November 19, 2008
zana za kazi zipo mapumzikoni
November 18, 2008
zawadi ni zawadi usambe utajiri jamani
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha,
Nyasa,
urafiki,
wageni
November 17, 2008
kuvua dagaa usiku

dagaa wa ziwa nyasa ni watamu sana, wananoga mno, ukila unajiumauma tu hamu na kuzidi kunogea. SASA ukitazama picha hii utaona KARABAI zimefungwa mtumbwini, hapo ndipo kazi inafanyika kwani ukisha funga hivyo kazi inaanza kwenda kilindini na anyavu ya kuvulia kusaka kitoweo kunoga na utamu kuliko chochote..... ebu taja kitu kingine kitamu kuliko dagaa? najua utataja nanii....... nini ile ...... sijui ebu inaitwaje!!!! aahaa tuache, hayo. haya ndiyo mambo ya nyasa na zana zao
Madhumuni
falsafa,
kumbukumbu,
maisha,
mapenzi,
mengineyo,
mila na desturi,
urafiki,
uzuri,
wageni,
zana
kazini hakuna matata
Madhumuni
kumbukumbu,
Nyasa,
wageni,
zana
November 15, 2008
hatuchoki tunataka haki sawa hapa siyo longolongo
Madhumuni
kumbukumbu,
siasa,
ushenzi
Chuo Kikuu sehemu ya Mlimani
Tanzani ni migomo, maandamano kila mara. Chuo kikuu kimefungwa na kampasi zake zote WANAFUNZI wamegoma. Tunahitaji mabadiliko siyo uongozi wa mazoea HAPA. UONGOZI UMEKWAMA, UMEELEMEWA WANABAKI KUONGEA MPAKA MKOROMEA YANAKAUKIWA MATE
November 13, 2008
kipindupindu kiingie ikulu

sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?
kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?
kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani
kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani
ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema
Subscribe to:
Posts (Atom)

