August 31, 2008

Ni kumbukumbu yangu leo nawapenda nyote

Nimetimiza mwaka mmoja tangu nilipoanza kuandika makala katika gazeti la RAI,ingawaje nilkitimiza mwaka mmoja mwezi aprili tangu nilipoanza kuandika makala lakini kwa hakika hili ni gzeti kubwa TZ kwahiyo kuadnika makala katika gazeti hili ni ndoto.Nilipenda kuandika katika gazeti hili wakati ule likiwa chini ya ninayemwita 'Mwanafalsafa' mze wangu Jenerali Ulimwengu,nina mpenda sana.Ingawa sasa anamekwisha kuanzisha gazeti lingine la Raia Mwema, soma www.raiamwema.co.tz bado naamini ipo siku nitafanya kazi na mzee huyu hakika nakipenda kichwa chake kina utajiri wa fikra. Najipongeza kwa kuwaambieni nawapenda nyote. Pia najipongeza tangu nilipoanzisha Blogu yangu,nayo leo nimetimiza mwaka mmoja sasa na kwa kiasa fulani inanipa moyo kwani nimepata marafiki wengi ambao wananishauri na tunawasiliana sana. Sina cha kuwaambia zaidi ya NAWAPENDA SANA,TUPO PAMOJA KAMA SAMAKI NA MAJI.
Amina, adumu sana ndugu yetu Ndesanjo Macha

hata mkibisha lakini tunavyo hivi

sina hakika kama kweli tunavifahamu hivi viti lakini kwetu tunaita HINGOLOMBI/VINGOLOMBI yaani hata wale waliodhani havina maana walianza kuibeza picha lakini nikasema poa mimi siviachi katu.Vipo vingi sana huku nyasa,nakumbuka maiaka ya nyuma tulitumi kama vijiko kwa ajili ya uji. Mambo yalikuwa bomba sana yaani nikivitazama vinanikumbusha mbali sana hata kama nina umri mdogo.

August 28, 2008

kumbukumbu tena

Nilikwisha kueleza kwamba kipindi hiki siyo kizuri kwa wale wasiozoea usafiri wa meli shauri ya dhoruba kali. Sasa kuna dhoruba ambayo kwa wale wasoizoea wanaweza kujikuta akisafiri kama yupo rumande. Dhoruba ni kali sana kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwezi septemba kwahiyo wanaweza kutumia magari kwa barabara za Mbamba bay au ile ya jijini Mbeya

Karibuni nyasa

jionee fahari,nyasa nakupenda sana. kuna yeyote ana hoja kwamba hii siyo hali halilisi ya nyasa?jieleze

Mv Ilala kazini

ukija mbamba bay unaweza kwenda Malawi kwa kutumia meli hii hata kama una mizigo mikubwa kiasi gani.Kwa ile Mv Mtendele inashindwa kutia nanga shauri ya bandari yetu mbamba bay ni ndogo