January 05, 2009

Gumzo letu na dada Yasinta

Jamani natumaini hamjambo woteeeeeee wa kijiwe cha maswali magumu. Nipo kamili tena nazidi kuwakilisha kama kawaida.
Nadhani wengine mlikuwa mnangoja kujua labda tulipiga gumzo gani na dada Yasinta. Bila shaka mambo ya wanablogu yanafurahisha sana na utamu wa mashairi kama kaka Fadhy poa sana.
Katika kupiga gumzo na dada Yasinta, kuna jambo amenifanya nitafakari sana na wakati mwingine huwa najiuliza nianze vipi.

Gumzo la kawaida kuhusu mambo ya teknolojia, blogu na maisha kama ilivyoblogu yake. Jambo lenyewe linahusu VITABU. Nilimkuta kashika kalamu ya wino anaandika, nikauliza kulikoni mwenzetu huchoki? Akatabasamu na kusema 'kutafakari jambo muhimu lazima uandike ukizingatia kuandika ni jambo muhimu pia". Hapo gumzo likazama kuhusu vitabu maana kama ajuavyo napenda kuandika vitabu kuhusu jamii yetu.
Lakini alikuja na swali hili: "Kwanini huandiki vitabu kama unaweza? Si ni jambo la kukaa na kutafakari tu kisha unaandika kwa uamkini?akaongeza, Au hakuna soko la Vitabu? Basi andika vitabu vya wototo, haiwezekani?"
sijui kama mnanielewa ninachotaka kukisema? Ni jambo la kujiuliza sna katika jamii zetu kwani waandishi wa vitabu wanapotea, wengi waliopo wanaandike vile ambavyo vinadumu kwa muda mfupi.
Ni vigumu kupata vitabu kama RAI YA JENERALI, MAKUADI WA SOKO HURIA achilia mbali vile vya Issa Shivji{mwaka jana katoa Pan africanism or Pragmatism?} kizuri. Kwa kweli dada Yasinta kanipandisha moli kama wamasai.
Ndiyo maana nilisema katika maoni yangu fulani kama Simon Kitururu anapaswa kuandika vitabu vya falsafa, Fadhy naye awe Shaban Robert wetu, mzee wa changamoto nye awepo, dada Koero kama vile kitabu cha THINK BIG{umekisoma?}, Bwaya, Kaluse, Kalama tuleteeni UTAMBUZI wenu jamani. Ni hayo tu

January 03, 2009

Mandhari na Maudhui

Uzuri, Maudhui na Mandhari ya maeneo ya milima ya kaskazini mwa mbamba bay. yaani toka maeneo ya Kilosa, Matenje, Kwambe, Ng'ombo, Chamate, Linda, na mengineyo. Miinuko na vilima

January 01, 2009

20009+ YASINTA+ Wanablogu


2009 Pamoja daima.Wanablogu wote Nawatakieni mafanikio mema zaidi.Na kudumisha maendeleo ya Blogu zetu.Nimefurahi zaidi kwani jana nilikuwa na mwanablogu dada Yasinta,na kupiga gumzo la hapa na pale.Anatuandalia kitu kingine;tanzaniaresan2009.blogspot.com
NAWATAKIA SAFARI NJEMA.
ZIDUMU BLOGU ZETU na WANABLOGU DAIMA

2009 amani iwe nanyi kama MZEE WA CHANGAMOTO

Amani Heshima na Upendo kwako ndugu. Natumai kuwa u-mwema na unamalizia mwaka vema. Basi napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa mchango wako wa namna moja ama nyingine katika nyanja hii ya blog. Uwepo wako ni muhimu sana na kwa hakika tunajifunza mengi. Natumani (pamoja na wana-changamoto wote) kuwa mwaka ujao utakuwa mwema zaidi na tutaendelea vema katika ile nia ya KUIELIMISHA, KUIBURUDISHA NA KUIKOMBOA JAMII YETU kwa kadri ya uwezo wetu.
Heri ya mwaka mpya wa 2009 toka CHANGAMOTO YETU BLOG.

Salamu zako zipo http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/12/happy-new-year-bloggers.html

"www.changamotoyetu.blogspot.com"

December 31, 2008

Wanaopuuza shauri yao


nimesoma maoni ya Koero katika shajara/blogu ya Bwaya kuwa wapo wanaotazama blogu kama upuuzi. Nimefarijika kuona dada Koero kawagundua watu hawa lakini anawashangaa wanasoma mambo ambayo wanasema ni upuuzi. Namshukuru kwa kuwabaini LAKINI naomba uwaaambie blogu siyo upepo wa kupita, hii ni hatu nyingine zaidi ya kusoma magazeti na kuangalia luninga. Hapa hatuhitaji wahariri wakuu wala waandamizi bali nidhamu imejenngwa na mtu mwenyee. Kwa hakika watu tunajikuta tunafanya mambo ya ajabu lakini kujipa muda angalau kufanya jambo linalokufanya uwe bize na kuepusha porojo za hovyo LAKINI watu wengine hawaelewi. Jamani nia yangu ni kwamba pamoja na kwamba wanasema ni upuuzi ambao wanausoma lakini wajue kuwa blogu siyo upepo. Nashukuru dada Koero amegundua hilo maana kuna watu ukiwaeleza hili jambo wanaona kama ujinga fulani, eeeeh shauri yao wanaopuuza tunajua hawaamini kuwa wasomaji wanaweza kuwa wahariri na wahariri wanaweza kuwa wasomaji. Hivi huamini tunaishi zama zingine za teknolojia? Wape maneno yao dada Koero asante kwa kutukumbusha wanaopuuzia blogu/shajara shauri yao.

December 30, 2008

wazee wa kazi ndiyo zetu

tunavua hivi na tunafanya hivi kama tupendavyo. kazi ipooooooooo