30 January 2009

Nimeibukia wapi? usiwaambie uhamiaji

Duh! nilidhani nikiwa katika linchi la watu nitapata muda wa kutosha, lakini kumbe jamaa kaniandalia ratiba ya kuzurura kama chokoraa??? Yaaani mara huku mara kule.... Halafu jana nilikuwa napekuliwa mpaka nguo za ndani..mmhh hujui chupi wewe au? Unajua nilikuwa nawaza sana mambo ya kuzamia lakini sikujua kama nitakamatwa(natania).
Basi katika mambo ya hapa na pale, nilikuwa kwanza pale Zimba baada ya kutoka kalonga. Mwendo ukiwa umekolea hadi kwa mwenyeji wangu nikaona jamaa limenuna ghafla halafu linaniuliza... ujinga "eti huku hakuna safari lager wala kilimanjaro, kwahiyo nijiandae kunywa pombe zao za Kuchekuche" Nakwambia nilibadilika na kuwa mwekundu ghafla hadi jamaa likashangaa. Kama kuna kitu sitaki nasema sitaki narudia sitaki kukitia mdomoni ni POMBE!
Mmmh samahani. jana wakati narudi nilibishana sana wale jamaa wa uhamiaji eti kwakuwa niliwaachia kitambulisho cha maktaba na kile cha lotto kitita cha akiba!
Nikaa nimejinafasi katika mgahawa mmoja hivi ili kutumia huu mtandao, eti jamaa wanakuja na kusema oyaa MTZ mbona unanunanuna? Nikaona wanasengenya kinyanja wakidhani sijui! Nakwambia nilipayuka kwa lugha hiyohiyo halafu wakaomba msamaha, duh!
Ngoja kuna jamaa hapa kando linachungulia lugha ya kiswahili, linanicheki toka nyayoni mpaka kwenye bichwa langu. Nimeliuliza we jamaa vipi? tena kwa lugha yao,limeshangaa na kuchekacheka.
Mmmh leo narudi tena kwa uhamiaji kuchukua vitambulisho vyangu vya Lotto na maktaba, aiseh asikwambie mtu, waafrika hatupendani wakati mwingine duh!
Ngoja mwenyeji wangu Mark Wood na Sonny Banda wananiangalia pia niandikacho, huku nimekunja uso kama nimekula pilipili. Eti jana walinipelaka kunywa kuchekuche na nyama choma. Sitaki kusikia kulewa hapa! Kwaheri kwanza!
wakati naendelea kuandika kuna toto la Kitasha limeingia lipo pembeni hapa, Duh! Toto limeiva limefunga kanga kama wabongo. Halafu linachungulia, nimelikonyeza kijicho, likaachia meno 32 nje, hiyo ndiyo salamu bwana. Mmmmmh ebu mcheki yupoje? Aiseh mmmmhh na BARIDI ya Mbeya nikikumbuka??????? halafu linaandika kwa spidi kali sana.

6 comments:

 1. Hivi ulikuwa wapi?
  mara mbeya, mara kalonga nchini Malawi!
  Mbona hueleweki?
  Ok nasubiri zawadi za Samaki aina ya Kamongo, ole wako usilete!!!11

  ReplyDelete
 2. Koero);
  nipo nipo na nimerudi. Ni hivi nilikuwa Mbeya, lakini nikaingia hadi pale jirani kwa kamuzu banda tena vijijini bwana, kuna washakaji Mark Wood na Sonny Banda, hawa jamaa wanaendesha utafiti wa madini, kwahiyo ni watu wangu sana.
  Lile toto la kitasha halafu nilipokumbuka baridi ya nilipokuwa Mbeya DUH!
  UMENSOMA SASA, nimezurura klama chokaraa

  ReplyDelete
 3. mkuu ,habari,za siku nyingi?
  kaka niko huku kaka
  www.ringojr.wordpress.com

  rasta hapa kaka.

  ReplyDelete
 4. Nilikuwa na wasiwasi utadakwa uko na ndoa ya mkeka!:-)Mashehe hawakuwepo nini maana nasikia wasiokunywa pombe wanavilevi vyao ambavyo havihitaji hata kuvaa nguo:-)

  ReplyDelete
 5. Duh! Simon! sijadakwa bwana, unajua kule wengi ni wakristo bwana, HALAFU hii ya vilevi inawezekana kuwa kweli maana mmmmmh yapo sijui yanaanzaje lakini yapo yapo kwanza toka zamani

  ReplyDelete

Maoni yako