November 25, 2008

Je wajua kuhusu mimi?

Najua natamani kuumbwa nyoka ningevua magamba milele nisingezeeka, kwani nina ujanja nabasti mama Pancha. Lakini...... Nakupenda ndiyo maana nilikutaka, tulitakana, tukapendana na kuelewana. Najua miezi imepita hadi leo tumedumu lakini uchungu nilionao ni kukupoteza wewe ninayekupenda. Sina wa kumlilia ila wewe naomba unielewe, nakupenda sana usidhani nafanya dhihaka. Kicheko changu kinaficha mengi nazuia simanzi,sipendi kuonewa napenda kupenda lakini sijapendwa lakini nakulilia wewe uliniependa kwa dhati hilo najua nami nasema nakupenda ndiyo maana nakubembeleza. Hivi nini kinatutenganisha? nini kinachokusibu mpenzi wangu? kosa langu ni hilo tu, hakuna jingine? nani kakudanganya mahabuba wangu, nani kakwambia maneno au akili ya kuniacha? Ni kosa hilo tu unaniacha, ni hilo tu ndilo unakasirika kiasi hicho? nimekosa mbele za mungu na kwako pia. Nakupenda kuliko unavyodhani eti sikujali. Siyo mimi niliumbwa hivyo siyo kwamba sijali ila nakujali tatizo kwangu ni kujipa malengo na kanuni. NAKUPENDA SANA MPENZI WANGU amini nakuambia njoo tuvue samaki, tulime mihogo na mengine NISAMEHE au niambie nifanye nini ili unisamehe MACHOZI YANATOKA hakuna wa kunifuta. RUDISHA MOYO WAKO ili TUANZE UPYA, MAPENZI MAPYA, MIPANGO MIPYA
Akupendye Daima: Mnyasa wa Nyasa na Mvuvi wa samaki hodari
MARKUS MPNGALA

moja ya mtaa hapa Mbinga

November 23, 2008

karibu tunakula, sijui utakifurahia chakula chetu..

hebu tazama nyuso za walaji hawa, watazame kwa umakini kisha sema mwenyewe wapo katika hali gani. Kuna jambo unalojifunza? Inakufikirisha kidogo? Tunahitaji kuanza upya mapinduzi? JIKOMBOE SASA, UHURU DAIMA.

November 21, 2008

alaah kumbe wavuvi nao wanaofisi zao, kumbeeee


mnyasa naye yupo

November 20, 2008

Mwl Klayson karibu sana Nyasa


Nasema sana KARIBU NYASA

November 19, 2008

zana za kazi zipo mapumzikoni