Nimekwisha kusema kwamba mwezi Julai kuna dhoruba sana hivyo kama siyo wazoefu wa kusafiri kutumia meli basi nashauri kuacha.Wakati huu dhoruba kali watu wanatapika hovyo,hali ya hewa mbovu yaani mawimbi sana.Huu ni msimu wa dhoruba toka julai mpaka mwezi agosti mwishoni inategemea mabadiliko ya hali ya hewa maana inaweza kupitiliza hadi Septemba.Kuweni makini au tumieni usafiri wa magari toka Ng'ombo,Mbamba Bay,Liuli na mwambo wotewa ziwa nyasa usafiri upo Lundu, Lituhi na maeneo mengine
July 05, 2008
Muwe Makini Usafiri wa Meli Mwezi Julai
Nimekwisha kusema kwamba mwezi Julai kuna dhoruba sana hivyo kama siyo wazoefu wa kusafiri kutumia meli basi nashauri kuacha.Wakati huu dhoruba kali watu wanatapika hovyo,hali ya hewa mbovu yaani mawimbi sana.Huu ni msimu wa dhoruba toka julai mpaka mwezi agosti mwishoni inategemea mabadiliko ya hali ya hewa maana inaweza kupitiliza hadi Septemba.Kuweni makini au tumieni usafiri wa magari toka Ng'ombo,Mbamba Bay,Liuli na mwambo wotewa ziwa nyasa usafiri upo Lundu, Lituhi na maeneo mengine
Kimya Kimya Leo Mawazo Sana
Madhumuni
amani na upendo,
Liwazo,
zana
July 04, 2008
Kiangazi Mambo Huwa Bomba Sana
Kipindi hiki ziwa nyasa huamabatana na dhoruba kali sana,wakati mwingine inategemea hali ikoje maana dhoruba inaweza kuvuka hata mwezi septemba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.Lakini matajaio kuanzia septemba mambo huwa bomba sana hali inamkuna kila mmoja,watu huogelea sana ndiyo msimu wa wanyasa kupumzika kidogo.Ni kipindi safi sana ambacho kila mmoja anakifurahia,iwapo hakuna mabadiliko ya hali ya hewa.Hakika ni kipindi chetu hicho ndipo tunapoona mambo bomba sana.Inakuwa kama hivi...
Madhumuni
chinula,
kumbukumbu,
Nyasa
Yasinta Watajie Jina...Anaitwaje Huyu...
Nimesahau jina nimejaribu hadi nikataka kupiga ngumi ukuta.Lakini kuna jamaa anapenda sana kujificha mapangoni kama wale jamaa wa al Qaida,amenikumbusha eti saizi nimesahau.Haya dada Yasinta wasaidie kuwatajia jina la huyu mnyama.....halafu pale Liuli karibu na hospitali wamejazana sana kama ndiyo kambi yao
Sina Neno Hapa kazi tu
July 03, 2008
Madhumuni
kumbukumbu,
mila na desturi,
Nyasa
Ndani Ya Meli Ya Mv Songea
kwa utulivu na safari yenye uhakika.Lakini tafadhali mwezi julai siyo mzuri kwa wale wasiozoea usafiri wa meli kuna dhoruba sana mwezi huu mpaka agosti mwishoni.Karibuni nyasa utamu kolea
Madhumuni
Hisia za moyo,
Nyasa,
zana
Utulivu Wa Ziwa Nyasa
Kwa wale wanaopenda usafiri wa meli kipindi hiki siyo kizuri kwao iwapo tu siyo wavumilivu.Mwezi julai huambatana na dhoruba kali sana hivyo wale wasiozoea safari za meli hutapika sana.kwa hiyo tujihadhari kama hatujazoea mawimbi makali.Hapo ni Mbamba Bay,ukiwa mtaa wa zambia upande wa magharibi ya mji kutazama mashariki.
Madhumuni
amani na upendo,
uzuri,
wageni
Bandarini Mbamba Bay Utamu Kolea
Hapa ndipo Mv Songea inapotia nanga.Tazama kwa umakini ujione uzuri hata kama ni kidogo acha tujivunie.Unajua nini?Kuna jamaa anapenda sana kuja hapa kutazama shughuli zinavyokwenda.Mara kwa mara ukimuuliza anakwamba anaenda kumpumzika Bandarini kutazama kazi na vituko vya wanyasa visivyo na shari.Mv Iringa nayo hutia nanga hapa ila lile meli la Malawi kubwa kama nini sijui linabaki kilindini na kutumia maboti.Jamani meli kubwa hilo utafikiri za wale jamaa walioenda kuvamia uarabuni.
Madhumuni
mbamba bay,
zana
July 02, 2008
Karibuni Tena Mbamba Bay
Ukitazama mbele kabisa unaona kama kuna majengo fulani-hapo ni karibu na Hoteli ya Neema.Yaani mahali pale ni pazuri sana kuna barabara toka uwanja wa hoteli hiyo mpaka ziwani yaani unabarizi tu taratibu siyo kwa usafiri bali matembezi.Kwa wapendanao wanajua matembezi lakini mnyasa hata sijui mimi kuvua samaki tu.Hili eneo lenye mawe pana uwazi mzurisana ambao hutumika kwa kujipumzisha nyakati za mchana.Hii ndiyo Mbamba Bay ndugu yangu karibu tena mmm lakini dadangu pale Ruhuwiko bloguni anaumia shauri amekosa sana utamu wa nyasa....ngoja nitakutumia basi la ungo uje kwa kasi kisha kurejea ughaibuni.
Madhumuni
mapenzi,
mapumziko,
mbamba bay
Mnyasa Nimetua Mbinga Leo Unasemaje.......
Angalia picha hii kwa umakini halafu niambie inakupa fikra kidogo?Mmhh hapa ni barabara kuu ya Mbinga mjini pale,ukingalia kwa mbali kidogo kuna jengo au mnara fulani-hapo ni jimboni au makao makuu ya jimbo la mbinga.Sasa itazame barabara hii halafu jiulize ni mara ngapi unapenda hali hiyo,ni namna gani unaweza kuwa na ustadi wa mazingira bora au maisha bora kwa kila raia.Lakini sitaki ulaumu ila nimependa sana hii picha nilipoipiga kwa mara ya kwanza kwani inaonyesha njia kuu ya mjini na maduka pembeni.Ukiwa upande wa juu pale karibu na hoteli ya Madina njia panda ya benki ya NMB na barabara ya kwenda kiwanda cha kahawa ndipo barabara hii ilipo.Ni barabara kuu katikati ya mji.Habari ndiyo hiyooo wabunge wa jimbo la Mbinga magharibi na mashariki.
Madhumuni
kumbukumbu,
mengineyo,
wageni,
zana
June 30, 2008
Andaa Ugali Wa Muhogo
Samaki maarufu kama kandogo.kama una njaa wala hakuna shida njoo tu ule...smahani ni mbaya sana kukomba mboga.
Madhumuni
kumbukumbu,
Nyasa
Meli Imetia Nanga Mbamba Bay kwa Utulivu
Nilikwisha kusema kwamba usafiri siyo tatizo wewe njoo nyasa jioneeeee mwenyewe.Hii ni Mv Songea ambayo inafanya safari zake toka Mbamba bay hadi itungi.Pia inafika hadi Malawi katika vituo vya Nkata bay,Nsisi, na vituo vingine kisha kurejea mbamb bay hadi Itungi.
Madhumuni
mbamba bay,
zana
June 29, 2008
Sitaki Ushahidi....Je ndivyo Ilivyo?
Naandika haraka haraka leo nina mpango wa kwenda kuogelea mpaka usiku kwani kila siku natumbukia tu kidogo lakini leo ni kuogelea kwelikweli.Mmmm sasa ebu tazama katuni hiyo halafu fikirisha ubongo wako.Jaribu kujenga picha ya watoto yatima kisha fikiria wanaolea watoto hao halafu jaribu kuyafikiria mahitaji ya kiuchumi yaani kipato cha maisha.Sitaki kutoa jawabu ila jaribu kutafakari.KWA HERI mimi sitaki ushahidi lakini ndivyo ilivyo?.Ooo sijasahau...karibu sana kaka Mbilinyi katika gazeti hili la nyasa.....karibu ule vitoweo vitamu......Jamani nakwenda kuogelea webnzangu wameshaanza ona waleeee..huwaoni?utajiju..
Subscribe to:
Posts (Atom)


