06 February 2009

Katika kuwaza na kuwazua, ni kama nalamba mchanga gizani halafu sichafuki. Nawaza mengi kila nijionapo, maana najiona mimi kwani yanagusa maeneo niliyokulia.
Niliwaona wengi, nikawaringia kwakuwa nyumbani tunakula ugali kwa uma na visu, nikaringa ati tunakula mezani, halafu tulala mkekani. Hapo sijakwambia kitanda cha Demu wangu mmoja cha Teremka tukaze . Nakumbuka nilivyokuwa kikojozi hadi mama ikawa kila siku makofi, nakumbuka dingi alivyokuwa mkali utadhani mwandamizi wa jeshi la Hitler.
DUH! nakumbuka enzi zile tunakunywa chai (tunaita Chingambu) bila sukari ya Mtibwa, enzi za kula viporo vya ugali wa muhogo na dagaa usiku wa manane halafu tunajiona wajanja. Nakumbuka mengi niwaonapo wenzangu kama hawa, nawaza wakati ule tunalala kwenye mkeka tuliokojolea.
Nakumbuka mama alinipa adhabu ya kulamba sehemu niliyokojolea mkojo, nakumbuka jinsi nilivyokuwa nimebuka vumbi sababu ya soka langu. DUH! niwaonapo hawa najiona mimi, japo kwangu afadhali vipi wale wakuangalio kama hawa? Nakumbuka mengi sana sana sana sana nashindwa kunena zaidi EEH! Mola tuonyeshe Nuru

No comments:

Post a Comment

Maoni yako