December 27, 2008

karibu nyumbani Yasinta, nina HAMU

duuuh unajua kwanini huwa naandika sana kuhusu huyu mtu? usiulize wewe pigia tu mistari au vipi. Ni jambo jema sana kukukaribisha tena nyumbani,kunyumba, hakika ni raha sana. Nashukuru pia kwa muda wote ambao umetumia katika shajara/blogu yako maana kuna kipindi ulikuwa katika mawazo sana kama siyo MAWAZONI, ndiyo maana nilisema nitafungua MASHTAKA iwapo ungeacha kublogu. Leo nafarijika namna unavyofanya kazi njema na kuibua mada motomoto ambazo hufikirisha. Hata hivyo naamini kutokuwapo kwako hewani ni kwa muda mfupi nina hakika na naamini utarejea tena baada kula DAGAA NYASA weeeeeeee karibu kunyumba bambu likolo la manyungu, mbulika, magege,kitimoto,ULANZI, komoni, myakaya na mambo mengi sana. Karibu nyumbani jamani maskani palipali pa mfaranyaki au kubombambili mmmm kuruhuwiko kwa Matetereka? haha ha ha nina raha sana maana nyumbani ni nyumbani, wale DAGAA wamefanya kazi sana maana najua mate yamekujaa mdomoni leo. KARIBU NYUMBANI dada Yasinta lakini kumbuka mashtaka yangu ukiacha kublogu tu yapo palepale!!! Erik a.k.a spite boy + Camilla a.k.a baby boom karibuni nyumbani. PAMOJA DAIMA

Dada KOERO karibu ndani !!

Jamani eeeeeeeeeeh, sina neno ila karibu sana tena sana dada KOERO, hakika tutajenga mnara katika miamba. hakuna jambo rahisi kama kuifanya nafsi ifurahia kile unachokiona kinafaa daima. Ni jambo ambalo kila mtu anaweza kulitenda ikiwa tu anaongozwa na dhamira imara lakini ni uwezo wa kuyabadili mazingira yetu kwa wakati wetun ndiyo huu ni WAKATI WETU, TUNAWEZA HAYA TWENDA NA DADA KOERO. KARIBU NDANI katika SHAJARA wengine mnasema BLOGU poa tu.

Ni mimi Markus Honorius Mpangala mvuvi wa nyasa na mnyasa wa nyasa.

December 25, 2008

wanablogu karibuni ndani

aaah si mmezoea kwenda disko, gesti ******, baa, kilabuni na mambo kadhaa kuhusu raha zetu? jamani siye tunawakaribisha hapa, ndiyop starehe zetu hizi na kipindi hiki cha sherehe za kila mwaka. wanashajara za mtandaoni karibuni ndani. Lakini kama huwezi sema tukusaidie

December 24, 2008

waambie ROHO yangu nzuri, AMA ZANGU AMA ZAO

nashangaa wananichukia bila sababu, sijawatendea madhambi lakini wananitumia ujumbe wa simu wataniua, eeeh ongezeni juhudi sitoacha kundika kile ninacho amini tena mimi mfuasi wa MALCOM X, kwangu Martin Luther King jr siyo shujaa! naamini hivyo licha ya kukubali umahiri wake, napenda ukali wa X kwani unaonyesha msimamo siyo kupewa sifa za upole na ustaarabu, waambie ROHO ni nzuri kuliko picha. Sijawatendea madhambi nashangaa wana chuki, wanataka kunihukumu, wamefanya kikao cha kumaliza roho yangu, nasema niueni anza hata sasa mimi sitishwi kwa ujumbe mfupi wa maneno ya simu eti sitowezi kuzuia kifo, eti wataniua kwsababu zao sijui nilichowakosea lakini SITISHWI na mtu yeyote wambie AMA ZANGU AMA ZAO hiki ni kima changu ama chao iwe mtaani maskani au mahali popote pale, kwani dunia nzuri kama picha hii hutoa taswira upendo na nafasi zetu. Waambie upendo wangu haupo kwa maadui, ndiyo kwani naogopa KUFA labda sijazaliwa waambie tena na tena ukiona uzuri na upole wa picha hii utadhani hakuna SHARI. Anzeni basi, kwani HATARI KITU GANI?

kazi+kumbukumbu

ninakumbuka enzi zile tukilima mpunga, ekari kibao na shangazi yangu pale Ngindo, yaani ilikuwa tka asubuhi saa moja hadi saa kumi na moja jioni. Duuh kwa mwendo wa kuchoka na kulegea kila kitu. nipumue siku hizi huuuuuuuuuuuuuuuuuu nalima kwa kompyuta

December 23, 2008

bongo yako inafanya kazi au siyo!!!!!

Siyo kila NDIYO kiundani maanake kuna NDIYO zingine huambatana na utani, isiwe bendera fuata upepo halafu kesho unakosa mwelekeo!!!! unafikiria nini unapotazama hii picha kwani wewe "hoteli" yako ipoje nyumbani, je ni kama hii???? naacha sisemi mengi

December 22, 2008

Nimerudi, Nimepona jamani


Ni saa 1 na dakika 10, naadika haya haraka haraka {angalia picha kutoka ugonjwani hiyo}. Nimepiga maana kaka Fadhy Mtanga anasema wanyasa hatujui kupiga picha ha ha ha ha ha. Nimerejea jamani baada ya kuwa kando kwa siku kadhaa maana apangalo maulana hakuna wa kulizuia, malaria yanibana sana nikashindwa hata kufanya mazoezi ya kukimbia kama dada Yasinta {much respect sister. Malaria yalinifanya niwe kama mwehu muda wote nachukia. Nawashukuru walionipa faraja na kunijulia hali yangu, msijali sana PAMODA DAIMA, dada Yasinta asante na wengine, kama jina lako halipo hapa naweka ....................... ili ujaze jina lako. Watu wangu wa nyasa maanake naona walidhani jamaa kaacha blogu. Sivyo waungwana siwezi nasema siwezi maana blogu kwangu ni TULIZO LA MOYO mmm najua mtakumbusha mashairi niliyokwisha kuyaimba hapa jinsi ninanyomzimia mtu fidodido ha ha ha ha ha. bila kumsahau rafiki yangu mkubwa Fita Lutonja, Redrose Janeth {we belong together} mola akulinde zaidi