Nakumbuka kuna wakati jamaa mmoja aliwahi kunieleza kwamba mwili haujengwi kwa matofali,sikumwelewa shauri nilikuwa sipendi tabia yake ya kula vitu vingi bila ustaarabu.Basi nilipokutana na akina mama hawa nikasema......kama siyo kuishi nyasa nitaishi wapi?Wakacheka na kusema kama ninataka ndizi niseme.... Nikashangaa kwani nilikuwa nasifia nyasa wao wanasema nichukue ndizi.Mwingine akaongeza kwa kauli ileile ya yule jamaa kuwa mwili haujengwi kwa matofali.Nikaelewa,kisha nikapewa mkungu wa mmoja.Nikasema AFYA NJEMA NYASA.tukaagana nikiwa tayari nimewapiga picha hii.Imekukuna sana?Yaani mimi hunitoi hapo.... haya tuanze kushindana kula hizo ndizi..
June 20, 2008
Afya Njema Nyasa

Madhumuni
falsafa,
familia,
mila na desturi
Asubuhi Njema Na Kujipatia Kitoweo
Tunachangamka kama hivyo ili kujipatia kitoweo kwani samaki ndiyo nguzo yetu kuu.Njoo usikubali kuhadithiwa
Madhumuni
Hisia za moyo,
zana
Kuipenda Kazi Ndiyo Msingi Wa Maendeleo
Sema unaloweza lakini kwetu nyasa hapa hakuna swala la kulalamika kwamba hakuna ajira kama hao watu wa mjini.Nani atakufundisha kupenda kazi yako kama huijali na kuiheshimu.Mwangalie anavyotoa msuli wa kujituma katika kazi.Hii picha imenikuna sana,nimetabasamu sana wakati naweka kwani kuna jamaa hapa anachungulia ninavyoandika na kuiweka anashindwa kuniuliza.Lakini akiuliza tu nitamwambia amesahau kama yupo nyasa nini?Niseme nini jamani......
Mama Kabeba Kitoweo.... Nyasa
Ebu angalia tabasamu lake halafu niambie nimwambie akutayarishie nini.Wala usihofu kila kitu kipo sawa.Karibuni nyasa.Najua tayari njaa imeshakukaba shauri hao samaki wanakukuna sana.Andaa ugali wako wa muhogo halafu itazame picha hii lakini kwa wanyasa hakuna kuangalia picha bali wanakula kitoweo kamili.Usiogope muombe tu wala wanyasa siyo wachoyo
Madhumuni
chiwindi,
kumbukumbu,
Nyasa
June 15, 2008
Rais Anapo Blogu,Wewe Unangoja Nini?
Mwanzo sikuamamini kabisa kwani niliambiwa na rafiki yangu kwamba kuna myasa mmoja palejirani yetu naye anablogu yake.Nikauliza huyuhuyu Rais Bingu wa Mutharika tunayemfahamu?Basi nikamtumia swali hilo rafiki yangu yule Chikoko Cryton wa Malawi pale nikamwuliza hilo...akanitumia anauani hii..http//;www.Bingu-Mutharika-nts.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)