July 16, 2008

kumbukumbu unaionaje hii

ni vema kujivunza mengi lakini siyo kujua kila kitu unatakiwa kuwa bingwa wa ubunifu,mtumwa ndani ya jamii mapinduzi kila siku.Wewe ukipata mia moja,sifuri atapewa nani?...Kumbukumbu tu hii

July 15, 2008

ujumbe wa leo

'Utii bila uhuru ni utumwa'

July 14, 2008

uzuri wa nyasa?ngoja nikuambie

Tazama vizuri usije ukafikiria hapa ni peponi..natania lakini karibu nyasa

Kumbukumbu + Nyasa + Uzuri

Wapi pale,ni pwani ya mbamba bay au unaonaje mwenzangu.Tazama hii picha halafu ninong'oneze asisikie yule Yasinta wa Ughaibuni...itakuwa varangati...uatajuaje kama natania.Ni mbamba bay pwani ya ziwa nyasa

July 13, 2008

Asante Yasinta kwa kumbukumbu

July 12, 2008

Jioni Njema Nyasa

Jua linatua magharibi yaani machweo.Hivi ndivyo linavyoonekana

July 11, 2008

Panaitwaje Vile? Lundu

Hapa ni moja ya maeneo ya Lundu yaani hapa ndipo ukurasa mkuu wa maisha yangu ulipo.Hapa ukitazama unaona mlima huo,halafu uapnde wa kushoto ndiko uelekeo wa bandari ya Lundu ilipo.Mv Iringa na Mv Songea hutia nanga hapo,hapaonekani yaani ni kushoto zaidi kwahiyo picha ilitaka mlima.Ni ukurasa mkuu wangu wa maisha,mwone mnyasa yupo kazi na zana