29 July 2009

KUMRADHI WATU WANGU+KARIBU

Nimekuwa kimya sana, hii ni kutokana na majukumu pamoja na shule, muda wangu unaliwa sana na hawa jamaa. Ukimya wangu hauna maana kwamba nimeitosa, ni jambo gumu sana kuachanba na blogu kwani ndiye mke wangu, ndiyo kipenzi changu, ndiye faraja wangu kwa maana kila nikitazama na kusoma maandiko ya kaka Fadhy Mtanga, huku Kitutruru na kule yuko Mzee wa changamoto, angalia mzee wa fikra pevu Bwaya, angalia utambuzi wa Nyegerage(ingawaje alisindwa kunijibu maana na neno hilo wakati wa semina za Freddy Macha) angalia kazi za Kaluse. Dada zangu Yasinta na Koero, yuko Nuru, Subi na wengine ............................. nimeweka deshi ili ujaze jina lako kwa maana tupo pamoja sana.

Nadhani wakristo wanaelewa pale katika kitabu chao cha Mithali kisemapo KUNA WAKATI WA KUNENA NA WAKATI WA KUNYAMAZA. Lakini mimi naweza kunena na kunyamaza, ila sasa tuseme vitabu vinamaliza muda wangu pia maana nimeamua kukusanya simulizi za JORAM KIANGO zote za riwaya za BEN MTOBWA. Tayari SALAMU TOKA KUZIMU na MALAIKA WA SHETANI nimekwisha kuvisoma kwakuwa zamaniu nilikuwa mdogo halafu sikutilia umakini, sasa nakusanya tu, na mwezi ujao nitajinunulia vingine viwili. Unadhani nimesahau utamu wa vitabu vya Prof Mbele? ebu tafuta ujionee mambo kama hujasoma.

Nachukua fursa hii pia kumkaribisha kaka Deogratius Ndunguru katika mambo ya nyasa, maana yamemkuna sana tena hadi akakumbuka Chimate na zile simulizi za mzee wake mashuhuri KANG'OMA. Pia jana nilikuwa na BAHATI LINGALINGA, furaha sasna kukutana na watu ambao tangu tukiwa wadogo sekondari na sasa wakubwa kibingwa.
Natumaini mtanisamehe kwa kutoonekana na sasa naahidi kurejea kiasi na nikipotea nitasema jamani mwenzenu nimebanwa au vipi waungwana? kumbukeni kuna wakati wa kunena na kunyamaza.

Lundu +nyasa= lundunyasa

3 comments:

  1. Tuko Pamoja Mkuu na nakutakia kila la kheri katika michakariko!

    ReplyDelete
  2. Kweli ulipotea kama shilingi ya mkolono karibu tena.

    ReplyDelete
  3. Nimefurahi sana kwa kujitokeza kwako. Karibu sana kaka. Nilikumiss.

    ReplyDelete

Andika maoni yako