September 09, 2008

hakuna kulala

September 06, 2008

umewaona hawa jamaa vema?

kwahiyo hawa jamaa yaani mama na mwana wanataka kushindana na mimi. hiyo olimpiki nawaambi kasi mlete daktari wa kuwatibu au natania? ndiyo nao wanajiandaa kwa olimpiki ijayo huko London kwa Toni BULEYA na mwenzie Godoro la KAHAWIA pamoja na MALIKIA ELIZETI. nakwambia hamnipiti mnajua dawa za Lupocho,Ntambitambi,Ngelengana,Matungulusi,na N'kwanchu? nakwambia. haya njooni huku nyasa muone jasho na damu... lakini nawapenda sana eti eeeh. Sitaki naona mnataka kuniharibia maandalizi{natania}. oooo nipo bize marafiki tuonane labda London kwa siku moja tu tutaongea najua hiyo hali hampendi lakini nina mambo mengi....nina mzizi ya kila kitu nawaambia mtavua jezi hizo sawa?{natania}

Olimpiki 2012 nyie chekeni tu...kazi ipo

Haya tena dadangu Yasinta kacheka sana niliposema maandalizi ya olimpiki nayaanza. unajua kwanini anacheka? ngoja nikumegee siri...aaah nimeghairi usije ukamwambia lakini sikiliza najua anawivu hawezi kukimbia mita 10000,pia 100 inamsumbua si umemuona alivyo? labda enzi zile akiwa kama Madonna mwaka 1992 angeliweza lakini sasa thubutu yake atajiju leo. Nakwambia sasa ni shughuli kwelikweli sitaki blah blah hapa wala mzaha. Najua hata Erick hawezi kuufikia moto huu yaani ni zaidi ya Usain Bolt yule jamaa anayetokea kule walikuwa wanahusudu sana BLACK BAMBOO eti sasa wanatingisha dunia kwa kukimbiza upepo. Asikwambie mtu yaani mpango wa kwanza kwenda kutambika mizimu kule BUTIAMA kwa Mwalimu JK Nyerere hakua kwere hapa. baada ya kutafuta pumzi sasa inatafutwa kasi. Ngoja nitakwambi nilitumi muda gani mita 10000 lakini mpaka nikaague kwanza kwa mganga ili nijue nitakimbia muda gani.....

September 05, 2008

Harakati za Olimpiki....London 2012

Kama mlidhani ni dhihaka basi mlikosea sana, najua kaka Mbilinyi na dada Yasinta wataanza kucheka hadi meno yawaanguke. Hakika mtajiju leo,nawaambia harakati za olimpiki zimekwisha kuanza,yaani hapo ni saa 6 mchana jua lilikuwa kali lakini wapi bwana kazi tu. Unamuona huyo jamaa anayjifanya swala tano(natania) ni Bwana Thomas naye ni kichwa ambacho kinakwenda pale chuo kikuu Dodoma,yeye isyo swala tano bali manjonjo tu hapo kanipa maziwa kupozea makali. Yaani nawambia kama mwadhani utani ebu waleta hao Erick na Yasinta niwaonyeshe sughuli pevu. Sasa nimeanza kukimbia mita 10,000 baada ya kufanikiwa ile ya 5,000 na 3,000 lakini msiniulize muda niliotumia msije mkafa kwa kihoro na wivu ati kwakuwa nimempiku Bolt na Powell huku nikumkumbuka kipenzi changu Josiah Thungwane toka kwa mzee madiba mandela. Nimepumzika kidogo wiki hili kuvua samaki lakini nimebanika wengi mno njooni mle kama vya watu vinaliwa ...mtalipa

siyo kuvua samaki pekee.......hata hii pia

hivi ni vichwa ambavyo vilikuwa vikinisumbusa sana.Utakuta kwa siku anaweza kukuletea maswali hata matano ambayo unaumia kichwa ile mbaya. Ni vichwa toka sekondari ya Magoza kule Tabata Segerea karibu na gerezani, usije ukadhani ni wafungwa hawa ni wanafunzi. Pembeni ni mkuu wa Taaluma Mrs Mbota. Halafu hicho kichwa kilichopo jirani nami ni Rahma Omary,halafu wenzake ni Mary Ndonde(toto la kinyasalipo mjini), na Elizabeth aliye na tabasamu. kwahiyo wanyasa hata hii tumo au unadhani kuvua samaki tu....hola hiyo...hapo acha utundu wa kompyuta

September 04, 2008

njaa inauma sana waungwana? karibuni kitoweo

shibe mwana malevya..... njaa mwana malegeza..... kulala na njaa kupenda....