August 04, 2008

gumzo,michapo na mseto

nashangaa hata sijui nataka kuandika nini lakini najikuta nataka kuandika.Ngoja kwanza,kuna kitu kinanifurahisha sana halafu sikijui sawasawa lakini najiona nina furaha toka jana niliofanya.Haa utashangaa eti sikijui huku nakifanya-ngoja ni hivi nahisi naandika lakini sijui naadika nini ambacho wanyasa wenzeangu wanafurahia. Nilikuwa mbinga juzi bwana nikaona jinsi watani wangu wamatengo wanavyochakarikia samaki,yaani wanahaha wananunua pale karibu na kituo cha mabasi katika soko la samaki.Aise niliwaona wanahangaika na kusukumana kisa kitoweo toka nyasa.Hivi najieleza vizuri kweli?unanielewa mnyasa mwenzangu?Nimekumbuka tena wenzenu huku nyasa sasa ni kula mpuchulela/kisamvu,kuoposha mandongo/kula mlenda,chaina bila kusahau mangatongo/eti wengine waita mbegu za upupu kazi kwenu.Huu ni msimu wa samaki kupotea shauri ya kuogopa kwisha(natania)naona kila mtu anahaha kupata japo kidogo mpuchulela.Mmh ni hivi nimepata kitabu kile cha 'makuadi wa soko huria' kiliandikwa na porofesa/profesa chachage chachage.unajua wanyasa kuatmka profesa ni kazi nzito sana?wao huita porofesa au yule osama wanaita usama/hosama.Unaielewa au nianze upya?Nahisi sijui kujieleza vizuri sijui nimepagawa na nini lakini najua kitabu hiki kinanikuna sana nasoma hadi maandishi yafutike yote.Mmm ngoja hivi kuna sababu ya watu kublogu?aah bora uniue kabisa kuliko kunizuia kublogu aise patachimbika yaani hapatoshi na mwendo wa kutunisha misuli tu. Ngoja nikomee hapa na michapo ya mseto

August 03, 2008

Mv Ilala ya Malawi katika ziwa nyasa

Rafiki yangu Cryton Chikoko alinitumia picha hii.Ni meli kubwa sana lakini siyo kuifikia ile ya Mv Mtendele.Hapo ipo katika moja ya safari zake.

July 31, 2008

wanyasa wakiwa na mitumbwi yao

ni zana ambayo inatufanya turinge sana.unajua kuna washashi wanapenda sana mitumbwi?wengine walifikiri kutumia mitumbwi ni umasikini,basi siku moja nikawaambia wengine kuwa huo ni utamaduni siyo umasikini.wakanywea wakawa kimya,wakaona kumbe siyo lazima kutumia maboti yao.

July 30, 2008

nyasa tu

Nisemavyo mnyasa leo

Ngoja leo nijikumbushe kuandika kama nilivyokuwa awali.Unajua nilikuwa naandika tu bila kuweka picha hapa kijijini?Kilichonifanya niandike tena ni kuona watu wana akili za mseto.Nikikwambia watu wanaakili za mseto ujue hakika zimejichanganya zile zenye uvundo,uozo na zile zenye hekima za kudunduliza.Kwanini watu hawataki kuamini kwamba uwezo wao ni fimbo ya maisha?Kuna sababu gani watu kulilia peremende yenye mchanga?Ni hivi sijui leo nikasirishwa au ninawaza nini lakini naona ninachoandika hakieleweki.Labda nimechanganyikiwa.Acha bwana waenze zao huko wasitake kunighasi mnyasa miye kwani wananini,hawaniwezi navua samaki sana tu.Kuna sababu ya kumghasi mtu katika maisha yake?Ngoja,ni hivi natumia muda mwingi kupambana kuendeleza msingi wa maisha lakini najikuta nataka kukwama eti sababu naona fulani kapendeza au nahisi ana maisha maridadi,jamani huu upungwani nimeuvaa hapa leo hakika hata sijui naandika nini. Hivi nimejieleza vizuri au sieleweki hata kidogo?Mmmh labda nimechanganyikiwa kwani leo nahisi hali tofauti.ngoja nikapumzike kidogo pale ufukweni labda nitapata wazo zuri baadaye.aaaaaah nimekumbuka,hivi kuna sababu ya mimi kulazimisha kuwa kama wengine mfano maisha,itikadi,itifaki,falsafa na mengineyo?.Umenielewa?ngoja bado aaaah acha nipumzike kwanza