July 10, 2008

Siyo Uvuvi pekee .....hata usafi pia

Ukanda wa ziwa nyasa unategemea sana maji ya ziwa nyasa kwa matumizi ya nyumbani.Wengi wamenufaika na ziwa hili kwani maeneo mengi hayana maji ya safi ya bombani.Achila mbali maeneo ya kama Mba Bay,Lundo,Chinula,Liuli na Lituhi lakini maji kwa maeneo mengi ni suala sugu.Kwa mbali wanaonekana watu wakifanya usafi wa nguo zao.Lakini yule mbunge wake sijui anafanya nini kila siku anatetea chama chake cha majambazi

July 09, 2008

kumbukumbu Profesa Chachage S Chachage

"Laiti kama wahenga waliomwaga damu yao takatifu katika vita ya ukombozi ya Majimaji wangalifufuka leo na kuwasikia wajukuu wakiusifia ubeberu na ukoloni mamboleo,bila shaka wangewakana na kulaani kwamba huu sio uzao wao"........"Utii bila uhuru ni utumwa" Jamani leo ni kumbukumbu ya mwanafalsafa wa kitanzania ambaye alifariki julai 9 2006.leo ni miaka miwili kamili tangu alipofariki.Tafura kitabu chake maridadi cha MAKUADI WA SOKO HURIA. Unajua kama mzee mkapa yule rais aliyestaafu alimchukia sana Chchage?Huyu alikuwa katika sayansi ya siasa UDSM-mlimani.Hayo ni moja ya maneno yake,huyu jamaa alikuwa kiboko waulize watawala wa enzi za mkapa.Mungu amlinde daima

Nimesahau!Ah Nyasa pale.....

July 08, 2008

Siyo Ukali Bali Anafurahia Nyasa

Kuna swali dadangu Ruhuwiko bloguni aliniuliza kuhusu huyu mnyama,nilikwepa kulijibu shauri nilikuwa natafuta kwanza picha yake na sasa nimeibamba.Ilikuwa adhuhuri fulani watu wakakusanyika kushangaa huyu mnyama wengine wakajiuliza ni Mamba gani huyu asiyejificha?Lakini ukweli ni kwamba dadangu alikuja nyasa toka ughaibuni lakini akaogopa kuogelea kisa mamba.Kimsingi huyu ni mnyama ambaye anaogopwa sana na Binadamu.Pale Liuli mzungu mmoja aliitwa Rainer alishikwa kwenye jicho na mamba mpaka kifo kikamkuta ikadaiwa ni sayansi ya kiafrika.Mimi sijui ila kwa hakika mambo wapo lakini kusema ndiyo hatari katika ziwa letu ni hapana,hawa ni wanyama ambao kila mmoja anatamani kuwaona,niambie kama unaogopa nikupe mbinu za kupuuza na kukupa nyakati za kuibuka kwa mamba ziwa nyasa.Kwa faida ya wasomaji ni kwamba nyakati za masika ni rahisi sana,hususani mwezi desemba na machi.Pia kiangazi hasa mwezi oktoba jua kali na joto kali,mamba hutokea sana vipindi hivi lakini siyo kuhatarisha maisha....hivi nimejitahidi kujibu au sijaweza?.....

July 07, 2008

Nashindwa kusema Labda nitakosea

Hivi unajifunza nini unapotazama picha kama hii.Kuna lolote unalojifunza?Niambie wewe unayeiangalia mimi sijui.Lakini jiulize wale wezi walioongozwa na yule jamaa anamvi anatoka mondulini...au monduli nini sijui.Jikomboe sasa

Mahaba Ni Raha na Faraja.....

Kuna raha,utamu,faraja,nidhamu na ukakasi.Au kuna ile hali ya kuona kwamba unaishi halafu hufurahii maisha yenyewe,unabisha?...Jamani samahani usije ukadhani kwamba nimechanganyikiwa.Lakini mahaba,raha na mafunzo ya kuyasaka yapo. hakika.Unajua kwanini.Nakumbuka wakati fulani nikiwa hapa nyasa maisha yanakwenda chini ya amri za wazazi{jambo ambalo hadi sasa nafuata amri za wazazi hao} lakini huku pembeni unastawisha gumzo,watu wanafurahia wanaona gumzo limenawiri utafikiri limewekwa mbolea kumbe mnyasa anaongoza gumzo.Gumzo lenyewe nimelikumbuka wakati ule tunatafuta ujiko mitaani si unajua mambo ya kinyasa?Basi hayo mahaba tunawaona watu yameshamiri ni raha tupu,kila mtu anaona hii ni raha na faraja.Kuona hivyo jamani mbona sisi hatuna gumzo la kustawisha mahaba na raha.Jamaa akaibuka kwamba inawezekana katika nafsi zetu hakuna maana ya mahaba..lakini tukamuuliza tutafute vipi?Eeeh jamaa akaanza ukitaka mahaba lazima uyatafute hakika hivi au ukitegemea kuwa yanakuja hilo umekosea.Basi suala lenyewe ni hili kuna rafiki yangu mnyasa hapa ana mambo ya ajabu kila siku yeye analalamikia kukosa mahaba na faraja za mahaba yenyewe.Kumbe nimegundua anaogopa kutafuta,akiona akina dada anatamani kuyasaka mahaba lakini anaogopa kuanza hata kuongea neno japo kusalimia...lakini ananilazimisha nimfundishe kuyatafuta mahaba shauri ni faraja.Nimeshindwa sababu mimi nimezoea kuvua na kutengeneza nyavu zangu shauri yake....jamani anayeweza popote ulimwenguni amsaidie au awasiliane nami hapa bloguni nimsaidie lakini tafadhali hakikasha unaweza kumtimizia maana ameniambia kuna zawadi nono kwa atakayemfundisha kuyasaka...au labda ajifunze katika blogu ya kaka Mbilinyi...ngoja nitamwambia ili anipunguzie mzigo kwani nimechoka kelele zake...lakini rafiki yangu mmmhh siwezi kuacha kumsaidia....ngoja nikomee hapa kwanza..

July 06, 2008

Mwalimu wangu Ndesanjo

Nimemkumbuka mwalimu wangu ndesanjo,Nimemkosa sana kila nikifikiria namna ninavyoringa katika blogu hii najikuta nataka kumwuliza mengine mwalimu wangu kwani bado yananipiga chenga.Njoo mwalimu wangu mwanafunzi wako nimekukumbuka sana....kuna teknolojia zingine zinanishinda....nifanyeje...ebu mwangali hapa alikuwa kwenye warsha ya mambo ya teknolojia India

July 05, 2008

Muwe Makini Usafiri wa Meli Mwezi Julai

Nimekwisha kusema kwamba mwezi Julai kuna dhoruba sana hivyo kama siyo wazoefu wa kusafiri kutumia meli basi nashauri kuacha.Wakati huu dhoruba kali watu wanatapika hovyo,hali ya hewa mbovu yaani mawimbi sana.Huu ni msimu wa dhoruba toka julai mpaka mwezi agosti mwishoni inategemea mabadiliko ya hali ya hewa maana inaweza kupitiliza hadi Septemba.Kuweni makini au tumieni usafiri wa magari toka Ng'ombo,Mbamba Bay,Liuli na mwambo wotewa ziwa nyasa usafiri upo Lundu, Lituhi na maeneo mengine

Kimya Kimya Leo Mawazo Sana

July 04, 2008

Kiangazi Mambo Huwa Bomba Sana

Kipindi hiki ziwa nyasa huamabatana na dhoruba kali sana,wakati mwingine inategemea hali ikoje maana dhoruba inaweza kuvuka hata mwezi septemba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.Lakini matajaio kuanzia septemba mambo huwa bomba sana hali inamkuna kila mmoja,watu huogelea sana ndiyo msimu wa wanyasa kupumzika kidogo.Ni kipindi safi sana ambacho kila mmoja anakifurahia,iwapo hakuna mabadiliko ya hali ya hewa.Hakika ni kipindi chetu hicho ndipo tunapoona mambo bomba sana.Inakuwa kama hivi...

Yasinta Watajie Jina...Anaitwaje Huyu...

Nimesahau jina nimejaribu hadi nikataka kupiga ngumi ukuta.Lakini kuna jamaa anapenda sana kujificha mapangoni kama wale jamaa wa al Qaida,amenikumbusha eti saizi nimesahau.Haya dada Yasinta wasaidie kuwatajia jina la huyu mnyama.....halafu pale Liuli karibu na hospitali wamejazana sana kama ndiyo kambi yao

Sina Neno Hapa kazi tu