Utamu wa raha ni heshima, upendo na amani. Wawili huwa kama kumbikumbi na wengine hujiona kama JOTO na PANGABOI. Ndiyo Joto hupozwa na Panagaboi. Na yule umpendaye hakuna MWISHO haijalishi kama yuko mbali,karibu,jirani. Utamu wa roho na kupenda kwa moyo heshima ni kigezo kwani hata MOYO wako hunena kwa raha. Nikupe nini mziwanda wangu, KUMBIKUMBI wangu au nifanye nini ewe PANGABOI wangu? Moyoni najua naumia lakini naamini hakuna mwisho kwani NAKUPENDA. Najua kila MAWIO na MACHWEO hakuna MWISHO wa Penzi letu. Niambie basi nifanye nini,nikupe nini je niandike ujumbe mfupi kwako kila sekunde?Basi nina JOTO nawe ndiwe PANGABOI wangu nipulizie upepo nipe ubaridi ili nipunguze HARARA, wajua naandika huku nina simanzi? wajua kama ninasambaratika? Ooooooh nipe JOTO nikupe PANGABOI. Njoo basi tuongozane kama KUMBIKUMBI na MAPENZI yetu yadumu. HAKUNA MWISHO WA PENZI.Akupendaye mnyasa mvuvi mahiri, mkulima satadi na mtafuta FARAJA kwako. MWAAAAAAAAAAAAAAAH
mimi Markus Mpangala wa kijijini.
NB; Asante dada Yasinta kwa Picha hii. PAMOJA DAIMA!!



