18 February 2009

Tunaweza kuishi bila Penzi au Mapenzi?

Tuishivyo ndivyo tufanyavyo. Na kama tufanyavyo ndivyo tuishivyo basi tunaweza kuangalia mwenendo wa maisha yenyewe. Sina hakika kama kuna tofauti kati ya PENZI na MAPENZI, maana inaweza kuwa kinyume kinyume halafu nikapotosha maana. Unampenda mtu, una hamu naye, roho yako inapwita,inahamanika,inachezhceza lizombi.

Sijui unajichukuliaje unampenda mtu fulani, au unataka penzi la fulani maana wapo wasemao nataka penzi lako bilakujiuliza kama umwambiaye naye anahitaji penzi lako au la! Unaweza kuhitaji penzinla fulani lakini kwa tafsiri ya haraka penzi ni ngono na kupeana utamu uupedwao. Lakini wapo wanaosema au kulalamika katika ndoa zao kwamba hawatosheki. Lakini ukiuliza hawatosheni nini wanasema PENZI bila kutoa ufafanuzi kwamba penzi wasilotosheka ni ngono au nini.

Inawezekana ukawa mmoja wapo kwamba ukasema mpenzi mbona leo umechemsha au umemaliza mapema? Lakini kila siku unalilia penzi ambalo unasema ni tofauti na mapenzi. Sijui inawezekana kuwa tofauti lakini HAMU ya kutaka penzi la mwenzako inatokana na nini? Na kama kweli utamu wa penzi ni ndoa, inakuwaje wengine wanarejea penzi lao la kwanza eti wamekumbuka UTAMU wa kale mavi ya kale hayanuki.

Kwanini uingie kwenye ndoa halafu usijiulize ndoa ni nini? Ikiwa utamu wa penzi ni ndoa na wale wanaoshikana mikono kwa raha na kuambatana kila leo kama kumbikumbi na kusema MAPENZI matamu au Penzi ni tamu wanapata wapi utamu ambao siyo halali hadi uhalalishwe kanisani na msiikitini eti sasa mnaweza kufaidi PENZI mtakavyo, kwani awali hamkufaidi mtakavyo na kujua utamu wa Mpenzio upo mahali gani au ukimtyekenya shemu fulani inampagawisha na kuelgea kama mlenda wa BAMIA?

Utakuta tunaweza kupenda kupendwa na kutamani au kunogea kufanya PENZI ambalo siyo tendo la ndoa mpaka lihalalishwe na wawakilishi wa imani. Ni imani gani unajua kama mpenzi wako ni bomba sana kwani PENZI akupalo ni lile litokalo Ghana au Nigeria? Inawezekana utamu huu ni sawa kama ule wa mnyasa na yule demu mkanada awawzaye umasikini wa waafrika. Je kwanini wengine wanataka penzi la dada zao na kaka zao au binamu nyama ya HAMU?

1 comment:

Andika maoni yako