Jua linatua magharibi yaani machweo.Hivi ndivyo linavyoonekana
July 12, 2008
Jioni Njema Nyasa
July 11, 2008
Panaitwaje Vile? Lundu
Hapa ni moja ya maeneo ya Lundu yaani hapa ndipo ukurasa mkuu wa maisha yangu ulipo.Hapa ukitazama unaona mlima huo,halafu uapnde wa kushoto ndiko uelekeo wa bandari ya Lundu ilipo.Mv Iringa na Mv Songea hutia nanga hapo,hapaonekani yaani ni kushoto zaidi kwahiyo picha ilitaka mlima.Ni ukurasa mkuu wangu wa maisha,mwone mnyasa yupo kazi na zana
July 10, 2008
Siyo Uvuvi pekee .....hata usafi pia
Ukanda wa ziwa nyasa unategemea sana maji ya ziwa nyasa kwa matumizi ya nyumbani.Wengi wamenufaika na ziwa hili kwani maeneo mengi hayana maji ya safi ya bombani.Achila mbali maeneo ya kama Mba Bay,Lundo,Chinula,Liuli na Lituhi lakini maji kwa maeneo mengi ni suala sugu.Kwa mbali wanaonekana watu wakifanya usafi wa nguo zao.Lakini yule mbunge wake sijui anafanya nini kila siku anatetea chama chake cha majambazi
July 09, 2008
kumbukumbu Profesa Chachage S Chachage
"Laiti kama wahenga waliomwaga damu yao takatifu katika vita ya ukombozi ya Majimaji wangalifufuka leo na kuwasikia wajukuu wakiusifia ubeberu na ukoloni mamboleo,bila shaka wangewakana na kulaani kwamba huu sio uzao wao"........"Utii bila uhuru ni utumwa" Jamani leo ni kumbukumbu ya mwanafalsafa wa kitanzania ambaye alifariki julai 9 2006.leo ni miaka miwili kamili tangu alipofariki.Tafura kitabu chake maridadi cha MAKUADI WA SOKO HURIA. Unajua kama mzee mkapa yule rais aliyestaafu alimchukia sana Chchage?Huyu alikuwa katika sayansi ya siasa UDSM-mlimani.Hayo ni moja ya maneno yake,huyu jamaa alikuwa kiboko waulize watawala wa enzi za mkapa.Mungu amlinde daima
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha,
siasa.
Nimesahau!Ah Nyasa pale.....
July 08, 2008
Siyo Ukali Bali Anafurahia Nyasa
Kuna swali dadangu Ruhuwiko bloguni aliniuliza kuhusu huyu mnyama,nilikwepa kulijibu shauri nilikuwa natafuta kwanza picha yake na sasa nimeibamba.Ilikuwa adhuhuri fulani watu wakakusanyika kushangaa huyu mnyama wengine wakajiuliza ni Mamba gani huyu asiyejificha?Lakini ukweli ni kwamba dadangu alikuja nyasa toka ughaibuni lakini akaogopa kuogelea kisa mamba.Kimsingi huyu ni mnyama ambaye anaogopwa sana na Binadamu.Pale Liuli mzungu mmoja aliitwa Rainer alishikwa kwenye jicho na mamba mpaka kifo kikamkuta ikadaiwa ni sayansi ya kiafrika.Mimi sijui ila kwa hakika mambo wapo lakini kusema ndiyo hatari katika ziwa letu ni hapana,hawa ni wanyama ambao kila mmoja anatamani kuwaona,niambie kama unaogopa nikupe mbinu za kupuuza na kukupa nyakati za kuibuka kwa mamba ziwa nyasa.Kwa faida ya wasomaji ni kwamba nyakati za masika ni rahisi sana,hususani mwezi desemba na machi.Pia kiangazi hasa mwezi oktoba jua kali na joto kali,mamba hutokea sana vipindi hivi lakini siyo kuhatarisha maisha....hivi nimejitahidi kujibu au sijaweza?.....
July 07, 2008
Nashindwa kusema Labda nitakosea
Hivi unajifunza nini unapotazama picha kama hii.Kuna lolote unalojifunza?Niambie wewe unayeiangalia mimi sijui.Lakini jiulize wale wezi walioongozwa na yule jamaa anamvi anatoka mondulini...au monduli nini sijui.Jikomboe sasa
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha,
zana
Mahaba Ni Raha na Faraja.....
Kuna raha,utamu,faraja,nidhamu na ukakasi.Au kuna ile hali ya kuona kwamba unaishi halafu hufurahii maisha yenyewe,unabisha?...Jamani samahani usije ukadhani kwamba nimechanganyikiwa.Lakini mahaba,raha na mafunzo ya kuyasaka yapo. hakika.Unajua kwanini.Nakumbuka wakati fulani nikiwa hapa nyasa maisha yanakwenda chini ya amri za wazazi{jambo ambalo hadi sasa nafuata amri za wazazi hao} lakini huku pembeni unastawisha gumzo,watu wanafurahia wanaona gumzo limenawiri utafikiri limewekwa mbolea kumbe mnyasa anaongoza gumzo.Gumzo lenyewe nimelikumbuka wakati ule tunatafuta ujiko mitaani si unajua mambo ya kinyasa?Basi hayo mahaba tunawaona watu yameshamiri ni raha tupu,kila mtu anaona hii ni raha na faraja.Kuona hivyo jamani mbona sisi hatuna gumzo la kustawisha mahaba na raha.Jamaa akaibuka kwamba inawezekana katika nafsi zetu hakuna maana ya mahaba..lakini tukamuuliza tutafute vipi?Eeeh jamaa akaanza ukitaka mahaba lazima uyatafute hakika hivi au ukitegemea kuwa yanakuja hilo umekosea.Basi suala lenyewe ni hili kuna rafiki yangu mnyasa hapa ana mambo ya ajabu kila siku yeye analalamikia kukosa mahaba na faraja za mahaba yenyewe.Kumbe nimegundua anaogopa kutafuta,akiona akina dada anatamani kuyasaka mahaba lakini anaogopa kuanza hata kuongea neno japo kusalimia...lakini ananilazimisha nimfundishe kuyatafuta mahaba shauri ni faraja.Nimeshindwa sababu mimi nimezoea kuvua na kutengeneza nyavu zangu shauri yake....jamani anayeweza popote ulimwenguni amsaidie au awasiliane nami hapa bloguni nimsaidie lakini tafadhali hakikasha unaweza kumtimizia maana ameniambia kuna zawadi nono kwa atakayemfundisha kuyasaka...au labda ajifunze katika blogu ya kaka Mbilinyi...ngoja nitamwambia ili anipunguzie mzigo kwani nimechoka kelele zake...lakini rafiki yangu mmmhh siwezi kuacha kumsaidia....ngoja nikomee hapa kwanza..
Madhumuni
habari,
Hisia za moyo,
mapenzi
July 06, 2008
Mwalimu wangu Ndesanjo
Nimemkumbuka mwalimu wangu ndesanjo,Nimemkosa sana kila nikifikiria namna ninavyoringa katika blogu hii najikuta nataka kumwuliza mengine mwalimu wangu kwani bado yananipiga chenga.Njoo mwalimu wangu mwanafunzi wako nimekukumbuka sana....kuna teknolojia zingine zinanishinda....nifanyeje...ebu mwangali hapa alikuwa kwenye warsha ya mambo ya teknolojia India
Subscribe to:
Posts (Atom)

