June 20, 2008

Afya Njema Nyasa

Nakumbuka kuna wakati jamaa mmoja aliwahi kunieleza kwamba mwili haujengwi kwa matofali,sikumwelewa shauri nilikuwa sipendi tabia yake ya kula vitu vingi bila ustaarabu.Basi nilipokutana na akina mama hawa nikasema......kama siyo kuishi nyasa nitaishi wapi?Wakacheka na kusema kama ninataka ndizi niseme.... Nikashangaa kwani nilikuwa nasifia nyasa wao wanasema nichukue ndizi.Mwingine akaongeza kwa kauli ileile ya yule jamaa kuwa mwili haujengwi kwa matofali.Nikaelewa,kisha nikapewa mkungu wa mmoja.Nikasema AFYA NJEMA NYASA.tukaagana nikiwa tayari nimewapiga picha hii.Imekukuna sana?Yaani mimi hunitoi hapo.... haya tuanze kushindana kula hizo ndizi..

Asubuhi Njema Na Kujipatia Kitoweo

Tunachangamka kama hivyo ili kujipatia kitoweo kwani samaki ndiyo nguzo yetu kuu.Njoo usikubali kuhadithiwa

Kuipenda Kazi Ndiyo Msingi Wa Maendeleo

Sema unaloweza lakini kwetu nyasa hapa hakuna swala la kulalamika kwamba hakuna ajira kama hao watu wa mjini.Nani atakufundisha kupenda kazi yako kama huijali na kuiheshimu.Mwangalie anavyotoa msuli wa kujituma katika kazi.Hii picha imenikuna sana,nimetabasamu sana wakati naweka kwani kuna jamaa hapa anachungulia ninavyoandika na kuiweka anashindwa kuniuliza.Lakini akiuliza tu nitamwambia amesahau kama yupo nyasa nini?Niseme nini jamani......

Mama Kabeba Kitoweo.... Nyasa

Ebu angalia tabasamu lake halafu niambie nimwambie akutayarishie nini.Wala usihofu kila kitu kipo sawa.Karibuni nyasa.Najua tayari njaa imeshakukaba shauri hao samaki wanakukuna sana.Andaa ugali wako wa muhogo halafu itazame picha hii lakini kwa wanyasa hakuna kuangalia picha bali wanakula kitoweo kamili.Usiogope muombe tu wala wanyasa siyo wachoyo

June 15, 2008

Rais Anapo Blogu,Wewe Unangoja Nini?

Mwanzo sikuamamini kabisa kwani niliambiwa na rafiki yangu kwamba kuna myasa mmoja palejirani yetu naye anablogu yake.Nikauliza huyuhuyu Rais Bingu wa Mutharika tunayemfahamu?Basi nikamtumia swali hilo rafiki yangu yule Chikoko Cryton wa Malawi pale nikamwuliza hilo...akanitumia anauani hii..

http//;www.Bingu-Mutharika-nts.blogspot.com

June 14, 2008

Maximo AKimwelekeza Jambo Shabani Nditi

Wacheaji wote wa taifa stars nawapenda sana lakini aina ya uchezaji wa Shabani Nditi unanikuna sana yaani najihisi kama nipo katikati nakula ugali wa muhogo na samaki pembeni halafu kuna mtu ananisumbua lakini kwa kunifurahisha...yani we acha hebu mwangalie anavyomsikiliza kocha wa timu ya Taifa yetu Marcio Maximo yaani rahaaaaaaa nicheke nina mwanya?

Tulimwomba Mungu Atulinde kama Hivi

Hivi wachezaji wetu walivyomwomba mungu awalinde shauri ya kuwakilisha taifa dhidi ya kameruni leo jumamosi

Twende Pamoja!!! Hivi ndivyo Walivyoshangilia Leo Dhidi ya Kameruni

Pamoja na uwezo wetu mdogo wa soka lakini tumewaonyesha Kameruni tunajua maana ya soka ....kama hivi kwa umoja wetu

Toka Nyasa Mpaka Ughaibuni

Ni uzuri wa nyasa.Ebu tazama kizazi cha nyasa hiki kutoka ughaibuni.Hapo toka kushoto Philo,dada Yasinta{yule wa blogu ya Ruhuwiko},Eric na Camilla ee bwana wamependeza au?hata kama hutaki hii ndiyo nyasa ucheke una mwanya?njoo nyasa jionee