06 August 2009

NYAZODE, Kikao tarehe 9 Agosti hii

Ndugu zangu wananyasa na wengine, natumaini mko salama na mwenyezi hayuko mbali nanyi. Basi ni kwamba kile kikao kijacho kitafanyika tarehe 9 mwezi huu wa Nane, bila shaka tutakuwa pmaoja kwa kila hali, naamini kwamba kikao hiki ndicho kile ambacho kitaidhinisha wale wanachama wapya ambao siyo kwamba siyo wanachama bali wanajumuiya ya nyasa ambao kwa kila namna wanaguswa na hali ya huko. naamini kila siku mambo yanabadilika na mtazazmo unabdilika.

karibuni hakikufanyika kikao shauri ya mitihani ya baadhi yetu na majukumu ya hapa na pale. hata hivyo naamini kila kitu kinakwenda sawa na tutafanikiwa katika jukumu hilo. kama nilivyosema awali kuwa sisi ni watu tulioamua kufanya kile amabacho Wamrekani wamekuwa wakifanya kwa kukiita VOLUNTEER, na mara ya kwanza nilikiona pale Ng"ombo ambapo walikuja kufundisha mambo kadhaa kuhsu dini. nakiri wakti huo sikufahamu zaidi lakini sasa naona hakuna hata haja ya hao kuja kwetu tena.

Nakumbsha tu kwamba unaweza kuwasiliana na watawala wetu ambao wanajua kila jambo. nawashukuru wale walioniandikie barua pepe kuulizia jambo hili, kwakweli nawshukuru sana na natumaini kila kitu kitakuwa swa katika mstari wake. Naamini kwa pamoja tutafanikiwa na kuunda jeshi la mtu mmoja ambalo litakuwa na nia yenye manufaa zaidi.
Ni kwam,ba kikao hiki kitafanyika Mabibo Hostel, yaani hosteli za chuo kikuu cha Dar es salaam, na kama kuna madiliko basi tutafahamishana mapema. Jamani likizo ndiyo hiii na wengi wetu watakuwa katika ameneo yetu kama kawaida na tunafurahi tu kwamba mtazamo utazidi kupanuka.

KIBWAGIZO, hadithi za JORAM KIANGO bwana ni tamu sana. Nakumbuka enzi zile nilikuwa nikisoma juu juu tu katika gazeti la HEKO ama katika hadithi zenyewe. Lakini sasa nimeamua kusoma upyaaaaaaaaa yaani sitaki kupitwa maana najua sasa nimekomaa kweli kuliko wakati ni msingi, basi nimekusanya SALAMU TOKA KUZIMU, MALAIKA W SHETANI, NYUMA YA MAPAZIA na NAJISIKIA KUUA TENA.
Usifikiri nimemaliza hapo kwani najua nina deni la TUTARUDI NA ROHO ZETU, DAR ES SALAAM USIKU, ..................................... na vingine vyote vilivyoandikwa na hayati BEN MTOBWA.

jamani vitabu raha sana, halafu yaone maviongozi yetu yaliyopo madarakani kazi zao ni KUJAMBA NA KUJAZA VITAMBI MATUMBO MAKUBWA KAMA MABWAWA hawana hata kitabu cha kutusiulia japo jambo. mmmmmm samahani, HIVI umesoma vitabu vya Profesa Mbele? Mmmmmhhhh najua dada Yasinta ataanza na zake eti ndiyoooooooooo, haya bwana salamu zao hukoooo

1 comment:

  1. Mmmh wenge kyani! haya nene nijova lepe chinu lelu.

    ReplyDelete

Maoni yako