02 June 2009

NYAZODE, ndiyo hii hapa sasa

Katika mkutano wetu wa jumapili ya jana kumefanyika jambo amabalo nimelifurahia sana. Kilichofanyika ni kuendelea kujitokeza hata wale ambao hawapo vyuo vikuu, bali hata kama yupo katika shughuli zake ilimradi tu anahusika na nyasa kwa kupitia elimu aliyoipata pale UNDO sekondari, kwahakika mambo ni mazuri.
Rasimu ya katiba inaandaliwa, kuwakaribisha wanachama yaani wanaoweza kutoa mawazo yao au kujumuika nasi katika lengo hili.

Sasa ni NYAZODE# hii ni NYASA ZONE DEVELOPMENT GROUP, tumebadili jina hilo ili kila anayejiunga asione yupo katika mkusanyiko bali yeye ni mwanakikundi ambaye anahitajika sana. Suala la katiba, uongozi na mambo muhimu yamejadiliwa, yanamalizika sasa. Kikao kijacho ni kuiweka vema rasimu yetu ya katiba na, mpango wa kufungua akaunti ya akiba ya NYAZODE.
Hii itasaidia hasa pale tutakapopitia baadhi ya shule za sekondari kuangalia wanafunzi wenye matatizo ya ulipaji karo hapa nyasa, na kuwaangalia katika michango mbalimbali. Pamoja na kusaidiana sisi wenyewe kama wanajumuiya hiyo katika mambo mbalimbali. Tumekusanya wengi na tutazidi kuwaelekeza wengi pia.

Hakika tunaweza CHANGE WE CAN BELIEVE IN *YES WE CAN
Tunashukuru pia Bwana Kapinga kutuunga mkono katika jukumu hili, maana Waraka wa kwanza wa Petro 3# 3-4> anasema NAYE NI NANI ANTAKAYE WADHURU MKIWA WENYE JUHUDI KATIKA MEMA?

2 comments:

  1. Naona mambo si mabaya. Kwa kweli safi sana kuona mnataka kufanya mabadiliko. Haya ndipo maendeleo nawatikieni kila kitu kiende kama mlivyopanga. Mtafanikiwa tu. Pia ni nafurahi kuwa umerudi.

    ReplyDelete

Andika maoni yako