23 January 2009

Asante Mkodo Kitururu

Nikiwa mawazoni, huku na kule, mara hapa na pale jamani kichwa chaniuma. Mnyasa nitakuwa safarini kidogo, nikapumzike sehemu zenye baridi. Siyo siri kaka Simon Mkodo Kitururu falsafa zake zanipa matumaini na ukweli wa maisha. Najua kuwa na akiba ya ya maumivu ni nzuri sana kwani ipo siku utalipiwa nayo.
Katika kuwaza na kuwazua, nikakumbuka Koero Mkundi na maoni yake kuwa maua yapo mtaa wa Samora, lakini alijua kuwa naugulia UA langu halipo tena nami. Najua kaka Mkodo kasema unaweza kutokea kwa mlango wa mwingine, mwenzenu nilijua haya mambo binafsi lakini naona bora kusema tu ili nipewa mafunzo. Nakumbuka niliususa mlango wa Canada, nikauvunjilia mbali kwa mikogo, nikasema mahaba ya kitasha basi, eti sasa duuuuh majonzi na kilio tu, inakuwaje?.

SASA hakika najua wanablogu tuko pamoja kama samaki na maji, mizizi na ardhi. Nashukuru mafunzo uliyonipa kaka Mkodo Kitururu, ingawa Koero alikuwa mwoga (anaficha nini?), kaka Fadhy Mtanga asante kwa shairi linipalo "Johari ya Matumaini" kama kitabu cha Barack Obama.
ASANTE kaka kwa Akiba ya Maumivu, nimeielewa mkuu, na hata ile ya Penzi la Pua na Kamasi, ni kweli kumpengesha mtu kamasi za penzi nako kunahitaji uwiano lakini uwiano huo hata kama unamizani za tufani,lazima lifike pwani. Naacha kwanza nimechoka kidogo ndiyo maana najipa likizo naenda mkoa wenye baridi ukanipe nguvu za ziada.
Dada Koero naomba unichagulie wimbo basi nijipumzishe kwa raha.

3 comments:

  1. Sikiliza huu wa Ziggy Marley:

    LOVE IS MY RELIGION.........

    ReplyDelete
  2. Asante ndugu yangu, nadhani nimepumzika vya kutosha huku nikiweka akiba ya maumivu. si unajua penzi la pua na kamasi alivyosema kaka mkodo? iko poa kabisa ile

    ReplyDelete

Andika maoni yako