December 01, 2008

mauzo ya kondomu

Mara nyingi napenda habari mpya zenye vituko ambavyo vinanipa kazi ya kutafakari lakini sipendi vituko au habari za kunichosha ingawa sichoki mwili akili inagota.

SASA: Mauzo ya Kondomu huko Korea yamepnda sana tokana na watu hususani vijana wadogo kujihusisha na utamu wa ngoma ya kikubwa NGONO. Mauzo hayo ni kwa mujibuwa Dk Janet Hyde aliyefanya utafiti katika jamii za watu wa Korea toka chuo kikuu cha Wiscons. Anasema wingi wa Runinga, pamoja na mhusiano mabaya ya wazazi majumbani ni mambo ambayo yanaaminika kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana wa umri mdogo.

Wengi wanaangalia vipindi ambavyo vinaashiria au kupandisha mzuka kama siyo midadi ya ngono na hawavai kondomu. Lakini hivi karibuni utafiti unaonyesha kondomu inanunuliwa sana tu ili kujiburudisha na majambozi ya kiutamu utamu!!!! Vijan wengi ni wale wadogo wenye umri wa miaka 13 na 15 ambao anadai wameshafanya ngono kama siyo kufaidi utamu huo katika umri mdogo. Mauzo yameongezeka sana kipindi hiki kuliko ilivyokuwa awali:Na maadili yamekuwa mabaya sana siku hzi huko KOREA

HIVI ndivyo vituko, lakini nafikiri unaweza kuwaza jambo. JE JAMII ZA KITANZANIA ZIPO VIPI? VIPI WALE WAPUMBAVU WANAODAI UTANDAWAZI huku hawana lolote katika utandawazi wenyewe? Je utandawazi hauna maadili? PAMOJA DAIMA!!!!!!

zawadi yako dada YASINTA

Ngoja nikupe zawadi nzuriiiiii sana dadangu kwani umenifanyia kazi nzuri katika blogu yangu. Hebu tazama hapo hilo ua vipi, ni kwaajili yako dada Yasinta na familia yenu yote.ASANTE.

November 30, 2008

usafiri wetu niyo huu

November 27, 2008

unapofurahia kunywa, ujue na kushughulika

naam mambo shughuli za kulima kahawa. hapo ni suala la kukausha si mnajua tunakausha kwa njia za asili au mnafanyaje ninyi.

November 26, 2008

ndizi ndizi KAPOLOTA karibu sana

wale walaji wa ndizi KAPOLOTA karibuni. Dada Yasinta huko ughaibuni unazikumbuka hizi

BREAKING NEWS: inaendelea.......

Kila mtu amesikia kuhusu mashtaka ya mawaziri wa zamani wa serikali ya Mkapa, bwana Dani Yona na Basil Mramba. haya ndiyo mashtaka dhidi yao.

BASIL MRAMBA
( alikuwa waziri wa fedha katika utawala wa Rais Benyamini Mkapa)
ANASHTAKIWA KWA MAKOSA YAFUATAYO:
1.KUISABABISHIA SERIKALI HASARA.
2.KUDHARAU MAPENDEKEZO YA TRA(mamlaka ya mapato)KUTOTOA MSAMAHA WA KODI
KWA KAMPUNI YA MS/STEWART YA UINGEREZA OKTOBA 10 2003 ALITOA NOTISI YA SERIKLI YENTE NAMBA 423 MWAKA 2003.
3.OKTOBA 15 2004 ALITOA NOTISI NAMBA 424 DESEMBA 19 2003 YA MSAMAHA WA KODI KWA KAMPUNI HIYO.
4ANATUHUMIWA KUTOA NOTISI YA SERIKALI NAMBA 497 MWAKA 2004 OKTOBA 15 ILI KUOTOA MSAMAHA WA KDI KWA M/S ALEX STEWART KINYUME NA MAPENDEKEZO YA TRA.
5.NOVEMBA 15 2005 AKIWA MWAJIRIWA WA SERIKALI ANATUHUMIWA KUTOA NOTISI YA SERIKALI NAMBA 377 YA 2005 KURUHUSU MSAMAHA WA KODI KWA KAMPUNI YA STEWART.
6.ANASHTAKIWA KWA KURUHUSU KUSHINDWA MAJUKUMU YAKE NA KUSABABISHA HASARA KWA SERIKALI SHILINGI 11,752,350,148.
7.ANATUHUMIWA KUTOA NOTISI NAMBA 423 NA 424 MWAKA 2003,NAMBA 497 NA 498 ZA MWAKA 2005 AMBAZO ZILIISAIDIA KAMPUNI YA ALEX STEWART KUTOLIPA KODI NA KUISABABSISHIA SERIKALI HASARA
8.DESEMBA 18 NA 19 MWAKA 2003 ALITOA NOTISI NAMBA 423 YA MSAMAHA WA KODI KWA KAMPUNI
HIYOHIYO

DANIEL YONA
(alikuwa waziri wa nishati na madini utawala wa Mkapa)
1.KUACHA UDHIBITI WA MADINI UFANYIKE KIENYEJI BADALA YA KUPELEKA KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
2.UZEMBE NA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA KAMA KWA BASIL MRAMBA.
3.KURUHUSU KAMPUNI YA M/S STEWART NA KAMPUNI TANZU YA M/S ALEX STEWART(ASSEYERS) GOVERNMENT BUSINESS CORPORATION KUSAINI UCHIMBAJI MADINI.
4.MATUMIZI MABAYA YA OFISI WAKIWA WAAJIRIWA WA SERIKALI.
5.KUTIWA SAINI KWA MKATABA WA NYONGEZA WA MIAKA MIWILI KWA KAMPUNI YA M/S STEWART KATI YA JUNI 14, 2005 HADI JUNI 23 JANA KINYUME CHA SHERIA ZA MANUNUZI YA UMMA NA SHERIA ZA MADINI.
6.MRAMBA NA YONA WANATUHUMIWA KUTUMIA VIBAYA MADARAKA YAO KATI YA MACHI 2005 NA MEI 2005 KUMWALIKA DK. ENRIQUE SEGURA WA KAMPUNI YA M/S STEWART KUKAMILISHA NYONGEZA YA MKATABA KABLA YA TIMU YA SERIKALI HAIJAANZA KUFANYIA KAZI SUALA.

NB; waungwana si mnakumbuka Mramba alisema tule NYASI ili ndege ya Rais inunuliwe, ha ha ha ha wala siwahurumiii. Na huyu Yona si ndiye aliyenunua Kiwira goldmine pale Kyela. hupajui? pale njia panda kituo cha ushirika.
ITAENDELEA ..............BREAKING NEWS USISHANGAE MNYASA NAPATA WAPI..... DUNIANI HATA UKIOGA BAFUNI TUNAKUCHUNGULIA TU..

November 25, 2008

Je wajua kuhusu mimi?

Najua natamani kuumbwa nyoka ningevua magamba milele nisingezeeka, kwani nina ujanja nabasti mama Pancha. Lakini...... Nakupenda ndiyo maana nilikutaka, tulitakana, tukapendana na kuelewana. Najua miezi imepita hadi leo tumedumu lakini uchungu nilionao ni kukupoteza wewe ninayekupenda. Sina wa kumlilia ila wewe naomba unielewe, nakupenda sana usidhani nafanya dhihaka. Kicheko changu kinaficha mengi nazuia simanzi,sipendi kuonewa napenda kupenda lakini sijapendwa lakini nakulilia wewe uliniependa kwa dhati hilo najua nami nasema nakupenda ndiyo maana nakubembeleza. Hivi nini kinatutenganisha? nini kinachokusibu mpenzi wangu? kosa langu ni hilo tu, hakuna jingine? nani kakudanganya mahabuba wangu, nani kakwambia maneno au akili ya kuniacha? Ni kosa hilo tu unaniacha, ni hilo tu ndilo unakasirika kiasi hicho? nimekosa mbele za mungu na kwako pia. Nakupenda kuliko unavyodhani eti sikujali. Siyo mimi niliumbwa hivyo siyo kwamba sijali ila nakujali tatizo kwangu ni kujipa malengo na kanuni. NAKUPENDA SANA MPENZI WANGU amini nakuambia njoo tuvue samaki, tulime mihogo na mengine NISAMEHE au niambie nifanye nini ili unisamehe MACHOZI YANATOKA hakuna wa kunifuta. RUDISHA MOYO WAKO ili TUANZE UPYA, MAPENZI MAPYA, MIPANGO MIPYA
Akupendye Daima: Mnyasa wa Nyasa na Mvuvi wa samaki hodari
MARKUS MPNGALA

moja ya mtaa hapa Mbinga