November 11, 2008

Je ni mapenzi yangu kuwa hali hii??


sijui jawabu, labda nimekosa thawabu
Hakika sina aibu, maisha ni yangu
Ni maisha yangu, ndiyo thawabu yangu
kamwe hiana si kwangu, nangoja adabu

Naishi kivyangu, siishi waishivyo
Moyoni furaha yangu, imani ilivyo
Furaha imedumu, haina kasoro
kuishi kudurusu, thawabu yangu

Salamu wenye heri, mola awarehemu
mioyo iwe buheri, nafsi zidumu
Moyoni sina huzuni,jirani usiniudhi
yangu yakuudhi, yako yanipa riziki?

Aghalabu sipigi kite, kwani mola ajua
mababu wasisikitike, moyoni natunza
imani isipotee, liwalo leo na kesho
faraja inikuze, upendo udumu hata mtondogoo

Wanipata ewe mwanadamu, sikio walitega?
akilize zidumu,ubongo wako umejaa
wanielewa ewe chakaramu, kesho unaogopa
sifazo ewe mwanadamu, itakupa malapa

ooh kwaheri ewe mnumanuma, ewe mpenda lukuma
alamsiki nakwambia, buheri na afya njema
sina hiana nakuga kwa pendo, iwe siku njema
siku ya upendo siyo mitego,iwe daima pamoja

Karibuni MBINGA, karibuni sana

kahawa yetu ni nzuri sana ARABICA itazame kwa makini uone uzuri wake. MBINGA kwa raha zetu

November 09, 2008

akili inachangamka sana + uzuri wake

hata kama iweje wala sitobadilika

nakupenda nyasa yangu

November 05, 2008

unakula, ulamba, unamung'unya, unadokoa=utamu tu

ukiwa na njaa sana usiibe wala usidokoe sema tukugawie. huyu maarufu kama LINGOVA samaki wanaopatikana zaidi wakati wa masika. watamu sana

Lini mliacha ubaguzi nawashangaa sana

acha niwashangae sana kwa kumchagua huyu jamaa ambaye mnadai waafrika hawana lolote? au kwakuwa mlimsomesha wenyewe? ninyi waafrika huku mnashangilia kuwazidi wamarekani nawashangaa sana? huyu atakuja kuwafundisha kuandika hotuba za Marais wenu? atawafundisha kuhusu kuwajibika na kushtaki wevi? Je unaposhangilia kumzidi Mmarekani mwenyewe unamaana gani??? poa lakini YES WE CAN, CHANGE HAS COME IN AMERICA. hONGEREA sana ewe mwana wa mvuta tumbaku wa KISUMU i love u so much my brother maana ile kujiamini kwako kumenipa somo kali au vipi Obama mwanawane
PAMOJA DAIMA

kunoga tu