October 04, 2008

OKTOBA ni mwezi wa historia ya afrika

nadhani mwajua yanayojiri kwamba ni mwezi wa historia ya afrika huko Uingereza. Mwezi Februari ni huko Marekani. Lakini swali, JE HISTORIA YA AFRIKA IMEANDIKWA IPASAVYO? NI KWELI KWAMBA USTAARABU WA AFRIKA ULIANZIA MISRI, LAKINI NI KWELI KWAMBA MISRI HAWAKUISHI WATU WEUSI AU MAPIRAMIDI HAYAKUJENGWA NA WEUSI? tafakari
Jikomboe. Uhuru daima

jamani vipi mmekwisha kusahau mwezi huu?

Jamaa huko ughaibuni wanasherekea historia ya mtu mweusi(waafrika) ndiyo ni huko uingereza kwa makamu mweyekiti wa viongozi wezi wa kura na waongo bwana Godi Blauzi sijui ni kinara mkuu wa uingereza.kumbuka mwenyekiti wa marais waongo na wezi wa kura ni Joji Kichaka kule washing..... huko majuu wanasherekea historia yetu watu weusi mwezi huu oktoba eti disko litakuwa huko Leicester sikwea na palase sijui. Historia yenyewe wanaipotosha kuhusu mtu mweusi tangu kule Misri. ndiyo maana nimeweka mtandano wa DAILY MOTION mjionee ukweli wetu watu weusi

karibuni nyasa

njooni nyote marafiki na waio marafiki nyote mwakaribishwa
UZURI ZAIDI

October 01, 2008

zana za kazi hizi

Mitumbwi imetu;lizana baada ya kazi yake

September 29, 2008

kama... kama ... kama nini?

aaaaaah acha niseme bwana kwani huwa siataki ushahidi mwenzenu bali naweka tu hapa mjionee ninayoyaona miye.mengine niliyaona kale lakini nilikuwa haifadhi bila kujua wapi nitaweka lakini shajara zinarahisisha mambo kama hivi. Hivi ni kama... kama.. kama nini? eti unaonaje?