06 July 2009

Kwa Ajili Yako Mpenzi

Jambo la kweli kuhusu ukweli ni kwamba ukweli UNAUMA. Kwakuwa unauma, na kwakuwa tunapenda UTAMU badala ya uchungu, tunapenda uongo mtamu kuliko ukweli mchungu. Kadiri uongo unavyokuwa mtamu zaidi, na kadiri tunavyoupenda zaidi ndivyo tunavyopumbaa. Zipo njia mbili ambazo kupitia hizo tunaweza kupumbaa zaidi. Kwanza ni kuamini jambo ambalo si lakwqeli na pili ni kukaa kuamini lilele la kweli.

Kuna mambo ambayo sipendi kuyakubali, laikini sitoweza kuyakataa. Kuna mambo ambayo sitopenda kuyakumbuka, lakini sitoweza kuyasahau. Na kuna mambo ambayo sitokuwa na uwezo wa kuyalazimisha, lakini sitakuwa na hiari nayo. Kwa muda mrefu umekuwa ukidhani unaweza, lakini kwajili yako mpenzi pokea nasaha zangu.Kama ni upendo wangu ni mkubwa lkakini sitoweza kujizuia kuvuruga amani yako, na kwakuwa napenda uwe na amani kwahiyo itakuwa vigumu kukuvura na upendo wako.

Na kwakuwa unapenda kuona upendo machoni pako, basi tarajia kuuona ikiwa utaleta upendo wako. Nadhani uliamua mwenyewe kuamua, lakini kama ulikosea kuamua na sasa unaona kama makosa hayo ni makubwa, basi tafakari kwanini uliamua huku ukiangalia hao wanao. Waone kwa upendo, watazame kwa amani na mabaya yote ya mumeo yasahau. Kwakuwa nilikuwa napenda uwe karibu yangu lakini ukaamua uliyoamua basi hakuna sababu ya kulalamikia uamuzi wako.

Unapaswa kuelewa hakuna binadamu aliyekamilika, na hata kama kuna mtu anadhani atakupenda zaidi ya unavyopendwa na mumeo hilo sahau kwani huo ni unafiki. Na kama kweli unadhani upendo wake upo kwako na ndiyo maana hadi ametoa talaka, hilo mimi siliafiki tena natumaini kwako litakutokea tu kwani kama amefanya hivyo kwa mwingine, je itashindikana vipi kwako? Na kama anakupenda hata kuamua kuvuruga ndoa yake ili akuoe wewe jaribu kutafakari kwa kina. Mimi nilikupenda na nakupenda, lakini uamuzi wako wa kuolewa ni jukumu lako, halikuwa langu.

Kama mwanamke mwenzio ameachwa eti kwaajili yako, je wewe ungependa kutendewa hivyo? Je wewe haliweza kukuta hilo? Na mwanzo mpenzio ulimpendea nini? Na kwanini uliniambia nikushauri kuhusu kuolewa wakati uliamua? Nakupenda sana naomba tulia na ndoa yako kipenzi changu. Mungu akulinde pokea UA.

Markus Honorius Mpangala
Mbinga-Ruvuma
Tanzania

2 comments:

Maoni yako