August 28, 2008

kumbukumbu tena

Nilikwisha kueleza kwamba kipindi hiki siyo kizuri kwa wale wasiozoea usafiri wa meli shauri ya dhoruba kali. Sasa kuna dhoruba ambayo kwa wale wasoizoea wanaweza kujikuta akisafiri kama yupo rumande. Dhoruba ni kali sana kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwezi septemba kwahiyo wanaweza kutumia magari kwa barabara za Mbamba bay au ile ya jijini Mbeya

Karibuni nyasa

jionee fahari,nyasa nakupenda sana. kuna yeyote ana hoja kwamba hii siyo hali halilisi ya nyasa?jieleze

Mv Ilala kazini

ukija mbamba bay unaweza kwenda Malawi kwa kutumia meli hii hata kama una mizigo mikubwa kiasi gani.Kwa ile Mv Mtendele inashindwa kutia nanga shauri ya bandari yetu mbamba bay ni ndogo

August 27, 2008

Pekupeku

Ndiyo sijaiba wala sikuruhusiwa kuitumia picha hii lakini imenikumbusha mbali sana. Kaka yangu Mbilinyi kaanza mazoezi ya kutembea pekupeku,yaani wakati ule ukijifanya unavaa kandambili basi huonekana ufahari sana. jamani kutembea pekupeku hapa nyasa ni kama utamduni na maisha yenyewe lakini tunaulamba suti nakadhalika

August 23, 2008

Haya tena kama kawaida wanyasa

najua wengine mmenuna eti kisa sijablogu kwa wiki kadhaa,jamani ni majukumu haya kuvua samaki kwahiyo tuliondoka kijijini kwetu kwenda vijiji vya mbali kuvua samaki kwahiyo hata muda wa kwenda mbinga mjini ikawa ngumu sanna.Eti leo hata dada Janeth kaandika ujumbewa hasirakwanini sijablogu na nimeweka picha zamani sana.Niliomba msamaha lakini inaonekana hana raha na kasi ya kublogu siku hizi.Haya kama kawaida wanyasa nipo tena. sijasahau kuna habari ya kutembea peku hebu isome hapo kaka Mbilinyi