10 September 2009

MNISAMEHE WATU WANGU, NIKIWAKOSEA

Najua uungwana ni vitendo ndiyo maana nasema hivi kwasababu kuna kipindi katika picha zangu za kuhusu wale jamaa wa RICHMONDULI a.k.a wakurichmondooooo kuwa nilikebehi imani ya wakristo. Naomba nieleweke kuwa sikukusudia kuwadhalilisha bali nilikuwa nawakilisha kuwa hapa tulipo kuna nini kwa wenzetu katika ulimwengu huu.

Kwahiyo kama waliokwazika na picha ile na hata wakaniandikia waraka pepe kuwa nimedhalilisha dini basi MNISAMEHE SANA nawaomba hilo. Vilevile kama kuna jambo nililoandika katika blogu hii limewakwaza na ambalo uandikaji wake siyo kwa nia ya mafumbo mafumbo na majungu ya muziki wa Taarabu naomba mnisamehe sana kwani siyo lengo langu katika blogu hii.

Pia kuna wale wanaoghadhibishwa na mwenendo wa blogu yangu wa polepole naomba mnisamehe sana kwani nawaheshimu wasomaji na wadau wangu LAKINI naipenda sana shule na wala sina haja ya kushika chupa za BIA ama misokoto ya akina LoL......... najua mnaokwazika mnanifundisha jambo. NAJUA pia nifanyalo ni kwa burudani za watu a nyasa na wanablogu wengine wahusuduo blogu yangu. NAWASHUKURU KWALO. jambo moja ni kwamba naweka tu kanuni kama nilivyoweka awali, naweka tu kwani naamini ni utaratibu wangu bila kujali ukaribu na umbali wetu.

Naomba wanisamehe woteeeee niliowakwaza kwa kuweka habari au gumzo ambalo kwa namna moja ama nyingine limewakwaza. Nachukua fursa hii kuwaambieni hivyo kwani maisha yangu siyo ya kuigiza na wala mimi siyo mwigizaji mzuri kama JORAM KIANGO katika MALAIKA WA SHETANI cha Ben Mtobwa anavyotuasa kuwa watu wanaigiza- maana huwezi kucheka na mtu ama kujifanya unazungumza naye mengiiii kwa raha na burudani za hapa naple halafu PEMBENI unafundo la GHADHABU. Naomba mnisamehe kwa yote nimejifunza- nitaendelea kujifunza mengi toka kwenu wanablogu na wasomaji wengine. Naamini kutenda kosa siyo kosa ila kurudia kosa. Nakiri makosa kwa yale niliyowakwaza wenzangu.

Pia wale walioniomba kuhusu kuweka matangazo katika blogu yangu, nitawajbu leo. Kwamba blogu yangu sihitaji tangazo la mtu la kibiashara ama lenye mlengo wa kufanya ubepari/biashara bali blogu yangu inajitolea kwa matangazo ya wale wanaohangaikia maisha yao kama nilivyofanya kwa VUNGA. hayo n aina ya matangazo niwekayo. Tangazo la kahawa ya Mbinga ni kujitolea kwangu kwani nilikwisha kuzungumza na mabwana wa pale na wakanielewa.
Blogu yangu haifumbi mtu na wala siyo ya ukoo wa akina HONORIUS MPANGALA bali ni kijana mpole tu Markus Honorius Mpangala na wala hatumii FALAKI ili aweze kuishi na kutambua makosa yake.

AMANI KWENU, TUPO PAMOJA NAWAPENDA NYOTEEEEEEEEE, KARIBUNI NYASA

1 comment:

Maoni yako