August 23, 2008

Haya tena kama kawaida wanyasa

najua wengine mmenuna eti kisa sijablogu kwa wiki kadhaa,jamani ni majukumu haya kuvua samaki kwahiyo tuliondoka kijijini kwetu kwenda vijiji vya mbali kuvua samaki kwahiyo hata muda wa kwenda mbinga mjini ikawa ngumu sanna.Eti leo hata dada Janeth kaandika ujumbewa hasirakwanini sijablogu na nimeweka picha zamani sana.Niliomba msamaha lakini inaonekana hana raha na kasi ya kublogu siku hizi.Haya kama kawaida wanyasa nipo tena. sijasahau kuna habari ya kutembea peku hebu isome hapo kaka Mbilinyi

August 18, 2008

historia hii

nimelikumbuka kanisa hili lipo pale Makwai au nakosea dadangu Yasinta.nakumbuka enzi zile nikiwa lundo

August 17, 2008

yaleyale ya kuvua kusaka kitoweo

mnyasa kwa kuwasaka samaki humuwezi yaani anajua majira ya kila aina kwa samaki mbalimbali.Karibuni nyasa,si unaona hapo walivyobize na kazi yao