October 15, 2008

malaya/umalaya+uzinzi/mzinzi+uasherati/msherati/chupi mkononi/kahaba/ukahaba=UKIMWI?

Jamani hii ni kampeni ya ONE LOVE, huku ndiko unaambiwa subiri/tosheka naye/acha ngono/umalaya/uzinzi/uasherati. yaani weka neno lolote lenye maana ya jamaa anapenda ngono. kampeni ya kuwaweka sawa vijana kwamba UKIMWI unaua au kuwa waaminifu(?) sijui nini na mengine kibao, lakini mnajua kwamba kondomu zipo? mnafanyaje pale mnapokula raha zenu nyie watu? mimi sijui sababu sijui lakini najua kuna watu akina chupi mkononi n.k aiseh mambo juu ya mambo.unapomwambia binti wa miaka 16 kwamba awe mwaminifu.atosheke naye/awe na subira hivi mna maana gani? semeni huo ukimwi ni kuonjana/kutakana/kubanjuka/kubanjuana/utamu/kunoga/asali/uroda? eeeeh kama hujui kufa angalia kaburi. Simama uhesabiwe vinginevyo kaa chini usahauliwe.ONE LOVE

kunyamba mwengaa/ uzuri jamani

October 14, 2008

kama ninge...... kama ningekuwa Nabii Mwalimu Nyerere

wale wanaoabudu dini zao wana manabii wao. Nami sioni soni kukuita Nabii wa kweli kwa imani ya kiafrika wala iyo wale waliozaliwa mashariki ya kati. Mungu wetu yu pamoja nawe. kama ningekuwa wewe .........
wamatengo hamyambu yambu

October 12, 2008

hamu+utamu+uzuri+utulivu=nyasa

smaki aina ya ngorokoro
korido za Mv Ilala ambayo hufanya safari zake toka Malawi-Tanzania. hii ni mali ya Malawi na yapili kwa ukubwa baada ya Mv Mtendele

October 11, 2008

ufukweni kijijini kwetu LUNDU

hapa ni kijijini kwetu LUNDU. halafu ukiangalia nembo ya LUNDU upande wa kulia utaona watu wanafurahi sana ni utundu mdogo. sasa hapa ndiyo kwangu yaani kijiji nilichozaliwa.karibuni msije mkaja na pombe hatutaki

ni maisha tu kwani nani anajali hali hii

mafisadi nao wanatumalizia kitoweo cha maendeleo