December 22, 2008

Nimerudi, Nimepona jamani


Ni saa 1 na dakika 10, naadika haya haraka haraka {angalia picha kutoka ugonjwani hiyo}. Nimepiga maana kaka Fadhy Mtanga anasema wanyasa hatujui kupiga picha ha ha ha ha ha. Nimerejea jamani baada ya kuwa kando kwa siku kadhaa maana apangalo maulana hakuna wa kulizuia, malaria yanibana sana nikashindwa hata kufanya mazoezi ya kukimbia kama dada Yasinta {much respect sister. Malaria yalinifanya niwe kama mwehu muda wote nachukia. Nawashukuru walionipa faraja na kunijulia hali yangu, msijali sana PAMODA DAIMA, dada Yasinta asante na wengine, kama jina lako halipo hapa naweka ....................... ili ujaze jina lako. Watu wangu wa nyasa maanake naona walidhani jamaa kaacha blogu. Sivyo waungwana siwezi nasema siwezi maana blogu kwangu ni TULIZO LA MOYO mmm najua mtakumbusha mashairi niliyokwisha kuyaimba hapa jinsi ninanyomzimia mtu fidodido ha ha ha ha ha. bila kumsahau rafiki yangu mkubwa Fita Lutonja, Redrose Janeth {we belong together} mola akulinde zaidi

December 17, 2008

naipenda sana picha hii

dada Mary Mbunda akiwa katika shughuli za nyumbani. Yuko pale Lituhi kwa rafiki yangu mkubwa RAYMOND NDOMBA {much Respect Brother} najua tupo pamojadaima kama samaki na maji au mizizi na ardhi Mkuu

maneno ya Al-rawahy hilal

"Hi, Brother, Nimefurahi zaidi kwa ushindi wa Taifa Stars. Hongera kubwa kwa Taifa Stars na JK na WADAU WOTE WA BLOG YAKO, Hongera Bongo na watanzania wote popote walipo mimi ni mdau mkubwa wa blog zote za Bongo, napenda kufuatilia na kujua habari zote, nakuomba kama ndugu upost furaha yangu hii na hongera zangu hizi kwa wadau wote kwa ushindi mkubwa wa kuingia fainali za kombe la afrika, Tunaombea zaidi Stars wafanye vizuri katika michuano hiyo kila la kheri amin"
http;//www.borntosuffer1.blogspot.com
hilal24356@yahoo.vom

NB; ujumbe huu ulitumwa nyasa desemba 14.2008 kwahiyo waungwana wote Raha na shangwe kwa ushindi wa Stars

December 16, 2008

yote maisha+ipo siku yatakwisha.....

karibu sana wala usiogope ndugu, karibu nyumbani maskani wala usitie shaka. hapa ndiyo nyumbani karibu sana

tunasaka kitoweo cha Noeli hii

nadhani haya mambo toka babu na bibi mpaka mjukuu anatumia tu hakuna matata. jamani hebu waangalie mazingira yao ya kazi, yanakufikirisha? mimi sijui bwana