03 March 2009

Penzi, Mapenzi na Thamani ya Mtu

Unajua au umewahi kunisikia napenda, napendwa au nataka kupenda? Daima nashangazwa na mwelekeo wa upande mmoja. Mara nyingi utaona iwapo Mwanaume anamtongoza mwanamke, kuna vitu vinamwongoza hadi kufikia hatua hiyo. Inaweza kuwa tamaa yaani anahamu ya kualala na mwanamke ( kuchungulia UVUNGUNI). Usishangae jina la Uvunguni maana ndiyo maneno ya waungwana na mabadiliko ya tafsiri kwamba ni UVUNGUNI kati ya mwanamke na mwanaume wanapofanya kile wanachoona kitamu zaidi wakiwa SIRINI.

Jambo linalonishangaza ni hulka za wanawake kudai kwamba kuna wanaume wanaotongoza ili kuwachezea wanawake au kuna wanaume wanaotongoza kwa nia ya kuwachezea. Sijui undani wake lakini si haba mambo haya kusikia. Utasikia 'unanipenda kweli au unataka kunichezea tu? Lakini ukitafsiri dhana ya kuchezea ni pana kwani hakuna asiyemchezea mwenzake kwa namna yeyote ile hasa suala la mapenzi.
Wapo watu wanaona kwamba dhana ya kuchezea ni upofu tena nikiwamo mimi. Suala la kutongozwa halafu unasema anataka kukuchezea, kwani wewe humchezei mtu hata kama unaye katika uhusiano wa mapenzi?

Unaweza kubeza lakini najiuliza kwanini wanawake wanajiona wanathamani kuliko wanaume katika suala la kutongoza au kutongozwa? kwanini wanasema wanaume wanataka kuwachezea na siyo kudumu nao mapenzini? Kwani hakuna asiyemchezea mwenzake? Utona kwamba baadhi ya wanawake wanasema kabisa 'Mi nimechoka bwana, yaani unataka kunichezea hadi niweje?" Hili tunaweza kusema kwa wale ambao tayari wanachungulaina uvunguni.

Lakini kwa wale ambao wanatakana, wanahitajiana, wanataka kuanzana, yaani wanatongozana huku wengine hasa wanawake wakichukua muda mrefu kukubali ombi la kutongozwa. Hivi dhana ya kumchezea mwanamke ilianzaje, tulifikaje hapo? Kuchezewa nini hasa ambacho kina thamani kuliko utu wetu? Nini thamani ya penzi au mapenzi? Na nini kinachokamilisha mapenzi? Wengine mtasema SIYO LAZIMA TO DO? lakini ukiona watu wanajifanya hawapendi kuchunguliana uvunguni eti siyo lazima, waulize siku watakayofanya kuna jambo jipya litakalo kuwa nje ya PENZI au Mapenzi? Kwanini wanawake wanajipa thamani sana katika mwili wao hasa suala la mapenzi? KAZI MNAYO WAUNGWANA, JIULIZENI.

5 comments:

 1. Hii sio kweli ya kwamba wanawake wanajipa thamani. Nasema hivvi kwasababu wewe unajuaje kama anajipa thamni. Na pia siku hizi wananume wengi wana nyumba ndogo kwa hiyo hii ndio sababu wanasema UNANICHEZEA TU.

  ReplyDelete
 2. Ni tamaduni tu!
  Ze kubembelezwa zinatokana na desturi la sivyo zingekuwa ze kubembeleza.

  Sehemu nyingine wewe ungetongozwa na kulipiwa mahari ili uoe. Nenda hata India ucheki mwanaume anavyolipa aoe.

  Wanawake wa Kibongo wanatoka katika tamaduni za kufuatwa katika shughuli na Jamii ni jaji kwa hiyo mwanamke wa Tukuyu mwenye nguvu ndio awezaye kukutokea Dar kukuambia Kidume nimekuhusudu ingawa mlikuwa naye Tukuyu na alikuwa hatakukuangalia hakuangalii.

  Na kunauwezekano akikubali kirahisi atakutisha kwa sababu unajua tamaduni kuwa akubaliye haraka labda hadumu.

  Mimi nimefanikiwa kuwa mtoto wa mwisho na na dada wawili. Kuna kipindi mpaka nilikuwa nastuliwa na wanadada kuwa huyu kimwana anakupenda kwa sababu anaomba kuja kusukwa nywele wewe tu ukiwepo na ukianza zako anaenda saluni.Na mwanadada hanisemeshi ingawa nikigusa maharage nakuta ni ya mbeya kwa kitu kila mtu alisema lazima uyaloweke usiku mzima kabla hujapika. Ila naheshimu wanadada ambao wanaelewa tofauti ya wachezeaji na wapendao kikweli ingawa kuna mchezo wa Vidume kuwekwa kwenye jeduali moja.


  Kumbuka vimwana wanatoka sayari nyingine na vidume sayari nyingine katika swala la kuelewa hata la Birthday lini!:-(

  Lakini wanawake wana thamani ndio maana labda umeandika hii hot topic.

  AU?
  Samahani kwa mcharazo. Napita tu Mkuu!
  Tuko pamoja!

  ReplyDelete
 3. Wanaume wana mambo!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 4. natoka nje ya mada.

  mzee wa nyas, uliandika sana juu ya raha ya kujamba ukiwa peke yako.

  naomba uandike pia juu ya kama ni raha au nini sijui ya kuharisha ghafra ukiwa ugenini, kweni, safarini ofisini nk

  natuamini ommbi langu utalifanyia kazi kwa moyo wote ukijihadhari na harufu.
  bye

  ReplyDelete
 5. Yasinta! Soma kwanza ile mada ya kaka Kaluse halafu utaniambia hdna ya nyumba ndogo ni nini na inachangiwa na nini! Kimsingi najua kwasababu naona na kujifunza mara nyingi. Naona kwani wanawake wanadhani kwamba miili yao ina thamani kuliko hata jicho walilonalo wakati ni sehemu ya mwili. Lbda nakosea lakini pengine mnahitaji hoja ili tuelezana ukweli wa mambo.

  Koero najua unashangaa kuhusu UVUNGUNI lakini siyo mimi niliyenazisha bali nilichofanya ni kuwasilisha tu kwani nimeskina na kushuhudia wakiesma hivyo wenye kujua utamu wa uvunguni.

  Kaka simoni nimekulewa na ndiyo hoja tunazozitaka na kuelishana zaidi

  Kamala L; kaka jambo hili nahitaji muda usidhani siwezi kusema nitasema kwani kuna jambo nilishuhudia hakika ni noma lakini inabidi Koero aseme kitu maana ana vioja vingi sana vya namna hii.

  ReplyDelete

Maoni yako