December 06, 2008

njoo unangoja nini, mwenzio nafaidi

wageni tu jamani hata wenyeji poa karibuni. haya mwangalie na huyu naye

maandalizi ya Noeli, karibu

kambale bwana, unakumbuka utamu wake? kwa wale wasiomla poleni huyo ndiyo kambale toka BABU hadi Mjukuu wanakula. ERIK UMEWAHI KULA KAMBALE WEWE? mwambie mama asiwe na roho mbaya hivyo akutafitie huko Uswidi , mkikosa njoeni nyasa

December 05, 2008

alaaah! sina kipaji cha kupenda, sikujua hayo

Aghalabu ni ningelijua lakini hakika sijijui labda kwakuwa sijui ndiyo maana nipo hivi. Nakupenda ndiyo maana nilikuja mbele ya wazazi wako, ingawa hawajui wanajua sisi tunafahamiana na marafiki. Sasa kivipi ilikuwa vile jakamoyo ukaijenga ulikuwa ukighadhibika? mbona hukusema, ingawa mara chache ulinena? hukusema kama unajua sina kipaji cha kupenda sasa mbona najua hilo kama sina kipaji? Poa sina simile wala sipigi kite kwani najua WARINA asali hawajui utengenezaji wake, wao HURINA tu hawajui mweka SEGA ni nani. Sasa najua sina kipaji cha kupenda unatakaje? nitembee kama nani, niige za ughaibuni hapana! tena thubutu bwana. Sasa nifanyeje ingawa najua kwamba unanipenda lakini ile tarehe milele sitoisahau daima itakaa moyoni kama simanzi ulotaka kunipa. Dunia ni nini? mbona wanipa majonzi huku wajua nakupenda? Nashukuru umenisamehe lakini swali langu, KUMBE SINA KIPAJI CHA KUPENDA? alaah kwanini hukuninong'oneza? mbona ulikuwa kimya ukadai wanipenda, nashangaa hata mungu anatakaa kujifanya muumini wakati una zigo la madhambi? au kujiona bora mapenzini, acha dhihaka, kweli ndivyo nilivyoumbwa siwezi kujibadili au nisake kipaji kama RONALDINHO maana wahenga walisema WA MBILI HAVAI MOJA au tusemeje AOMBAYE KIGAE AWE NA CHAKE? sijui ila asante kunisamehe ingawa niliuchukia mwezi Novemba. Alaaah kumbe sina kipaje cha kupenda?????

December 04, 2008

kwa watu wangu wa BIA na ULANZI

naam kwa watu wa toka nyasa mpaka mjini, wote mliopo juu na chini ujumbe utafika. wale wangu wa BIA kaka Simon na dada Yasinta yaani wapenda BIA naona huu ulaji ndiyo zenu sana? ha ha ha najua wanywaji hapa kwetu wanaita KAPILI hasa wale samaki waitwao NTAKA na vipande vya KAMBALE. ooooh kuna wale wapenzi wa kufakamia misosi ya kwenye sherehe basi hii ni ZAWADI yenu ila wale wanywa BIA wangojee yao.

December 03, 2008

nawapenda Kingoli na Litumbandyosi, lakini poleni

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo makali imeleta maafa makubwa katika kijiji cha KINGOLI kata ya LITUMBANDYOSI iliyopo wilaya ya MBINGA. Upepo huo umeezua mapaa ya nyumba TISA. Akizungumza kwa masikitiko Afisa mtendaji wa kijiji hicho Aloyce Nchimbi alisema mvua hiyo ilinyesha kwa zaidi ya saa moja na kusababisha baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi KINGOLIkutokuwa na mahali pa kusomea.
Mvua hiyo iliambatana na upepo mkali imeezua MADARASA MAWILI ya shule ya KINGOLI na NYUMBA mbili za WALIMU pamoja na majengo mawili ya ZAHANATI ya kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya MBINGA Amina Masenza amesema kamati ya kushughulikia tukio hilo imeundwa na itafanya kazi mara moja

NB; waungwana poleni watani zangu na watu wangu wa mkoa wetu PAMOJA DAIMA

nimeirejesha tena hii kumbukumbu


nimeipenda hii picha, sijui labda naifikiria sana na kuyaelewa mazingira yetu ya hapa nyasa. Lakini kuna jambo nalifikiria kuhusu mazingira haya na nyuso za wavuvi wenzngu.Waangalie vema unaelewa nini??

December 01, 2008

mauzo ya kondomu

Mara nyingi napenda habari mpya zenye vituko ambavyo vinanipa kazi ya kutafakari lakini sipendi vituko au habari za kunichosha ingawa sichoki mwili akili inagota.

SASA: Mauzo ya Kondomu huko Korea yamepnda sana tokana na watu hususani vijana wadogo kujihusisha na utamu wa ngoma ya kikubwa NGONO. Mauzo hayo ni kwa mujibuwa Dk Janet Hyde aliyefanya utafiti katika jamii za watu wa Korea toka chuo kikuu cha Wiscons. Anasema wingi wa Runinga, pamoja na mhusiano mabaya ya wazazi majumbani ni mambo ambayo yanaaminika kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana wa umri mdogo.

Wengi wanaangalia vipindi ambavyo vinaashiria au kupandisha mzuka kama siyo midadi ya ngono na hawavai kondomu. Lakini hivi karibuni utafiti unaonyesha kondomu inanunuliwa sana tu ili kujiburudisha na majambozi ya kiutamu utamu!!!! Vijan wengi ni wale wadogo wenye umri wa miaka 13 na 15 ambao anadai wameshafanya ngono kama siyo kufaidi utamu huo katika umri mdogo. Mauzo yameongezeka sana kipindi hiki kuliko ilivyokuwa awali:Na maadili yamekuwa mabaya sana siku hzi huko KOREA

HIVI ndivyo vituko, lakini nafikiri unaweza kuwaza jambo. JE JAMII ZA KITANZANIA ZIPO VIPI? VIPI WALE WAPUMBAVU WANAODAI UTANDAWAZI huku hawana lolote katika utandawazi wenyewe? Je utandawazi hauna maadili? PAMOJA DAIMA!!!!!!

zawadi yako dada YASINTA

Ngoja nikupe zawadi nzuriiiiii sana dadangu kwani umenifanyia kazi nzuri katika blogu yangu. Hebu tazama hapo hilo ua vipi, ni kwaajili yako dada Yasinta na familia yenu yote.ASANTE.