutani lakini niliumia mpaka sasa nimefungwa bandeji nauugulia sana kisa kutetea wanyasa...njooni mnipe pole hata kuandika hapa natumia mkono mmoja tu wa kushoto......mbona hamnipi pole nanyi mna kisirani na wanyasa.....nitalianzisha varangati....ooooo ngoja nipone kwanza.

Funzo La Mnyasa Hata Kama Humpendi

Wanyasa ni watu ninao waheshimu daima kwani wana msimamo juu ya maisha yao.Unaweza kumwona mnyasa akiwa kazini kama hivi ukadhani mshamba au mtu asiye na staha kabisa.Basi unajidanganya yaani utakuwa unacheka huku unalia wala usidhani kama natania.Hawa ni watu wanaopenda kufanya yale wanayoamini yanamanufaa kwa maisha yao,hawana haja ya kuharakisha maisha kwani wanajua kila kitu hupangwa na mungu huku ukiwa na uthabiti wa mipango hiyo.Sasa hebu angalia mwenyewe hapo nyavu ndiyo hiyo,matarajio ni kukomba mchuzi wa samaki wa aina yeyote.Kwanza wanaheshimu kazi yao kwa kufanya kwa utulivu.Yaani myansa hata kama humpendi kuna mafunzo utapata au muulize yule rafiki yangu kule Landani alipofika akaduwaa kwa nyodo,lakini akaona kuna jipya kwa wanyasa,mwishowe akatoa heshima zote kama askari jeshini,upo?tazama kwa hamu samaki haji bure huko mjini kwenu wavivu wakubwa .....aaaah samahani natania....unanichukia mimi myn asa?aah!lakini ...ebuu ngoja kwanza.Sawa...ngoja nikomee hapa.

Mnyasa Kazini utamwambia Nini........Hapo vipi?

Mwangalie mwanaume wa shoka akiwa amekaza msuli kwa kupata kitoweo.Huyu ndiye mnyasa yaani hapa huwezi kumwambia aache ili akaishi maisha ya mjini ya kuuza machungwa eti umachinga..acheni hizo.Mh msije mkasema nadhihaki lakini ndiyo ukweli hamuuzi maji machafu na kuadi ni maji safu ta kunywa?eeeh bvasi jamani.Ngoja kwanza kuna wakati huwa naamini kuwa maisha ya wanyasa yanalindwa sana na mola wetu.Watu wanaweza kuishi katika hali ngumu lakini wale husikii magonjwa ama milipuko ya magonjwa kama maeneo ya mijini...kazi kwetu

June 01, 2008

Watunza Afya Zetu Hao,Wapeni Malipo Mazuri

Wauguzi ni watu muhimu sana katika ulinzi wa afya za wananchi katika taifa lolote.Hebu waone hapo walijipumzisha wakisiliza mawaidha ya kuboreshwa kwa malipo na kuiomba serikali iwasomeshe kwa kiwango kikubwa au mnasemaje?Najua wanafunzi wa vyuo vikuu watasema wanataka kuwabania "mshahara wao" wanaolipwa na ile bodi,au watasema ufisadi!hapana hawa ni watu muhimu sana hao.

Hawa Ndiyo Watunza Afya zenu Jamani...

Hawa ni wauguzi ambao wanahitaji sana mafao bora,alakini usiniulize nimewatoa wapi,lakini tunaamini afya zenu zinalindwa sana na hawa

May 27, 2008

Kumbukumbu,Kutoweka Kwa Rafiki Ya Baba Yangu

Jamani kama kuna kitu watu wanashindwa kukinunua hadi sasa.Unajua ni nini?Jibu furaha na huzuni.Hivi ni vitu ambavyo huwezi kununua popote na kama kuna mtu anauza hilo niambieni hakika nitajiua tena kujinyonga kwa utandu wa buibui wala usicheke.Nionyeshe nani anauza furaha na huzuni nimtunuku kifo changu hata kama ni mbele ya haki.OOH samahani sijaomba radhi kwanini nilitoweka hapa bloguni.Unajua majukumu mengine yalinibana yakanifanya nishindwe kuandika kuhusu wanyasa si unajua uvuvi samaki kunoga sana.Basi nilikuwa makini na usimamizi wa kumulika dagaa kitambo na ingawa tunasumbuana na mbalamwezi kwani dagaa tunawanasa kwa kutumia mwanga karabai na kutega nyavu na kuwavua hivyo mbalamwezi ukiwepo unaharibu mipango mutua ya kitoweo,mmenisamehe?aah sitorudia kosa nitatoa taarifa.Basi bwana furaha na huzuni ni hivi nimeuliza maduka yote hapa nyasa hayana, labda huko mjini mtanisaidia.Ni hivi leo nimewasiliana na dada yangu ambaye yupo makini sana na kazi zake yupo huko jijini Mbeya kwa Wanyakyusa.Huyu hana muda wa kupoteza mtoto wa nyasa,lakini usiniulize anafanya nini badala ya kuja kuchemsha dagaa,huo ni utaratibu tu.Mwisho ni huzuni,unaona sasa, pamoja na mikogo ya hapa na pale nina masikitiko/huzuni sana Rafiki ya Baba yangu amefariki.Ni habati ambayo nimeipata siku kama tano zilizopita.Nimeamua kumuenzi kwa kuandikia wanyasa wote kwamba Mzee Nchimbi Rafiki ya Baba yangu hatunaye.Mungu alitoa na mungu ametwaa,AMINA.kumbukumbu