Rafiki yangu Cryton Chikoko alinitumia picha hii.Ni meli kubwa sana lakini siyo kuifikia ile ya Mv Mtendele.Hapo ipo katika moja ya safari zake.
August 03, 2008
Mv Ilala ya Malawi katika ziwa nyasa
Rafiki yangu Cryton Chikoko alinitumia picha hii.Ni meli kubwa sana lakini siyo kuifikia ile ya Mv Mtendele.Hapo ipo katika moja ya safari zake.
July 31, 2008
wanyasa wakiwa na mitumbwi yao
ni zana ambayo inatufanya turinge sana.unajua kuna washashi wanapenda sana mitumbwi?wengine walifikiri kutumia mitumbwi ni umasikini,basi siku moja nikawaambia wengine kuwa huo ni utamaduni siyo umasikini.wakanywea wakawa kimya,wakaona kumbe siyo lazima kutumia maboti yao.
July 30, 2008
nyasa tu
Nisemavyo mnyasa leo
Ngoja leo nijikumbushe kuandika kama nilivyokuwa awali.Unajua nilikuwa naandika tu bila kuweka picha hapa kijijini?Kilichonifanya niandike tena ni kuona watu wana akili za mseto.Nikikwambia watu wanaakili za mseto ujue hakika zimejichanganya zile zenye uvundo,uozo na zile zenye hekima za kudunduliza.Kwanini watu hawataki kuamini kwamba uwezo wao ni fimbo ya maisha?Kuna sababu gani watu kulilia peremende yenye mchanga?Ni hivi sijui leo nikasirishwa au ninawaza nini lakini naona ninachoandika hakieleweki.Labda nimechanganyikiwa.Acha bwana waenze zao huko wasitake kunighasi mnyasa miye kwani wananini,hawaniwezi navua samaki sana tu.Kuna sababu ya kumghasi mtu katika maisha yake?Ngoja,ni hivi natumia muda mwingi kupambana kuendeleza msingi wa maisha lakini najikuta nataka kukwama eti sababu naona fulani kapendeza au nahisi ana maisha maridadi,jamani huu upungwani nimeuvaa hapa leo hakika hata sijui naandika nini. Hivi nimejieleza vizuri au sieleweki hata kidogo?Mmmh labda nimechanganyikiwa kwani leo nahisi hali tofauti.ngoja nikapumzike kidogo pale ufukweni labda nitapata wazo zuri baadaye.aaaaaah nimekumbuka,hivi kuna sababu ya mimi kulazimisha kuwa kama wengine mfano maisha,itikadi,itifaki,falsafa na mengineyo?.Umenielewa?ngoja bado aaaah acha nipumzike kwanza
July 28, 2008
umewahi kufika kijiji cha Mkili......
kama hujawahi basi hapa ni pale kijijini mkili,pale penye bandari ya meli yetu ya Mv songea.Pale mahali pana sifa moja ya mawimbi makali nyakati za masika.Yanaitwa Lulenga,basi nakumbuka mwaka 1999 mwezi januari nikiwa nakwenda shule pale lundo.Meli Mv Iringa ilipigwa mawimbi pale bandarini hadi nahodha Mzee Mwaisunga akasema inabidi kuiondoa meli kabla mawimbi hayajaharibu zaidi.Pia ziwa nyasa lina sifa kuu ya dhoruba kali,mfano Wasiozoea hawapendi kusafiri kutumia meli kipindi hiki hutumia magari shauri ya dhoruba.kaa chonjo kipindi hiki.
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
liuli
Subscribe to:
Posts (Atom)
