05 September 2009

Mara ngapi umesahau kutumia Kondomu???

Ndugu wanablogu na wasomaji wangu, niwaombe radhi kwa kutoweka hapa bila taarifa. Ukweli nilikuwa na hali mabaya kiasi, hali kiafya ilitetereka sana maana kwa muda mrefu sikuugua kama hivi. Malaria yalinibana sana kiasi ambacho nikashindwa hata kuandika ama kuwajulisha watu wangu, marafiki zangu. Lakini natumaini tupo pamoja na sasa nimerudi niko kamili na afya yangu iko salama hata leo nimeanza mazoezi ya viungo pia mdomdo. Mungu mkubwa, na nimewasoma wanablogu katika blogu zao kwa njia ya simu yangu ingawa sikuweza kuchangia lolote.

Tukiacha hilo, kuna jambo mara nyingi naliwazia kulisema nalo ni kuhusu matumizi ya zana ya KONDOMU. Nasema hivi kwasababu kuu moja, Mama yangu alipoanza kuniuliza swali hili ilikuwa mara nilipomaliza kidato cha juu. Swali hili lilitokana na kitu kimoja tu, kwamba kuna usiku fulani pale kwetu Lundu nilichomoka zangu usiku (ilikuwa mwaka 2005, mwezi Juni) na kwenda kujiburudisha na uvunguni kwa kutumia kionjeo cha utamu. Sasa.... asubuhi ilipofika akasema......Markus jana usiku ulikwenda wapi na kitandani kwako hukuwepo?.... nilibabaika...kwani ni kweli niliruka zangu ukutu kisha huyoooooo kwenye madogoli... si unajua kijijini ngoma za usiku na ahadi tutakutana ngomani???

Basi mama yangu aliniuliza kwa njia ya utani, na amekuwa akifanya hivyo mara nyingi siyo kwangu tu hata wadogo zangu ambao nao ni waelewa wa mambo. Baada ya kuona sijajibu nilikuwa wapi usiku ule... akasema sikiliza mwanangu...mara nyingi unakataa mambo ya ulevi na tabia ambazo hazipendezi ama hazikubaliki hata kama hazina madhara...lakini nakuuliza swali kwamba MARA NGAPI UMESAHAU KUVAA KONDOMU? Mama yangu alikuwa makini kwani muda wote alikuwa akinitazama usoni, na anajua kama sijapendezwa na swali huwa nanyamaza au kuondoka eneo husika kuliko kuonyesha ghadhabu zangu.

Kitu nilichofanya ni kumweleza Mama kuwa kweli nilitoka na anisamehe kwani nilikuwa ngomani. Na kuhusu swali lake nilimjibu kuwa NIMEMWELEWA. Lakini Mama akasema kuwa kama unadhani nakuingilia katika uhuru wako basi sahau kujiona uko huru kuliko uhuru wenyewe hata kama utakuwa kwako... nitaendelea kukuuliza swali hilo....najua hujaoa na naamini unaye mtu unauhusiano naye. Nikamweleza Mama inatosha nimekuelewa. Siri moja ni kwamba iwapo katika pilika za kutafuta kupata utamu kwa kutumia kionjeo cha utamu akijua Mama yangu kuwa ninayemchungulia uvunguni ni fulani basi ilikuwa lazima nisitishe na mahusiano yanakwisha hapo. Nilijifunza jambo!

Linaloshangaza wengi ni kwamba katika familia yetu suala la kupimwa ukimwi siyo jambo la kubembelezwa ni lazima na hakuna ubishi katika hilo. Sasaaaa.....niliposhindwa kumjibu Mama yangu kuwa kama nasahau kutumia ama kuivaa kondomu nilijua anamaana gani, na tangu hapo nilijiuliza kwanini Mama yangu alisema hivyo? Siyo kwamba sivai au situmii kondomu, la hasha nimeishaitumia mara kadhaa. Na kwakuwa sijachungulia uvungu kwa muda mrefu... daima nalikumbuka swali hilo na naelewa tatizo linalotukumba sisi vijana kubeba kondomu mifukoni lakini tukifika dimbani hatuwezi kuhimili kuzivaa vema au kujaribu kuvaa.

Ninaamini udhaifu huu unatoka na KUONGOZWA NA HISIA bila AKILI. Najua kuwa idadi kubwa ya wanawake wanakumbusha suala la kondomu wakiwa dimbani hata kama vichakani dakika moja kabla ya kuchimbana mitaro. Nasema hivi kwani sihitaji kusimuliwa nilifanya uchunguzi mwenyewe kwani enzi hizo baadhi yao wanakuuliza kondomu iko wapi? Halafu wanajifanya kususia mpambano usio na REFA wala washika vibendera. Tunapofikia hapo tunabembelezana kwa maneno ya YAANI HUNIAMINI? MIMI NATAKA NYAMA KWA NYAMA NIJISIKIE KUNOGA NA KUFAIDI UTAMU WAKO! AU NAKUAMINI DIA WANGU WASIWASI WA NINI ..... HAYA TURIDHISHANE BASIIIIII. Ona sasa..... wizi mtupu!!!!

Unaweza kudhani napenda porojo ama ninachosema ndicho ninachofanya bali naona na hata mimi mwenyewe enzi zangu nilikuwa nabeba hizo kondomu halafu namsikilizia MWALI wangu anasemaje kuhusu matumizi. Hapo ndipo nilipoonza kulidharau tendo lenyewe na kuona wanaotembea wakiringia uzuri na kile walichonacho kumbe bureeee! Ndipo swali linaporindima daima .. hata nikaweza kukaa kipindi kirefu zaidi ya mwaka mmoja bila kuchungulia uvungu sababu naona sioni jipya hata kama kuna watamu kama sukari ama asali. Kinyaa tupu,............... wizi mtupu!

Siku zote naona sisi vijana tulivyochakaramu wa kuhusudu kuchungulia uvunguni, lakini tunaposimuliana kwa umahiri wa matumizi ya kondomu, kumbe ni 10 kwa mmoja wanaotumia hata kama maambukizi ya ukimwi yamepungua. Najua kile tunachokifikiria pale tunapokaribia kuitafuna Mbunye (samahani kwa mcharazo mkali). Na siku hizi wale washikaji zangu wanawabatiza wanawake wakubwa wenye miaka kuanzia 20 na kuendelea eti klabu ya AC MILAN ya Italia kwamba wazee damu haina moto. Ndiyo maana wanasema kuna mafataki ya kiume, lakini mimi nasema kuwa mafataki ya kike yako mengi tatizo tu yanajifanya kuja kwa vituko na ishara....sasaaaaa jitu kama mimi nakutazama na halafu nikikufiria ukiwa huna nguo katika ule muda hata kama umevaa ujue nimeshakutupa jalalani. Hili ni jambo linalohitaji ujasiri ...siamini kwamba tunashindwa kumiliki akili zetu hata tukashindwa kuivalisha kondomu ile NDUDE iletayo utamu.,,.... kwani uwongo? mifataki inayoniandama...halafu ngoja nitapiga mtu ngumi za jicho... LoL.............

Niliwahi kuhudhauria mafunzo ya matumizi ya kondomu mwaka 2006, nakumbuka wakati semina inaendelea ukazuka mjadala nani awe anabeba kondomu na matumizi ya kondomu za kike. Siamini kuwa wanawake hawawezi kubeba kondomu ama kuzinunua na kuvisha vionjeo vyetu vya utamu.... na ni jambo la usikivu mkubwa vinginevyo tunacheza mchezo wa hatari. Ndiyo maana daima nakumbuka swali la Mama yangu kuwa mara ngapi umesahau kuvaa kondomu? Hapo kuna maana mbili, aidha umekuwa mzinzi kupindukia hata kama unatumia kondomu hizo AU unatakiwa kutumia kondomu pale unapokutana na MWALI wako katika mshughuliko wa kushughulika na kujipatia utamu kwa kutumia kionjeo cha utamu.

Tunaweza kujifunza mengi kwa kukabiliana na jambo hilo, tunaweza kuongozwa na akili zetu na siyo HISIA ambazo zinakufanya ujutie katika maisha yako yote. Na unaweza kuachana na tendo la kuchunguliana uvunguni siyo lazima ukaombewe na wenye itikadi kali na imani kali. Unaweza kuhamishia mapenzi yako katika vitu vingi tu ambavyo vinakusahaulisha kuwazia Mbunye au mguu wa mtoto....LoL... Haina haja ya kudhani kuacha kushiriki ngono ni tiketi ya kujichua bin PUNYETO kama wale WALIOFILISIKA MAWAZO wanavyotulazimisha kuamini ukiachana na mambo ya MTALIMBO basi utakuwa una jingine kando.

Naamini kidogo unaelewa ninachomaanisha kwani nikisemacho kinaeleweka sana na hakuna wa kubisha kwamba wengi kondomu inakuwa msamiati mgumu. NAKUULIZA WEWE UNAYESOMA HAPA BILA KUJALI UNA NDOA YAKO AU LA, JE NI MARA NGAPI UNAPOTOKA NJE YA NDOA UNASAHAU KUVAA KONDOMU? AU NI MARA NGAPI WEWE MWENYE MABINTI WASIOHESABIKA UNASAHAU KUVAA KONDOMU?

AMANI KWAO, AMANI KWENU, tuwe sote... sasaaaa usiseme nimekataza kuchungulia uvunguni kwani NENO LANGU SIYO SHERIA ila tu nakuusia......mimi nimelipuuza tendo lenyewe kwanza kisha watu wenyewe...lakini usiseme kuwa sitamani......bali NAONGOZWA NA AKILI SIYO HISIA! LoL...................

2 comments:

  1. Lugha uliyotumia ni sahihi sana sana, maana wengine wanajua kuvaa tu na walasio kutumia, unaposema kutumia maana yake ni kuvaa kwa usahii na kuzingatia maelekezo yote ya jinsi ya kujikinga na vvu wakati unafanya ngono (sio mapenzi)

    ReplyDelete

Maoni yako