June 06, 2008

Wanyasa Tumuombe mungu Tushinde

Huyu ndiye Mrisho Ngasa (mwenye jezi ya bluu)ambaye tutamkosa katika mechi ya Jumamosi hii tarehe7/6/2008 nchini Cape Verde katika mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia.Tutamkosa sana kwani mechi iliyopita hakuacheza baadaya kuumia nyonga mazoezini.ni mchezaji mahiri na mwenye msaada mkubwa kwa timu licha ya umri mdogo alionao.Tuloge na kuwanga kichawi kinyasanyasa

Timu Ya Taifa Imeondoka Leo

Timu ya taifa imeondoka leo kwenda nchini Cape Verde kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia.Hapa ni sehemu ya mashabiki wakishangilia timu ya taifa katika mechi dhidi ya Malawi iliyofanika hivi karibuni

June 05, 2008

Lizombe Limeumana hapa utasema nini

Usistaajabu kwani nimeondoka kidogo nyasa na kuingia mjini hapa na kukutana na picha hii muhimu sana kwa watu wa Ruvuma na wanyasa wote.Sina mengi ila tumshukuru kaka Richard Mwakienda kwa picha hii

June 04, 2008

Mwenye Mwanya aje,Washashi wanamtaka

kama una mwanya njoo nyasa utakutana na washashi pale Matema Beach nje kidogo ya bandari ya Itungi.N wengine ninawajua...unataka nikutajie?Sitaji mapaka unipe kwanza rushwa si unajua siku hizi rushwa ni kama kulamba asali,utamu ukizidi sana....natania bwana washashi wapo kibwena

Wanacheza,wanaselebuka na kuvinjari

sina maneno hapo,umenuna?kazi kwako ukiwa unakasirika mara nyingi utazeeka lakini ukicheka sana picha itapotea...polepole basi karibu nyasa hata kimyakimya

Mshashi Anavinjari Nyasa

Inaelekea huamini kama nyasa Washashi wanakuja kuselebuka..Bisha na hii.Halafu kuna jamaa anapenda sana kupingapinga mambo sasa nampa ngumi ya tumbo,sikio na mbavuni aaah samahani nilisahau bado sijapona ile ngumi ya ukutani ya yule jamaa.Hebu mwangalie Bibie huyo,anakukuna sana?eeeeh usije ukatangaza ndoa..wala sihusiki,lakini ananiambia anataka mvulana mwenye mwanya,je unao?

Ghorofa hilo! Wivu wa nini,Unacheka una Mwanya?

hapo sina hata maelezo ila wanyasa wanajua umuhimu wa kupumzika ndiyo maana wakajenga ghorofa hilo limegharimu hela nyingi sanajumlisha na za wale wezi wa wa benki kuu na yule Rais mwizi aliyemaliza muda wake mwaka 2005!unamjua?aakaa mie simjui nasikia alikuwa kibaka sana.unacheka,unaringa una mwanya....???

Unaonaje hapo?

Boti siyo mpaka uende ughaibuni,hata kwetu zipo waulize Litumbandyosi watakwambia,alikini usiniulize mimi mji huu uko wapi.Hebu tazama paleeeeeeee kuna dada mmoja hivi anapajua yule pale mtaa wa ruhuwiko bloguni bonyeza atakujibu

Wamo,Siyo Samaki pekee

kama unafikiri wanyasa wanachokiweza ni kuvua samaki na kujua majiraya kutega nyavy zao basi hujakosea ila hujui nini kinachoendelea hapo.Tazama wanaume wakiwa mzigoni wamekaza viuno,meno,miguu mpaka ngozi hakuna masihara hapo utaumia.kwanza inabidi uwe umeshiba sahani kama tano za ugali wa muhogo ikiwa wewe ni mgeni,lakini wenyewe ni nguvu za asili wale hawajui kwendaklabu za mazoezi kama huko mijini kwenu wanaogopa kansa shauri ya kutu za vyuma.

MV Songea inaingia Moja ya Vituo vyake Nyasa

Huna haja ya kuhofu,utamu wa nyasa ndiyo huuuuuuu.Ona watu wanangojea usafiri wao waupendao.

Tazama Uzuri wa Nyasa Yetu, Mazingira yetu

Nilipoandika kwamba mazingira safi,kama mlidhani nacheza basi mmenoa.Nyasa ndiyo jioni hapo uzuri unajionyesha wenyewe.Kwa mara ya kwanza nilipoitazama picha hii nikajiuliza swali moja.Kwanini yule rafiki yangu Christine wa Bavaria alilia na kugomea kuondoka Lundu pale ufukweni?Lakini nilipata swali la pili,kwanini wazazi wake waliamua kuwapo pale kwa masaa matano?,Sasa majibu nayapata kwamba ile kauli ya rafiki yangu yule kwamba "hapa naona nimependa upendo wangu wote,natamani ningelikuwapo kila siku,hakuna baridi kama kwetu,joto siyo kali ni la wastani haliumizi.Mbona hamchangamkii hii hali?lakini kifupi ni eneo zuri,nakuahidi Markus nitafika peke yangu mara nyingine bila hawa wazazi ambao wananilinda kama mtuhumiwa".Sikuwa na majibu ya haraka,na ingawa hajafika tangu mwaka 2003 lakini nimeamua kweka mtandaoni utamu wa nyasa kama huu,kwa yeyote ahayehusika karibuni nyasa

June 03, 2008

Washashi Nao Wamegota Nyasa

Naona nisiandike mengi,kwani nianchofanya ni kutoa ushuhuda wa "Karibuni Nyasa' ona Washashi nao wamegota.Washashi ni wazungu si unajua lugha za maeneo ya kizungu kwa vijana.Hatushangai tunajiunga nao tu...

Hawa Nao Wamo ......karibuni Nyasa

hapa ni Matema beach pembeni ya mji wa Kyela.Kuna ufukwe mzuri sana yaani ukanda wa ziwa hili ni utamu sana,Huyu Mshashi naye yumo katika kujiburudisha.Kairibuni nyasaaaaaa

Kitoweo.....Habari ndiyo hiyoooooooooo

Nashindwa hata kuongeza maneno mengi,jamani nyasa ni zaidi ya mnavyofikiri,Hivi niseme nini ili watu wapete kunielewa na nifanye nini ili niweze kuinua maisha ya nyasa...njoooooni muone....huyu samaki maarufu kwa jina Lingova ila wakiwa mengi tunasema Mangova.Aina ya Samaki hawa hupatikana zaidi nyakati za masika kwani ndiyo uzao wao hushamiri na kuenea zaidi.Picha hii kwa hisani ya rafiki zangu wapo pale Monkey Bay Malawi walinikuna sana waliponitumia nami naiweka hapa

Yule Mapunda Mpishi wa Kwenye Meli

Huyu ni mpishi wa shibe zetu ndani ya Mv Songea analonga na Mshashi.Yaani Mshashi hapo kagota hana mikogo shauri mambo ya nyasa siyo mchezo,Hebu waone wanavyoringa ndani ya Mv Songea hawana hata hofu juu ya Meli.Ziwa nyasa usafiri wa kutosha kama huu watu wa aina mbalimbali toka ughaibuni wanafurahia nyasa kazi kwako...mmmh usije najisifia kwa Washashi yaani wanyasa tuna ukarimu na msimamo hapo mshashi lazima adumishe nidhamu hakuna kuleta zake maana wanyasa kwa ngumi huwatoi si unajua kazi zao za uvuvi na kina dada mahiri na wakakamavu

Niambie Mnyasa Mwenzangu Maana Hawaamini

Tazama kwa umakini halafu jiulize wapi hapo....jibu ni Nyasa yetu ndugu

HataUsiku Kwa Mnyasa ni Uvuvi Tu

Watu hawachoki,samaki ni watamu hakika jionee mwenyewe wanaume wa kinyasa kazini.

Na Usafiri ndiyo Huo........ karibuni Nyasa

Hii ni Mv Songea ni meli ya kuaminika sana wala usihofu kama hayo magaro yenu ambayo ajali ni kama amri za usafiri wenyewe.Hii ni meli kubwa katika ziwa nyasa upande wa Tanzania.Na ile ndogo inaitwa Mv Iringa.Hapo ipo kazini na bila shaka kina Mzee Bukuru wapo ndani.Imenikuana sana Nyasa,yaani hii ni ari ya zamani,kasi ya zamani na nguvu za zamani...au unasemaje dadangu hapo ruhuwiko ya ughaibuni

Mnyasa Nimetua Chinula Wageni Mnasemaje hapo

Naam ndiyo nyasa yetu hiyo.Hapa ni barabara ambayo inakwenda moja kwa moja mpaka mji wa Mbamba Bay ambao ni mji mashuhuri sana katika ukanda wa nyasa una bandari nzuri sana,ingawaje sijaandika kuhusu sifa zake lakini polepole tutafika tu.Hapa ni maeneo ya kijiji cha Chinula pembeni ya mji wa Mbamba Bay.Angali nyumba zetu wala sina hamu na maisha yenu huko mijini.Usicheke basi kwani hatuna uhai?

June 02, 2008

Uoto wa Asili Nyasa Yetu...Karibu jionee

Angalia kunavyopendeza,angalia uoto wa asili,majengo ya asili.Lakini hapo ni makazi ya muda mfupi, unajua wanyasa huwa wanakwenda kuvua samaki mahli ambako hakujavulia siku nyingi?Basi wakifika huko hujenga nyumba kama hizo.Karibuni nyasa jamani yaani hapo tu sijawawekea wale wamisionari walioishi huku enzei zile za wale wahuni kutoka ulaya na wizi wao.Lakini kwetu walikuwa mapadre na mabruda.Mmh inanikumbusha nikiwa na ndoto ya kuwa Padre au bruda lakini samaki walinizidi kete wakanipa hamu ya kuvua.Muulize dada pale ruhuwiko{tafuta kwenye ukurasa wa Tovuti/blogu}bloguni akupe hamu ya wanyasa kuingi katika Monesteri za kijerumani..Mhh ngoja nikumegee msomaji unajua dadangu huyu alitaka kuwa nani?Utajiju nenda kaone pale Chipole misheni halafu utaniambia lakini usije ukanisingizia nimekwambia mimi..wala tena najificha uvunguni mwa kitanda...aaaah nimekumbuka kitu najua utasema mbona leo nina usongo wa kublogu...jibu sijaandika siku nyingi nimekuja na ari ya zamani,nguvu za zamani na kasi ya zamani.Naenda kula ugali na dagaa leo,tena jana jumapili nimekula

Nyasa .....Hiyo usiulize Maswali picha itakasirika ..

Usiul;ize mnyasa vipi mbona kuna mtu hapo humtaji au hao huwataji?Mimi nakupa madoido ya Nyasa wala sitaki kelele.Mimi mtoto wa kinyasa utanimbia nini wakati najua utamu wa kuishi nyasa.Ngoja kwanza...jana kulikuwa na kichekesho eti jamaa alitaka kunitwanga ngumi wakati naadaa hizi picha,kisa eti wanyasa wanajiona matawi ya juu wakati hawana lolote.Mimi nikamwambia ingelikuwa hawana lolote basi wangelikuwa vichaa kwani mungu katuwekea kitu na tunacho nacho ni ubongo hivyo huwezi kumwambia mtu hana lolote kimaisha.Labda akifanya ujinga au kuleta ujivuni wakati hana ujuzi wa kile anachokisema au kukifanya.Yaani wapo watu ambao hawapendi kuheshimu wanachofanya wenzao hata kama ni jambo dogo....Nakwambia nilikasirika nikapiga ngumi kali ukutani lakini niliumia mpaka sasa nimefungwa bandeji nauugulia sana kisa kutetea wanyasa...njooni mnipe pole hata kuandika hapa natumia mkono mmoja tu wa kushoto......mbona hamnipi pole nanyi mna kisirani na wanyasa.....nitalianzisha varangati....ooooo ngoja nipone kwanza.

Funzo La Mnyasa Hata Kama Humpendi

Wanyasa ni watu ninao waheshimu daima kwani wana msimamo juu ya maisha yao.Unaweza kumwona mnyasa akiwa kazini kama hivi ukadhani mshamba au mtu asiye na staha kabisa.Basi unajidanganya yaani utakuwa unacheka huku unalia wala usidhani kama natania.Hawa ni watu wanaopenda kufanya yale wanayoamini yanamanufaa kwa maisha yao,hawana haja ya kuharakisha maisha kwani wanajua kila kitu hupangwa na mungu huku ukiwa na uthabiti wa mipango hiyo.Sasa hebu angalia mwenyewe hapo nyavu ndiyo hiyo,matarajio ni kukomba mchuzi wa samaki wa aina yeyote.Kwanza wanaheshimu kazi yao kwa kufanya kwa utulivu.Yaani myansa hata kama humpendi kuna mafunzo utapata au muulize yule rafiki yangu kule Landani alipofika akaduwaa kwa nyodo,lakini akaona kuna jipya kwa wanyasa,mwishowe akatoa heshima zote kama askari jeshini,upo?tazama kwa hamu samaki haji bure huko mjini kwenu wavivu wakubwa .....aaaah samahani natania....unanichukia mimi myn asa?aah!lakini ...ebuu ngoja kwanza.Sawa...ngoja nikomee hapa.

Mnyasa Kazini utamwambia Nini........Hapo vipi?

Mwangalie mwanaume wa shoka akiwa amekaza msuli kwa kupata kitoweo.Huyu ndiye mnyasa yaani hapa huwezi kumwambia aache ili akaishi maisha ya mjini ya kuuza machungwa eti umachinga..acheni hizo.Mh msije mkasema nadhihaki lakini ndiyo ukweli hamuuzi maji machafu na kuadi ni maji safu ta kunywa?eeeh bvasi jamani.Ngoja kwanza kuna wakati huwa naamini kuwa maisha ya wanyasa yanalindwa sana na mola wetu.Watu wanaweza kuishi katika hali ngumu lakini wale husikii magonjwa ama milipuko ya magonjwa kama maeneo ya mijini...kazi kwetu

June 01, 2008

Watunza Afya Zetu Hao,Wapeni Malipo Mazuri

Wauguzi ni watu muhimu sana katika ulinzi wa afya za wananchi katika taifa lolote.Hebu waone hapo walijipumzisha wakisiliza mawaidha ya kuboreshwa kwa malipo na kuiomba serikali iwasomeshe kwa kiwango kikubwa au mnasemaje?Najua wanafunzi wa vyuo vikuu watasema wanataka kuwabania "mshahara wao" wanaolipwa na ile bodi,au watasema ufisadi!hapana hawa ni watu muhimu sana hao.

Hawa Ndiyo Watunza Afya zenu Jamani...

Hawa ni wauguzi ambao wanahitaji sana mafao bora,alakini usiniulize nimewatoa wapi,lakini tunaamini afya zenu zinalindwa sana na hawa