November 15, 2008

hatuchoki tunataka haki sawa hapa siyo longolongo

SIWAOGOPI HAWA WENYE NYWELE NDEFU NA KUNENEPEANA KWA SHIBE ZAIDI, BALI NAWAOGOPA WANYONGE NA WENYE NJAA- Julius Caesar. Chuo kikuu kimefungwa shauri ya migomo ya kutoingia madarasani. Lakini hawa walionenepeana halafu wakashangilia kwa mikogo eti OBAM kashinda. Zinawatosha ninyi??? sheria za kikandamizaji ataondoa huyo? wizi wa mitihani ataondoa huyo kuweka meli za kuvulia samaki ataleta OBAMA, kwania ananihusu nini?? ninyi ndiyo milompigia kura??? mliomba kwa mungu, ina maana asingejaza fomu basi mungu angelimjazia ha ha ha ha ha ha ha ha

Chuo Kikuu sehemu ya Mlimani


Tanzani ni migomo, maandamano kila mara. Chuo kikuu kimefungwa na kampasi zake zote WANAFUNZI wamegoma. Tunahitaji mabadiliko siyo uongozi wa mazoea HAPA. UONGOZI UMEKWAMA, UMEELEMEWA WANABAKI KUONGEA MPAKA MKOROMEA YANAKAUKIWA MATE

November 13, 2008

kipindupindu kiingie ikulu


sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?

kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?

kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema

November 11, 2008

Je ni mapenzi yangu kuwa hali hii??


sijui jawabu, labda nimekosa thawabu
Hakika sina aibu, maisha ni yangu
Ni maisha yangu, ndiyo thawabu yangu
kamwe hiana si kwangu, nangoja adabu

Naishi kivyangu, siishi waishivyo
Moyoni furaha yangu, imani ilivyo
Furaha imedumu, haina kasoro
kuishi kudurusu, thawabu yangu

Salamu wenye heri, mola awarehemu
mioyo iwe buheri, nafsi zidumu
Moyoni sina huzuni,jirani usiniudhi
yangu yakuudhi, yako yanipa riziki?

Aghalabu sipigi kite, kwani mola ajua
mababu wasisikitike, moyoni natunza
imani isipotee, liwalo leo na kesho
faraja inikuze, upendo udumu hata mtondogoo

Wanipata ewe mwanadamu, sikio walitega?
akilize zidumu,ubongo wako umejaa
wanielewa ewe chakaramu, kesho unaogopa
sifazo ewe mwanadamu, itakupa malapa

ooh kwaheri ewe mnumanuma, ewe mpenda lukuma
alamsiki nakwambia, buheri na afya njema
sina hiana nakuga kwa pendo, iwe siku njema
siku ya upendo siyo mitego,iwe daima pamoja

Karibuni MBINGA, karibuni sana

kahawa yetu ni nzuri sana ARABICA itazame kwa makini uone uzuri wake. MBINGA kwa raha zetu

November 09, 2008

akili inachangamka sana + uzuri wake

hata kama iweje wala sitobadilika

nakupenda nyasa yangu