October 12, 2008

hamu+utamu+uzuri+utulivu=nyasa

smaki aina ya ngorokoro
korido za Mv Ilala ambayo hufanya safari zake toka Malawi-Tanzania. hii ni mali ya Malawi na yapili kwa ukubwa baada ya Mv Mtendele

October 11, 2008

ufukweni kijijini kwetu LUNDU

hapa ni kijijini kwetu LUNDU. halafu ukiangalia nembo ya LUNDU upande wa kulia utaona watu wanafurahi sana ni utundu mdogo. sasa hapa ndiyo kwangu yaani kijiji nilichozaliwa.karibuni msije mkaja na pombe hatutaki

ni maisha tu kwani nani anajali hali hii

mafisadi nao wanatumalizia kitoweo cha maendeleo

October 09, 2008

habari ndiyo hiyo

hapa hakuna la mnadi swala wala sauti za kanisa, mchezo ni kujiburudisha, mchezo kufurahi yanini kujibana wakati muda wenyewe robo eti tutakwenda peponi mmmm

October 08, 2008

Labda leteni huku nyasa

sijaomba picha hii, lakini poa tu. Kuna jamaa walevi wanapenda sana hivi vitu. wengine wakunywa eti kupoteza mawazo. ebo nani kakwambieni mawazo yanapotezwa? mnajidanganya,mkipoteza mtapata wapi mengine. ndiyo nimechukua hapo bloguni Ruhuwiko kwa wanywa ulanzi na chimpunu(natania). jamani ukitaka kuwa na urafiki bora nami ni vema ukatofautisha haya makopo na nami. kama unasema unataka kupiga gumzo nami hakikisha pembeni hakuna makopo kama hayo. hata kama iwe mnasema 'mtoko' au 'matembezini' nakwambia nakuachia mtoko wako ukiniletea hayo makopo kama vipi kunywa kwa muda wako kisha harufu yako usilete kwangu au vipi waungwana. Unajua nini hapa nyasa hakuna, kwahiyo washamba tumekuwa wengi nasikia ukinywa tu unakufa. Kuna daktari mmoja alipogundua kwamba nina damu nyingi aliniuliza eti kama nakunywa pombe nusura nimzabe kibao, nikamwambia akome na akomae au vipi. karibuni nyasa lakini ONYO usije na hayo makopo ni haramu

maswali magumu

Mwanablogu Yasinta Ngonyani aliandika kuhusu yeye katika blogu yake. Ilikuwa Agosti 23, 2008 kwamba udadisi kwake ni sehemu ya maisha, akaongeza kwamba katika hali hiyo amejikuta amepoteza baadhi ya marafiki hasa wale wasiopenda maswali yake yaani walikuwa wakikerwa na maswali yake. Mimi sijui walikerwa kwasababu gani, wao wanajua. Sasa mimi namfahamu kiasi dadangu Yasinta, jamani hapo ni kiboko ya maswali yaani jamaa anauliza maswali mpaka unaona hee huyu vipi? Ukweli mmoja ya waathirika ya maswali yake ni Mnyasa hapa lakini kawaida ya Mnyasa ni uvumilivu na utulivu ndiyo uliobaini kwamba uulizwaji kwake maswali ni njia yake ya uwasilishwaji wa urafiki tofauti na wengine walivyokuwa wakidhani. Jamani dadangu anamaswali mpaka unaweza kuungua utadhaniumeunguzwa na moto. Sasa huwa najiuliza vipi mjomba wangu Erik na Camilla watakuwaje? nikajikuta nimegota,nimeishiwa maneno ya kuwatabilia. Lakini maswali yake yanakufanya muda wote uwe unafanya kazi ya kujibu na usipojibu heee umemkimbia au la. Jamani mimi nilivumilia na nimekubali kwamba kama alivyoandika ni kawaida yake kwahiyo naona poa tu. Habari ndiyo hiyo, kublogu/kuandika unachopenda

mwanamke auawa kwa kupigwa shoka

Na HAPPY KULANGA, SONGEA.

Watu wawili wameuawa kikatili katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wiki jana.Kamanada wa polisi Falhum Mshana alisema jana kwamba katika tukio la kwanza agnes Kabanda aliuawa kwa kukatwa na shoka kichwani na hawara yake aliyehamika kwa jina la Ally Makinda. Kamanda huyo alisema tkio hilo lilitokea oktoba 3 saa 3:15 usiku katika eneo la Majengo Kisiwani ambako Makinda alimkata mpenzi wake shoka na kukimbia.

Taarifa z akufa zilitolewa na Hassan Salum(28) mkazi wa majengo C ambaye alikuwa akipita nyumbani kwake na kuona mwili wa marehemu ukiwa katika uwanja wa nyumba ya Makinda. Alisema chanzo cha mauaji ni ugomvi uliokuwepo baina ya marehemu na mtuhumiwa, ingawa alisema hadi sasa polisi bado hawajui ugomvi huo ulisababishwa na nini. Lakini uchunguzi unaendelea.

Pili, KILOSA MBAMBA BAY.
MkaZi wa Kilosa katika mji wa Mbamba bay Meshack Ngalima(62) amefariki dunia baada ya kudondokewa na mwembe aliokuwa akiuka. Tukio hilo lilitokea oktoba 3 saa 5 asubuhi mwaka huu. Meshack alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo kidogo cha afya Mbamba bay alikopelekwa na mdogo wake kwa ajili ya matibabu.

October 07, 2008

weweeee mambo iko ukuuuuuu

jamani eti watu wa mjini nao wanabanjuka baharini. waone kwanza wanaogelea maji ya chumvi wakati kwetu maji salama kabisa

mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi......

na HAPPY KULANGA, SONGEA.
Mkazi wa Mpandangindo mkoani hapa (Ruvuma) Filbert Ndomba(17) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Songea kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 8.
Mwendesha mashtka Inspekta wa Polisi Patrius Mlowe alieleza mbele ya hakimu mkazi Joseph Fovo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo septemba 16 mwaka huu, saa nane mchana, katika maeneo ya Mpandangindo ndani ya manispaa ya Songea mkoani hapa.

Mlowe alidai kuw mshatakiwa alimuingilia kimwili kwa nguvu binti huyo na kusababishia maumivu makali ambayo yalimfanya apige kelele zilizomshtua mwenye nyumba pamoja na wapangaji ambao walikwenda ndani kwa kijana huyo na kumkuta amemvua nguo zote mtoto huyo na kumbaka.

Mshtakiwa amekubali kosa na kudai kuwa mtoto huyo alimfuata chumbani kwake ndipo alipoamua kumbaka. Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo oktoba ambapo hukumu itatolewa. Mshtakiwa alirudishwa rumande.

WAKATI HUOHUO, MBAMBA BAY.
Mkazi wa Mbamba bay Sevelina Komba(34) amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki isiyofahamika na kuvunjika miguu. Sevelina alikuwa akitibiwa katika hosptali ya wilaya ya hapa Mbinga, mkoani Ruvuma. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi(Happy Kulanga) mjini hapa,kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Falhum Mshana alisema tukio hilo lilitokea siku ya Idd Mosi, saa nne usiku katika maeneo ya hapa Mbamba bay.

Mshana alisema Sevelina Komba alifariki siku ya pili saa asubuhi katika hospitali ya wilaya Mbinga na kwamba aliymgonga hajafahamika baada ya kukimbilia kusikojulikana. Alisema mwili wa marehemu umezikwa jana na pia Polisi wanaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta aliyemgonga marehemu huyo.

uzuri+utulivumapenzi+upendo=karibuni nyasa

jamani maneno yanakwisha sasa nisemeje........... aaaah wapi nikose maneno. karibu nyasa jamani