Mitumbwi imetu;lizana baada ya kazi yake
October 01, 2008
zana za kazi hizi
Madhumuni
amani na upendo,
urafiki,
uzuri
September 29, 2008
kama... kama ... kama nini?
aaaaaah acha niseme bwana kwani huwa siataki ushahidi mwenzenu bali naweka tu hapa mjionee ninayoyaona miye.mengine niliyaona kale lakini nilikuwa haifadhi bila kujua wapi nitaweka lakini shajara zinarahisisha mambo kama hivi. Hivi ni kama... kama.. kama nini? eti unaonaje?
Madhumuni
familia,
kumbukumbu,
maisha,
Nyasa,
urafiki
September 27, 2008
SONGEA LEO HII ; Afungwa maisha kwa kulawiti
IMEANDIKWA NA HAPPY KULANGA,
SONGEA
Mkazi wa kijiji cha Mageuzi Mlilayoyo wilayani Songea Vijijini bwana Maneno Katuna(24) amehukumiwa kifundo na mahakama ya wilaya ya Songea baada ya kukiri kosa la kumlawiti mtoto wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Mageuzi mwenye umri wa miaka 8. Mwendesha mashtka Inspekta Patrius Mlowe alieleza mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Joseph Emmanuel Foyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 16 mwaka huu asubuhi kwa kumlaghai mtoto huyo kuwa anataka kumpa Chai. Aliiambia mahakama kuwa baada ya mtoto huyo kuingia ndani alimvua nguo na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile na kumsababishia maumivu makali hata akshindwa kutembea. Alisema mtoto huyo aligundulika na wasamaria waliokuwa wakipita jirani na nyumba hiyo walimwona mtoto huyo akilalamika kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata. Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake alikiri kosa na kuiomba mahakama imsaidie kwa maelezo kuwa umri wake kuwa mdogo na anahitajika katika ujenzi wa taifa. Hata hivyo madai yake yalitupiliwa mbali na hakimu Fovo ambaye aliamua kumhukumu kwenda jela maisha yake yote,akisema adhabu hiyo ni fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

habari,
kumbukumbu,
maisha
kwa wanaotaka kwenda majuu - III
kila la heri mnaotaka kwend majuu ila mjue wala sichukii na wala sina kinyongo. Msidhani nawaonea wivu kwani najua kimsingi wivu humuua mtu mjinga. Mbinu za kutaka misaada na yale ya BRAIN DRAIN saswa tu hakuna maneno msidhani nawashambulia.Sina uuwezo wa kuwashambulia mimi binadamu mwenye nafasi ndogo katika maisha yako.Ninachosisitiza ni kwamba nenda ughaibuni kwa mipango,jiandae,kuwa mkamilifu,soma tamaduni zao,kuwa mwangalifu,amini kwamba mipango,jiwekee malengo huko uendako,usidanganyike na wapenzi/mapenzi/mpenzi..lakini kuwa makini kwa kila hatua.
September 26, 2008
uzuri+utulivu = wageni mnakaribishwa
nchuwa/bao.........................jaza jina unalolijua
Madhumuni
amani na upendo,
kumbukumbu,
Liwazo,
maisha,
utulivu,
uzuri
kwa wanaotaka kwenda majuu - II
Awali nilikuwa sielewi kwanini hawa watu wangu wanataka kuondoka nchini mwetu, lakini baadaye nilipokuwa Uchina na bwana Mao rais wa pale nilielewa sababu zao kwani nilikutana nao wataalamu wetu walioondoka Tanzania. Walinieleza sababu zao zenye maana kabisa,nikaelewa kwamba wanamipango mizuri. ...hata hivyo nikawaambia msisahau nyumbani jamani si mnajua kule mmewaacha ndugu zenu. kumbukeni hata sisi tulisomeshwa na mkoloni halafu tukapambana naye kwahiyo hata ninyi mnaweza kupambana nami kama sifanyi yale yanayowapendeza,huo ni utumiaji wa elimu. Sasa mkiondoka hawa wasiojua kitu watapambana vipi,watanitikisa vipi wakati siwaogopi. Lakini vijana wetu wakifundishwa kwenda mahala bila mipango,kuondoka kinyemela kwa ahadi za watu wasiowajua wala utamaduni wao,nadhani taifa litaaibika sana. Mnamwachia Mwl.NYERERE kupamba na umasikini kwani yeye ndiye aliwaletea? Haaa(kicheko). Lakini ninyi watu lazima mfikiri siyo kuhubiri tu maghorofa ya ulaya na amerika hapa..hayakuja bure shauri yenu....na...na ....na elimu yenu bado mnawapatia kila jambo hawa ndugu zetu...(wazungu).Msidhani kwamba mnyasa ninaandika mambo gani..kwani naona ile kasi ya kutaka kuishi majuu kwa kusingizia kusoma na wengine kutafuta kazi imezidi sana.Wabongo hayo maneno ni ya huyu mzee pichani JULIUS KAMBARAGE NYERERE.kama siku ya mwisho kuwepo duniani ningelikuwa naye,ningelimuomba kichwa chake yaani ubongo wake tu basi. Lakini kama kweli tunadhani elimu bora iko huko ughaibuni,elimu yetu airekebishe nani? tukisha soma huko basi tunaomba kazi hukohuko tena kufagia n.k baada ya hapo unarudi bongo unalalamika mbona hali haibadiliki? eboo! huna adabu akubadilishie nani wakati ulipomaliza shule hukurudi kuibadilisha si ulikwenda kuishi na yule Mwenyekiti wa Marais waongo duniani Joji Kichaka? Natumia lugha kali bila kutumia tafsida ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi. Mungu akupe hekima Ndesanjo Macha, Fred Macha nipo nanyi daima.Jikomboe. Uhuru daima
Subscribe to:
Posts (Atom)